Seleman Kidunda usituangushe, leo mchape Katompa ili kulinda heshima ya Jeshi na nchi

Seleman Kidunda usituangushe, leo mchape Katompa ili kulinda heshima ya Jeshi na nchi

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Pambano la ngumi (VITASA) kati ya Seleman kidunda (JWTZ) na Katompa kutoka DRC ni Leo!

Ikumbukwe katompa miezi michache nyuma ndiye aliyemchapa Abdalla Pasi (dullaboy)

Kwa kutambua uzito wa Bondia Katompa RAIA kutoka DRC, ambaye kaja tena kupigana akiwa na ujumbe kutoka "jeshi la Kongo" Kwamba Jeshi la Kongo limemtuma KATOMPA Aje kumrudisha KAMBINI mwanajeshi wa kitanzania aliyepotea njia kuingia ulimwengu wa Masumbwi.

Hivyo kwa kutambua ujumbe huo! Wakuu wa Jeshi watafuatilia pambano Lako Leo Jioni!

Unabaraka za Jeshi kupambana, una baraka za inchi ya Tz, una faida ya mbinu za kivita, una mafunzo ya uvumilivu, una mbinu za kimedani, Unawakilisha nembo ya Jeshi, Una mafunzo mazuri hata kumchapa K.O

Ukikubali Kupigwa leo ni sawa na kumwangusha chini "JENERALI"

Itoshe kusema Ukipigwa na kurudishwa kambini na Raia KATOMPA, Hakika utambue kambi imejaa majani, Itabidi UFWEKE MAJANI kuzunguka Kambi nzima.

Updates
Leo ni Leo tena! Pambano linarudiwa uwanja wa majimaji songea 30 July 2022, Lazima mshindi apatikane songea hakuna mbeleko Leo mtu mzima anapasuka!
Bila kusahau mzee wa mikwara mandoga mtu kazi na Kaoneka!

Nani zaidi?
 
Aah ssana italazimika afyeke tu, lakini namkubali kwa kiwango kikubwa Selemani Kidunda hana maneno kama ya mstaafishwa Dulla Mdhaifu, hiyo mbabe ishapotea siku nyingi tu
 
Katompa yupo vizuri kuliko Kidunda mimi ni MTanzania napenda boxer na nimfuasi wa boxer kuliko hata Football nimemuangalia sana Katompa ni boxer mwenye maarifa sana hakamii ana hold temper vizuri ana organize ubongo wake kwenye kurusha ngumi zake.

KIDUNDA UMRI SIJUI KACHOKA NA MAZOEZI MI HATA SIELEWI.Anyway natamani tulipe kisasi ili ile aibu ya kutoka kwa Abdalah Pazi ifutike.
 
Hii ya leo ni moto sana Kidunda akidundwa Leo cjui ataiweka wapi sura yake maana pambano la juzi alionesha uwezo na boksa yake iliochakaa Leo asiivae au ndo ndagu yake?

Ivi na katompa ni Mjeda uko kongo? Mwisho wa yote atakaeshindwa leo ataandaliwa pambano na Twaha apo ndo vitaumana

Sent from my KISWASWADU using JamiiForums mobile app
 
Hii ya leo ni moto sana Kidunda akidundwa Leo cjui ataiweka wapi sura yake maana pambano la juzi alionesha uwezo na boksa yake il

Sent from my KISWASWADU using JamiiForums mobile app
Katompa tunamtengenezea CV tu hapa Tanzania alitakiwa akutane na TWAHA KIDUKU faster baada ya kumchapa ABDALAH PAZI kumpa Kidunda nikumuongezea CV tu kutuchapa waTZ
 
Sio mfuatiliaji sana wa masumbwi ila leo nataka niingie hapo ubungo plaza nishuhudie game.
 
Katompa tunamtengenezea CV tu hapa Tanzania alitakiwa akutane na TWAHA KIDUKU faster baada ya kumchapa ABDALAH PAZI kumpa Kidunda nikumuongezea CV tu kutuchapa waTZ
Maneno yako kama ninayakubali japo Kidunda ana techniques za kutosha, yote kwa yote tusijinyong'onyeze tunaweza kushinda
 
Back
Top Bottom