Uchaguzi 2020 Selemani Bungala (Bwege) asema Magufuli hakushinda kihalali. Atolea mfano wa aliyoshuhudia katika vituo viwili jimboni kwake

Kwani takwimu za TUME zinasemaje kuhusu idadi ya raia waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura? je, kati ya hao ni asilimia ngapi walipiga kura, labda tuanzie hapo.

Tume ya ubaguzi ni wapika data kama wapikaji wengine.
 
Sehemu nyingi inchi mzima ikifanyika ivyo ivyo
Kituo nilichopigia mimi huko Nyakato Mwanza, Lissu alipata kura 69 na Magufuli 41. Kuja kwenye majumuisho ya jumla, fomu imeandikwa Lissu 15 Magufuli 95. Jamaa wakaja juu, baada ya muda mfupi wakaja polisi, na kututaka tuondoke hapo. Kama tuna malalamiko, tuufuate utaratibu.
Kwa kweli, hata JPM na wabunge wake wanaotamba kuwa wameshinda kwa kishindo, wanajua fika wamepora demokrasia bila aibu.
 
Na hii TV ya kenya na watangazaji Mabwege kama mteja wao aliwezaje kushuhudia uharamia asilalamike wakati yeye ni mgombea atoe ushahidi mahakamani
 

Acha hizo kama Mungu sio CCM hakika kabla ya hilo genge kumaliza safari yao ya hapa Duniani wataona malipo yake.
Nakuhakikishia ipo siku Udhalimu huu utalipuwa kisasi kikuu.
Waovu wakikaa pamoja wanajisahau sana. Unajua hata historia za dini zinaonyesha kuna wafalme walipata mafanikio makubwa sana lakini walijikweza na kujiona kama miungu na kuwaumiza sana watu .

Ni ukweli ulio wazi Kura ziliongezwa na kupigwa Mara mbili mbili.
Nilikua nafuatilia kwa karibu sana . Niliwauliza baadhi ya watu ni kwani nini walikubali kuruhusu kura kubadilishwa na watu kupiga kura Mara mbili ?
Majibu niliyoambiwa ni ya kusikitisha sana. Nchi hii kama Mungu ndiye aliyeruhusu huu wizi na unyama walioufanya usalama wa Taifa kushirikiana na mawakala feki wa CCM waliokua wanawatisha Walimu waliosimamia kura basi tumwachie Mungu Mwenyewe huenda ameona mambo mazuri yanayokuja kupitia hawa mabapari na mabilionea walioiba kwa miaka mingi ndani ya serikali na sasa wanahofia Mali zao kubainika na kukosa mlinzi .

Lakini kama Uhuni uliofanyika umepangwa kutokana na tamaa ya watawala na vyombo vya dola vilivyokua vinashiriki kwa muda mrefu kutorosha twiga na madawa ya kulevia na kujilimbikizia Mali na sasa wanatumiwa na wanasiasa waliokua wanaliibia taifa kwa miaka mingi basi Mungu ataonyesha njia Miaka hii mitano CCM watavaa nguo nyeusi mana upepo wa kisulisuli utaibadili histori ya nchi kabla ya mwaka 2025 .Hakuna mtu atakayewaambia wananchi andamaneni Bali watajiorganise wenyewe na hapo ndipo mabadiliko yatakapotokea na Mali walizojilimbikizia wezi na madhalimu zitapeperushwa kama upepo wa kisulisuli na kutapanywa kwa wahuni wasio na ajira mitaani.

Tubuni kwa udhalimu huo mlioufanya. Ushindi ungeweza kupatikana kwa halali bila kuwaumiza wengine na kufanya wizi. Eti mashindano ya kumpatia Rais kura nyingi za kutengeneza . Kama watu wanapanga njama kuiba kura watashindwaje kuiba Mali za umma na kupoteza ushahidi huku wakiudanganya umma.

Mitandao ilipozimwa mlitegemwa watu watumeje picha za nakala halisi za matokeo.?
Kuna mambo yanakera sana kwa wanasiasa wanaotumikia Fedha na mali zao?

Hata hivyo tunataka maendeleo nchi nzima mana Yale mambo ya CCM kuchukulia ushindi wa uchaguzi kama ushindi wa mpira wa kuchambana na kushangilia bila kujua kuwa wana wajibu wa kuleta maendeleo nchi nzima kwa usawa na sio kutuonyesha uzinduzi wa ukanda mmoja miaka mitano kisa waliwachagua kwa wingi sasa mmechaguliwa kwa wingi nchi nzima wanataka maendeleo . Vile vihela vichache mlivyokua mnavipeleka kwnye maeneo ya mawaziri tu sasa njiandae kutolewa macho na wabunge wenzenu wa CCM .
Mtakopa China kama Zambia na watachukua mpaka Kanisa la Gwajima mana hamtaweza kulipa madeni yao na hamtaweza kuacha kukopa ili miradi ya maendeleo ifanywe kama mlivyoahidi .

