Brother Wako
Member
- Mar 18, 2017
- 23
- 22
Miaka yangu miwili kama muumini wa Imani hii, niliamini hakuna mtu anaweza kusikia maagizo ya Mungu kama hajafunguliwa kutoka kwenye nguvu za giza zinazomshikilia katika ulimwengu wa kiroho (wanaita vifungo). Lakini siku chache baada ya kutoka Selivesh, kwa msaada wa Neema ya Mungu, kulitafakari Neno la Mungu, na tafiti kadhaa, niliweza kutambua kwamba mimi mwenyewe nilikuwa kwenye Imani ya watu wanaonyanyaswa kiroho. Mpaka naamua kutoka, nilikuwa ninaamini nimefungwa na nguvu za giza, zinaa na laana za wazazi wangu licha ya kuwa nimeokoka na kuikiri Imani ya Kristo.
Selivesh ni imani inayoongozwa na kiongozi mwenye lengo la kuwanyonya na kuwanyanyasa kiroho, kimwili na kiakili waumini wake. Watu wake wanaelimishwa kutafuta majibu ya mambo yote yanayohusu maisha yao kwa kiongozi huyo. Kiongozi hujivisha vazi la imani ya Kristo kwa kutumia Biblia ili kuteka fahamu za waumini na kuwafanya watumwa wake. Huligeuza Neno la Mungu na kuwatafisria waumini wake ili kujifanya yeye ni nabii wa Mungu. Ili watu wake wafanikiwe, lazima wamuamini yeye nabii (2 Nyakati 20:20) na kuwafundisha kuwa lazima wamshirikishe yeye kila kitu ili wasipate matatizo katika maisha yao. (Wagalatia 6:6)
Watu wa Selivesh sio rahisi kuwagundua. Wao wenyewe hawatambui kuwa wako katika Imani inayolenga kuwanyanyasa na hawajui kuwa ni watumwa wa kiongozi anayewaaminisha wako sehemu sahihi itakayowafanya wafike mbinguni na kuwa wenye maisha ya baraka hapa duniani.
Vifungo vya giza vyote vinafunguliwa na kiongozi huyo. Ni jukumu la watu wachache wa Imani hii waliochaguliwa na kiongozi mkuu kuingia katika ulimwengu wa kiroho na kuona kinachofanyika kuhusu mtu mwingine ambaye inaaminika hawezi kusikia wala kuhisi Mungu akiongea nae kuhusu maisha yake.
Ukiwa mmoja wao, ukiumwa hutakiwi kwenda hospitali mpaka uwasiliane na kiongozi ili akuruhusu kwenda hospitali au upone tu kwa maombi, maana ukienda bila ruhusa yake, inaaminika mabaya yatakupata, hata ukiwa umezidiwa usiku wa manane jitahidi umpate na usipompata ni bora usiende. Utaambiwa hospitali ni mpango wa shetani unaotumika kuwaua watu kirahisi. Kwa mujibu wa mafundisho yao, wanaamini shetani hupandikiza magonjwa au ajali kwa mtu, akienda hospitali afe ili isemekane kuwa shetani alikusudia kumuua kupitia mikono ya madaktari ambao nao wamefungwa na nguvu za giza.
Unapokaribishwa Selivesh, unatabiriwa kuwa mtu mwenye mafanikio makubwa lakini kuna vitu vimekushikilia katika ulimwengu wa kiroho vinavyokuchelewesha kufanikiwa, mara nyingi vitu hivyo vinawahusisha wazazi, marafiki na ndugu. Muumini hupewa mifungo kwa uongozi maalum, mifungo ya kutokula na kunywa maji kuanzia siku moja (masaa 24) hadi siku saba kavu. Maisha ya kufunga hivi yanaendelea kwa miaka kadhaa kwa kuongozwa na kiongozi kwa sababu ya kuamini ni watu wachache wanaweza kukua kiroho na kumuelewa Mungu. Hivyo washirika hubaki chini ya uangalizi maalum wakingoja kukua kiroho ili wamuelewe Mungu.
Ni kawaida kuacha ndoto za maisha yako ziende ili kusubiri ahadi ya Mungu juu ya maisha yako inayopitia kwa kiongozi wako, sio wewe, maana kila kinachokuhusu lazima kipitie kwake kwa kuamini yeye ni mungu.
Anachokifurahia, ndio anaamua kiwe mpango wa Mungu kwenye maisha yako. Nikiwa katika imani hii, nilimshirikisha kiongozi juu ya ndoto yangu akaniambia haikuwa mpango wa Mungu nitulie mpaka nifunguliwe kwanza, na hivyo ndoto yangu ilizimwa palepale, niliamini kupitia yeye, ni sauti ya Mungu imenijibu, hivyo nilitakiwa kutii.
