Selfika na JF: Snap it. Show it

Hongera kama ulikuwa na weekend njema.

Kwangu ilikuwa ni kinyume chake, baridi kidogo liniue Kwa upweke Babu yenu 🤗

Nimetafuta nyimbo zetu za Mwaka 47, za kunifariji nimekosa.

Nimeangukia kwenye nyimbo ya Kijana mwenzenu Darassa ft Hamornize inaitwa mazoea.


Nimebaki kuicheza Kwa kuirudia kwenye redio yangu ya Mkulima japo kupunguza mawazo 😜

Hello Tuesday 🥂
 
Ahaha pole next time tena nikija bongo iyo
 
Mi nilikuwa hoi. Niliugua mafua ya ajabu kweli sijawahi ugua mafua ya namna hii. Na homa kali mwili ulikuwa umechemka na kutetemeka.
Pole sana Mkuu, Siku nyingine ukipigwa na mafua, hakikisha unafanya mazoezi ya kukimbia.

Baada ya Siku moja, mafua yote hupona

Ndiyo maana Wazee wanasema mazoezi ni tiba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…