Maendeleo hayana Vyama Vingi.
 
"Nyie watu wa Rufiji mna matatizo badala mchague Mbunge unachagua Bwege ,Bwege atawasaidia nini badala ya kuleta ubwege maana naona hapa hakuna alichofanya hata kujenga choo tu cha stand kwa pesa za jimbo ameshindwa "by JPM
Hujui hata Bwege alikuwa mbunge wa wapi, Rufiji ni watu makini ,tumesimama na CCM, tumesimama na Mohamed Mchengerwa, hayo mambo ya Bwege ya Kilwa huko
 
Vyama vya upinzani mjitafakari upya mienendo yenu iliyopelekea wananchi kuwatupa nje kwa sanduku la kura.Ukweli nikuwa wananchi hawakuwaunga mkono ndo maana hata maandamano mliyoitisha hawakuitikia iwe visiwani au bara.
 
Sasa unapiga kura isiyo ya siri halafu ujidai eti unampa kura wa mlengo mwingine? Labda kama unapakukimbilia!
 
"Nyie watu wa Rufiji mna matatizo badala mchague Mbunge unachagua Bwege ,Bwege atawasaidia nini badala ya kuleta ubwege maana naona hapa hakuna alichofanya hata kujenga choo tu cha stand kwa pesa za jimbo ameshindwa "by JPM
Kukosa akili ndio ugonjwa mbaya kuliko magonjwa yoote! bora ungekaa kimya kuficha upumbavu wako!
 
Vyama vya upinzani mjitafakari upya mienendo yenu iliyopelekea wananchi kuwatupa nje kwa sanduku la kura.Ukweli nikuwa wananchi hawakuwaunga mkono ndo maana hata maandamano mliyoitisha hawakuitikia iwe visiwani au bara
Sidhani kama unajua ulichoandika na ukweli ktk 'box la kura' ulivyokuwa! Ila watu kama nyie mpo wengi wenye akili fupi.
 
"Nyie watu wa Rufiji mna matatizo badala mchague Mbunge unachagua Bwege ,Bwege atawasaidia nini badala ya kuleta ubwege maana naona hapa hakuna alichofanya hata kujenga choo tu cha stand kwa pesa za jimbo ameshindwa "by JPM
Hela za halmashauri zinafanya nn.
 
Kuna msimamizi wa kituo kimoja ashaweka matokeo humu, yapo hivi..

Matokeo halisi:
T. Lissu kura 179
Jpm kura 31

Matokeo feki yaliyotangazwa:
T. Lissu kura 6
Jpm kura 370
 

Mkuu, hilo halibadirishi kitu cha muhimu hapa ni: NEC walikubaliana na Vyama vya upinzani kwamba watafuata utaratibu upi katika kuhesabu na kuhakiki idadi ya kura kika kituo - sasa kama kuna chama au wasimamizi wa vituo walio hamua kuweka mpira kwapani na kukimbia nao kwa kuwatisha au kufukuza mawakala wa vyama vingine ili wasihakiki kura basi hilo linadhilisha kwamba uhesabuji wa kura uligubikwa na mapungufu mengi - wahusika watafute namna ya kufikia maridhiano without offending anyone.
 


Huyo anayetumia lugha ya alama anafanana na Dr. Shika, "I miss him"
 
Hii filamu ya uchaguzi ni kichaa peke yake atakayeishangilia.Ila muda utatupa majibu.Wakati si milele na wakati wa Mungu sio wa mwanadamu.
 
Tunawataka Mawakala wa CHADEMA walioshuhudia watupe hizo Nakala, tuchukue kama sample tuone kama Lissu alishinda mbona tunaandikia mate na wino upo, mfano wa Bwege unaonyesha still JPM aliwin 70/67 .....zingine ni bla bla

Wewe unatoka sayari gani? 90% ya mawakala hawakuruhusiwa kushudia zoezi la kura kupigwa wala kuhesabiwa.Nawalioruhusiwa wengi waliondolewa kabla ya zoezi kwisha lastly hakunamahali waitoa nakala za matokeo zikiwana signature za wasimamizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…