tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,040
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Dorothy Semu amesema kuwa chama hicho kikipata ridhaa ya kuongoza nchi kitahakikisha ndani ya siku 100 kinaunda tume ya kijaji ili itoe majibu ya matukio ya nani wanaohusika kupoteza na kuteka watu nchini .
Ametoa kauli hiyo Oktoba 12, 2025 akiwa Kata ya Pasua na Kaloleni Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro wakati akiwanadi wagombea Udiwani wa Kata hizo na Mgombea Ubunge Jimbo la Moshi Mjini Ngassa Stephen ambapo amesema kuwa chama hicho hakija sahau na hawata sahau hali ya usalama wa raia.
Soma pia: Madeleka: IGP asiishie kupunguza matukio ya utekaji, akomeshe kabisa
"Hatutasahahu na hatutasahau hali ya usalama ya raia, tumeona namna watu wanavyotekwa wanasiasa wenye sauti kinzani,wanaharakati wanaosimama na demokrasi wengine wako jela,wengine wamepotezwa,wengine wameuawa tunasema hivi, ndani ya siku mia moja tutahakikisha tumeunda tume ya kijaji kutuambia nani alitepoteza watu hawa, aliye tekeleza amri hii na anaye ongoza upoteaji wa watu na utishiaji wa watu " Semu