Uchaguzi 2020 Selemani Bungala (Bwege) asema Magufuli hakushinda kihalali. Atolea mfano wa aliyoshuhudia katika vituo viwili jimboni kwake

Mwandishi mchokozi sana kamuuliza "kwa hiyo watanzania mtafanya nini" dah nasikitika hili swali limekosa jibu
 
"Nyie watu wa Rufiji mna matatizo badala mchague Mbunge unachagua Bwege ,Bwege atawasaidia nini badala ya kuleta ubwege maana naona hapa hakuna alichofanya hata kujenga choo tu cha stand kwa pesa za jimbo ameshindwa "by JPM
Wewe kukoment hapa tu hukutumia fedha zako bali za Lumumba,unawezaje kuwa na ujasiri wa kusema unachosema?
 
Tunawataka Mawakala wa CHADEMA walioshuhudia watupe hizo Nakala, tuchukue kama sample tuone kama Lissu alishinda mbona tunaandikia mate na wino upo, mfano wa Bwege unaonyesha still JPM aliwin 70/67 .....zingine ni bla bla
Unge elewa maana ya free and fair usinge andika huu upupu
 
Mwandishi mchokozi sana kamuuliza "kwa hiyo watanzania mtafanya nini" dah nasikitika hili swali limekosa jibu
Hajasema watamzania na jibu kalitoa kulingana na sheria zilizopo ...
 
Hapa kuwa na uchaguzi ilikuwa ni aibu tupu ya taifa
 
Lete wewe idadi yako sasa kama kura hazikufika 10M una uwakika gani ? Usikute hata kura hukupiga unabwabwaja tu hapa Jf ! Tatizo lenu ninyi mnafikili kura zinapigwa humu Jf! Chama chenu hakina wapiga kura ,ila kina washabiki uchwara tu kama wewe humu! Uchaguzi umeshakwisha na JPM ndie mshindi!.
 
Tunawataka Mawakala wa CHADEMA walioshuhudia watupe hizo Nakala, tuchukue kama sample tuone kama Lissu alishinda mbona tunaandikia mate na wino upo, mfano wa Bwege unaonyesha still JPM aliwin 70/67 .....zingine ni bla bla
Ww hujui chochote na hutakaa ujue chochote, mm nilikuwa msimamizi wa kituo! Najua kilichofanyika!!! Yalikuwa yanatekelezwa maagizo wala sio maamuzi ya wananchi!!,
Kiujumla uchaguzi huu ulikuwa wa hovyo sana
 
Yani kwa Mbowe ilikua lazima wananchi wamtoe ! Hamna chochote alichokifanya HAI !..Yani Chama chenyewe ,Mwenyekiti wao hajaweza kutetea jimbo!,Huo Ushindi wangetolea wap!
 
ACHA HOJA ZA KITOTO NA WEWE!.....WAKALA GANI SASA HIVI ANAWEZA KUFUNGUA MDOMO NA KUELEZA HAYO, KILA MTU ANAYAPENDA MAISHA YAKE NDUGU......HATA WAKALA AKIONGEA HAISAIDII KITU ZAIDI YA KUMUINGIZA MATATIZONI
 
"Nyie watu wa Rufiji mna matatizo badala mchague Mbunge unachagua Bwege ,Bwege atawasaidia nini badala ya kuleta ubwege maana naona hapa hakuna alichofanya hata kujenga choo tu cha stand kwa pesa za jimbo ameshindwa "by JPM
Rufiji iko Lindi? Hebu acha upumbavu jombaa...
 

Hata viongozi waliongia kwa kupindua nchi huwa ni viongozi. Narudia tena, waliopiga kura hawakufika 10m, hilo sikulazimishi uamini, lakini habari ndio hiyo.
 
Katika muktadha huohuo tusione mkimjadili Jpm hapa jukwaani! Maana Kama hakukua na Uchaguzi maana yake hata Rais hamumtambui !

Hili sio jukwaa la ccm, labda huko kwenye majukwaa ya ccm ndio msimjadili. Shetani mwenyewe anahubiriwa huko kwenye nyumba za ibada, kwani ni dalili kuwa anakubalika? Hatuna utaratibu bwa kutambua wezi wa kura tena za umwagaji damu.
 
Hicho unachosema siyo hoja! , kwa sababu zilizoongezwa zimempa Magufuli overall advantage kwenye kura zote za majumuisho nchi nzima.
MAGUFULI KATANGAZWA RAIS KWA KURA ZA KUBUNI ZA MA DSO NA RSO WALIJAZA KURA ZA MAJUMUISHO BILA HATA KUSUBIRI MASANDUKU YAFIKE MAKAO MAKUU YA WILAYA NA MIKOA AMBAKO HUHAKIKIWA NA KUTUMWA TALLYING CENTRE MAKAO MAKUU YA TUME .......NDIO MAANA MAJUMUISHO YA KURA YAMEKAMILIKA JUZI TAREHE 8/11

WEWE ULISIKIA WAPI MAJUMUISHO NA MATOKEO YA URAIS,WABUNGE NA MADIWANI NCHI NZIMA WANAJULIKANA NDANI YA MASAA 36 ....HUO UFANISI HATA UINGEREZA NA JAPAN WANAKOPIGA KURA KIELECTRONIC HAWANA .....SEMBUSE SISI AMBAKO SEHEMU NYINGINE MABOX YA KURA INABIDI YABEBWE NA PUNDA NA MASHUA ??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…