Seran
JF-Expert Member
- Feb 7, 2025
- 36,315
- 104,500
Mwambie haupendi hiyo tabia kwanza ni mbaya! Analiaje jikoni? Kwani mkiweka chakula mezani hali au.. mwambie ukweli anakuona unakaa kimya ndio maana hawazi hata kutenga vipande vyake vitau pembeni!Nimepata dada wa nyumbani, changamoto yake akiwa jikoni muda wote mdomo unatafuna.
Nikawa nampotezea naona anaonja kawaida ila juzi naenda jikoni namkuta kitimoto kaweka kwenye nyanya tayari, ametenga vipande vi3 pembeni vya kutafuna na muda huo mdomo una nyama.
Hapa anakaanga chips, hii awamu ya 3 kila akitoa na yeye anachota anakula
Ukiwa sebleni unaona jikoni ndo maana namuona.
Hii ni kawaida kwa wote au🤔
Mimi mdada wangu hawezi hizo tabia kwanza hana, kwahiyo si kawaida!