Imani hii ina utaratibu wa kubadilisha watu majina yao, utaambiwa jina ulilopewa na wazazi wako limebeba maana mbaya au limeambatana na vifungo vya kichawi. Kiongozi huwapa watu majina mapya na kuwafanya watu wakatae majina waliyopewa na wazazi wao. Mwanamke aliyejifungua mtoto anatakiwa kuwasiliana na kiongozi kuhusu suala la uchaguzi wa jina la mtoto. Inaaminika jina atakalotoa kiongozi, litamfanya mtoto kuwa mwenye mafanikio. Jambo hili limeleta mafarakano kwa wanandoa ambao wenzao hawaamini Imani hii. Watu wa Imani hii hujiita majina mapya yakifuatiwa na jina la kiongozi huyu, yaani huamua kuondoa majina ya wazazi na koo zao.
Waumini huaminishwa kuwa viongozi ndio wazazi wao, wazazi wa kiroho ni bora kuliko wazazi wa kimwili maana wanakilea kiroho chako (waefeso 6:1). Waumini wengi wamechagua kuwapenda na kuwaheshimu wazazi hao wa kiroho kuliko wazazi wao wa kimwili maana ni sehemu ya malengo ya elimu ya Imani hii.
Vijana wa jinsia tofauti hawaruhusiwi kuwa na urafiki ili kuishinda zinaa. Vijana ambao hawajaoa na kuolewa hufungishwa mifungo ya siku tatu mpaka saba, bila kula wala kunywa wakiikataa roho ya zinaa. Wanaaminishwa hawatakuwa na hamu ya mapenzi kabla ya ndoa, kitu ambacho hakisaidii maana vijana wamendelea kufanya zinaa pasipo kiongozi huyo kujua. Nabii hudanganya watu kuwa yeye anaona kila kitu katika ulimwengu wa kiroho.
Vijana hawawezi kumfuata kiongozi (Nabii) kumwambia kama wanawapenda wenzao wa jinsia tofauti na wangefurahia kuoana nao. Wamekuwa wakiambiwa ni roho ya zinaa inawadanganya. Wengine ambao wamepata wapenzi nje ya Selivesh wanaambiwa hawawezi kuoa au kuolewa nje ya imani hiyo, wanapaswa kuwaacha na kuwasubiri wapenzi ambao ni ahadi ya Mungu inayoonwa na kiongozi au msaidizi wake kwenye ulimwengu wa kiroho.
Uzalilishaji ndani ya imani hiyo ni kawaida, viongozi hutumia udhaifu wa washirika kama sehemu ya mafundisho, mtu husimamishwa mbele ya kusanyiko na kutolewa mifano ya aibu akidanganywa kuwa anapokuwa wazi mbele za watu, Mungu anamsikia na kumsamehe dhambi zake haraka kuliko anavyokiri udhaifu wake kimya kimya.
Waumini hulazimishwa kukiri dhambi zao za zamani kwa kiongozi huyo wakiaminishwa ndio watafunguliwa vifungo vyao, wengine huambiwa hawatapokea kipawa cha Roho Mtakatifu wala kufanikiwa mpaka wakiri dhambi zao, hivyo waumini hulazimika kukiri dhambi hata ambazo hawazikumbuki ili kuwafurahisha viongozi hao wawafungue maisha yao.
Kiongozi wa ngazi ya juu ndiye msemaji wa mwisho, jambo lolote linalohusu maisha ya mtu binafsi, yeye ndiye anafanya maamuzi ya mwisho. Hakuna mwenye uhuru wa kuhoji wala kukosoa chochote kilichosemwa na kiongozi huyo. Tamaa ya kila mwanachama wa Selivesh ni kuwa na mahusiano ya karibu na kiongozi huyo.
Miongoni mwa tabia mbaya zaidi katika imani hii, ni hali ya kujifanya wakamilifu mbele za watu wakati uhalisia sivyo ilivyo. Watu wa imani ya Selivesh wanalazimika kujaribu kufanya kila kilicho chema mbele ya watu wengi (hasa watu wa jamii yao), ili kujionyesha wanatimiza sheria inayopendwa na viongozi.
Ukipenda haki sawa huwezi kushinda. Wanatumia ustawi wako kama sababu ya kukunyanyasa kwa sababu wametumika kuleta mabadiliko kwako.
Ukijitoa Selivesh unaonekana ni muasi, kiongozi hukuombea mabaya na mtu yeyote anayebaki huko haruhusiwi kuwa na mahusiano na wewe tena.

Upvote
2