Senegal: Rais Faye azindua rasmi chama chake kipya, Wanachama wa Sonko sasa wanakimbilia kwa Faye

Senegal: Rais Faye azindua rasmi chama chake kipya, Wanachama wa Sonko sasa wanakimbilia kwa Faye

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, amezindua rasmi chama chake kipya cha kisiasa kinachoitwa Republican Patriots, hatua inayodhihirisha rasmi kuvunjika kwa uhusiano wake na mshirika wake wa siku nyingi na Waziri Mkuu wa zamani, Ousmane Sonko.

Viongozi hao wawili waliingia madarakani kwa pamoja katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2024, wakati huo Faye akiwa Katibu Mkuu wa chama cha Sonko cha PASTEF. Hata hivyo, uhusiano wao ulizorota vibaya kutokana na tofauti za kimitazamo kuhusu mikakati ya kiuchumi na mamlaka ya utendaji, hali iliyomfanya Faye kumfuta kazi Sonko kama Waziri Mkuu.

Kuanzishwa kwa chama cha Republican Patriots kunafuatia wimbi la wanachama na viongozi maarufu kuhama kutoka PASTEF na kujiunga na kambi ya Rais.

Pamoja na viongozi wa PASTEF kujaribu kupunguza ukubwa wa athari za kuhama kwa wanachama hao, Sonko—ambaye kwa sasa ni Spika wa Bunge—aliunga mkono mabadiliko ya katiba yanayolenga kumzuia Rais aliyeko madarakani kuongoza chama cha kisiasa kwa wakati mmoja.

Ingawa bunge lilipitisha mswada huo, Faye ameamua kuweka maamuzi hayo mikononi mwa wananchi kupitia kura ya maoni. Tarehe ya kura hiyo bado haijatangazwa, huku pande zote mbili sasa zikielekeza nguvu zao kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2027.

Soma pia Senegal: Rais Bassirou Diomaye Faye atangaza kuanzisha chama chake cha kisiasa, akijitenga na Pastef

1785068585841.png

===========

Senegal President Bassirou Diomaye Faye has launched a new political party, the Republican Patriots, formally solidifying his rift with long-time ally and former Prime Minister Ousmane Sonko.

The two leaders rose to power as a unified ticket in the 2024 presidential election, when Faye served as secretary-general of Sonko’s PASTEF party. However, relations deteriorated sharply over economic strategy and executive control, culminating in Faye dismissing Sonko as Prime Minister.

The launch of the Republican Patriots follows a series of high-profile defections from PASTEF to the President’s camp.

While PASTEF leadership has sought to minimise the impact of these departures, Sonko, who now serves as Speaker of the National Assembly, backed constitutional reforms designed to prohibit a sitting President from simultaneously leading a political party.

Although parliament approved the measure, Faye has opted to put the decision to a public referendum. A date for the vote has yet to be announced, with both camps turning their focus toward the upcoming 2027 local elections.

Source: Channel Africa, AP News & Reuters
 
Nchi za wenzetu ziko tofauti sana na hapa kwetu, yaani unampinga Rais comfortably kabisa. Sijui ni katiba au sijui ni wao tu politically wako matured... Hapa kwetu ukipinga tu Samia utakua umeli-miss kaburi.

Tatizo ujue kwanza imekuwaje!!!

Uyo Rais Faye. kama sio uyo Sonko
Faye bado angekuwa jela mpaka sasa!!

Kwamaana kwa msaada wa Sonko Faye katoka jela kaenda kuwa Rais wa nchi kama umeelewa kwa faida yako👈

Sasa sijui kama nisawa kulinganisha na Tanzania✍️
 
mifumo tumeilea sisi wenyew
Uoga mwingi na kutamana kuish kinyonge
Wasenegal hawachelew kukiwasha na washapitia hii hatua tyr
 
Tatizo ujue kwanza imekuwaje!!!

Uyo Rais Faye. kama sio uyo Sonko
Faye bado angekuwa jela mpaka sasa!!

