Sembe kilo imefika 1800 kwa sasa tutashaa

Sembe kilo imefika 1800 kwa sasa tutashaa

Na siku umekosa kabisa hiyo hela ya kununulia unataishije
Ntakua nimeshafariki (duniani)

nikiwa hai hivi haitokaa itokee nikose pesa ya unga nusu

labda unga wa brazil ila sio huu sembe na dona
 
Na huko katavi nimesikia gunia la mahindi ni 80000 kitu ambacho hata wakulima wa huko huko nao wanashangaa..
Narudia kusema tutashaa..
How credible and reliable is your information kaka? La sivyo tukufuate hapo sasa hivi kwa kusababisha taharuki kwa umma!
 
Yaani vitu vingne vinafanywa kwa sifa
Ukisharuhusu soko huria la vyakula hasa Mahindi, Maharange nk basi wa kuumia ni watu wa hali ya chini....sasa hivi watu wanalalia uji na bado kuna uwezekano wa kula pumba. Yaani vyakula vipo ila hela hawana.

watu wa hali ya juu na kati hata hawajui bei ya unga ni nini? kweli duniani hapa jamani hakuna usawa kabisa.
 
Wacha wakulima nao waonje raha ya kazi yao.

Ilikuwa kwao ni kilio mwanzo mwisho. Pembejeo kilio, mbegu kilio, hata soko lilikuwa kilio pia.
Angalao kwa muda mfupi nao watabasamu. Viva wakulima!
 
WAMERUHUSU KUUZA NJE NGOJA WACHUKUE MAHINDI YOTE ILI TUJITAMBUE VIZURI WAKENYA SI WAKUWAZOEA.
 
Wapi huko mzee maana sisi huku kwetu tunaishi nayo kwa buku tu
 
Na huko katavi nimesikia gunia la mahindi ni 80000 kitu ambacho hata wakulima wa huko huko nao wanashangaa..
Narudia kusema tutashaa..
Watanzania huwa hamueleweki hata kidogo, bei ya gunia la mahindi kwa mwaka jana ilikuwa chini mlilalamika sana kuwa mkulima ananyonywa, leo hii bei imepanda bado tena mnalalamika. Ni kipi hasa huwa mnataka!?.
 
Mimi sio mkulima tatizo ni bei elekezi

Back
Top Bottom