Adai Kikwete alikabidhiwa mapema ripoti ya Richmond Asema kama kumuokoa ni yeye aliyepaswa kufanya hivyo
Selii alizima ndoto za Rostam na Lowassa baada ya kuanika ushiriki mzima wa wanasiasa hao wawili katika mkataba huo. Akiongea kwa kujiamini na kuchambua hoja moja baada ya nyingine,
1. Selelii alisema Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mkataba wa Richmond ambapo yeye alikuwa mmoja wa wajumbe wake inaoushahidi kwamba Richmond ni mali ya Rostam.
2. Kwa upande wa Lowassa, Selelii alisema alibeba kampuni hiyo kwa maslahi ya binafsi ya rafiki yake huyo.
3. Selelii alisema "Rostam amewadanganya kwa kusema hahusiki na Richmond."
4. "Huyu Rostam ndiye aliyetafuta nyumba kwa ajili ya matumizi ya ofisi ya Richmond. Ni yeye aliyelipia pango la nyumba hiyo," alisema Selelii huku akitolea macho Rostam.
5. Alisema, "Kamati yetu ilihakikishiwa na mtoto wa Mucadam (Hussen Mucadam) ambaye ndiye mwenye nyumba kwamba nyumba iliyotumiwa na Richmond ilipangwa na Rostam."
6. Selelii alisema "hata jopo la waadishi wa habari lililofanya kazi ya kusafisha Richmond lilitafutwa na Rostam."
7. Alisema Rostam alifikia hatua ya kutumia waandishi hao wa habari mara baada ya vyombo vya habari kuanza kueleza utata wa mkataba.
8. "Ni huyu Rostam aliyekodisha jopo la waandishi wa habari watatu mashuhuri nchini kwa ajili ya kupoza makali. Tumezungumza na waandishi wa habari hawa mmoja baada mwingine na wote wametuthibitishia hili," alisema Selelii.
9 Alitaja hata majina ya waandishi hao kuwa ni Gideon Shoo, Jimmy Mdoe na Salva Rweyemamu ambaye sasa ni mkurugenzi wa mawasiliano ya rais.
10. "Kama hahusiki kwa nini aliwatafuta hawa waandishi wa habari? Kwa nini aliwapa kazi," alihoji Selelii.
Alisema mbali na waandishi wa habari na utafutaji wa nyumba, Kamati Teule iliweza kuthibitisha kwamba baada ya Richmond kuhuisha mkataba wake kwa Dowans, wafanyakazi watatu wa Caspian walionekana katika Dowans.
11. "Kwa maana nyingine, Dowans, Richmond na Caspian ni baba mmoja mama mmoja." Alisema Kamati Teule imepata ushahidi kwamba "fedha za Dowans zilihamishiwa katika akaunti ya Caspian; Rostam alikuwa akifuatilia mwenyewe fedha hizo hazina," alisisitiza Selelii.