Kwamaana kwa msaada wa Sonko Faye katoka jela kaenda kuwa Rais wa nchi kama umeelewa kwa faida yako👈

Sasa sijui kama nisawa kulinganisha na Tanzania✍️
wew kuna kitu unachanganya , aliyekuwa jela ni huyo wazir mkuu aliyetolewa na yeye Sonko ndo akaamua kumpa kijiti msaidiz wake Faye agombee urais kisha Faye akashinda na aliposhinda wazir mkuu wake akawa Sonko ila baadae wakatofautiana maana Sonko anaamin hiyo nafas ya urais ni yake na Faye aliipata kisa yeye alipitia mikasa kipind cha uchaguz na kumpa kijiti Faye
So kuna namna Sonko alikuwa anajiona mwamba dhidi ya rais Faye ambaye aliwai kuwa msaidiz wake hapo zaman
Hapo Faye na Sonko wote wana makosa
Faye kashindwa kumvumilia jamaa yake na kutafuta namna kumueliminate kisomi kweny siasa
Pia Sonko ameshindwa kuona utofaut wa nyakat maanba Sonko anamtizama Faye kama yule msaidiz wake wa zaman wkt Faye ss hv ni rais , hvyo Sonko alitakiwa kumuheshimu mkuu wake maana tyr yupo juu yake , na kama kuna makosa alipaswa kumfuata personal na kumuelekeza na sio kumkosoa kweny media na wanafanya kweny serikali moja
 
Nyote wawili mnachanganya mambo.

Sonko alikuwa mpinzani mkuu wa Macky Sall. Rais Sall akamfunga Sonko na katiba ya nchi hiyo inamtaka aliyetuhumiwa kwa kesi kama ile asiruhusiwe kugombea Urais.

Wananchi wakaandamana vikali, Macky Sall akamtoa Sonko jela ili wafanye mazungumzo wasogeze uchaguzi mbele ila Sonko akakataa akaona ni janja janja ya kuiba uchaguzi kama kawaida. Sonko akaacha kugombea na kumuunga mkono Faye (ambaye alimchukulia kama dogo).

Wakapanga akipata Urais anamteua Sonko awe Waziri Mkuu. Sasa Faye ni Rais, ana mamlaka kikatiba ila Sonko bado anamchukulia dogo.
Kwa kuwa Sonko ndio mkubwa kwenye chama, ndio ana-dictate chama kifanye nini. Basi Faye hana kauli kwenye chama, na bado Sonko anataka awe na kauli serikalini msimamo anaochukua yeye ndio uwe wa serikali.

Mwishowe Faye akamtoa serikalini, Sonko kwa kuwa anakubalika kwenye chama akamwambia Spika ajitoe. Akagombea uspika sababu chama chao kina viti vingi akashinda. Faye akaona ni move ya kufanya impeachment au kumnyima kugombea muhula wa pili. Akamuachia chama chake na kuunda hiki.

Kwa hiyo hivi sasa Senegal itakuwa na vyama vikuu vitatu. Cha Sonko, hiki cha Faye na kile cha Macky Sall ambacho bado kinaungwa mkono maana wapinzani walipoingia madarakani wanabishana tu hamna kitu wanafanya. By the way Faye atataguta coalition ya vyama uchwara kina CHAUMA na ACT Wazalendo za kule.
 
Tatizo ujue kwanza imekuwaje!!!

Uyo Rais Faye. kama sio uyo Sonko
Faye bado angekuwa jela mpaka sasa!!

Kwamaana kwa msaada wa Sonko Faye katoka jela kaenda kuwa Rais wa nchi kama umeelewa kwa faida yako👈

Sasa sijui kama nisawa kulinganisha na Tanzania✍️
Mkuu Samahani, umechanganya majina kidogo. Faye ndiye aliyemtoa Sonko gerezani na sio Sonko kuwa ndiye aliyemtoa gerezani Faye...

Iko hivi ni kwamba Sonko ndiye alikua anaenda kugombea urais na alikua ni mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa na alikua na uwezekano wa kwenda kushinda urais. Chama tawala wakamweka ndani kama ilivyo Tundu Lissu Tanzania. So Sonko akam-propose Faye agombee urais kwa kuwa yeye alikua hawezi kugombea kwa kuwa yuko jela... Faye akagombea urais na akashinda, ndipo akaenda kumtoa Sonko gerezani na akamteua kuwa waziri mkuu... Point yangu iko hapa kwamba Faye ndiye aliyemtoa Sonko gerezani... Ila Point ya Sonko kumsaidia Faye kupata urais hapo uko sawa..
 
wew kuna kitu unachanganya , aliyekuwa jela ni huyo wazir mkuu aliyetolewa na yeye Sonko ndo akaamua kumpa kijiti msaidiz wake Faye agombee urais kisha Faye akashinda na aliposhinda wazir mkuu wake akawa Sonko ila baadae wakatofautiana maana Sonko anaamin hiyo nafas ya urais ni yake na Faye aliipata kisa yeye alipitia mikasa kipind cha uchaguz na kumpa kijiti Faye
So kuna namna Sonko alikuwa anajiona mwamba dhidi ya rais Faye ambaye aliwai kuwa msaidiz wake hapo zaman
Hapo Faye na Sonko wote wana makosa
Faye kashindwa kumvumilia jamaa yake na kutafuta namna kumueliminate kisomi kweny siasa
Pia Sonko ameshindwa kuona utofaut wa nyakat maanba Sonko anamtizama Faye kama yule msaidiz wake wa zaman wkt Faye ss hv ni rais , hvyo Sonko alitakiwa kumuheshimu mkuu wake maana tyr yupo juu yake , na kama kuna makosa alipaswa kumfuata personal na kumuelekeza na sio kumkosoa kweny media na wanafanya kweny serikali moja

Lkn unajua Faye alifungwa kwa miez 11 kaachiwa week moja kabla ya Uchaguzi??

Unajua kwann kaachiwa??
 
Mkuu Samahani, umechanganya majina kidogo. Faye ndiye aliyemtoa Sonko gerezani na sio Sonko kuwa ndiye aliyemtoa gerezani Faye...

Iko hivi ni kwamba Sonko ndiye alikua anaenda kugombea urais na alikua ni mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa na alikua na uwezekano wa kwenda kushinda urais. Chama tawala wakamweka ndani kama ilivyo Tundu Lissu Tanzania. So Sonko akam-propose Faye agombee urais kwa kuwa yeye alikua hawezi kugombea kwa kuwa yuko jela... Faye akagombea urais na akashinda, ndipo akaenda kumtoa Sonko gerezani na akamteua kuwa waziri mkuu... Point yangu iko hapa kwamba Faye ndiye aliyemtoa Sonko gerezani... Ila Point ya Sonko kumsaidia Faye kupata urais hapo uko sawa..

Sijachanganya mkuu! 👈

Faye alikuwa ndani kwa miezi 9 au 11 aliachiwa week1 kabla ya
Uchaguzi So kafanya kampeni kwa iyo wiki moja✍️
 
Unachanganya majina, aliyefungwa ni Sonko sio

Fatilia upya mkuu utagundua Faye na Sonko wate walikuwa jela na walitoka wote iyo wiki 1 tu kabla ya Uchaguzi 👈

kwamaana Faye kafanya kampeni kwa iyo Wiki 1 tu

Faye alikuwa jela kwa miez 11 👈

kaachiwa wiki moja tu kabla ya Uchaguzi 👈

Katumia iyo iyo wiki moja kufanya kampeni 👈

lkn akashinda kwa msaada mkubwa wa Sonko 👈

pamoja na Rais wa zamani wa Senegal Abdoulaye Wade👈
 
Wametoka iyo wiki moja tu kabla ya Uchaguzi mkuu wa Senegal ✍️
 
Katufuteni tena iyo historia yake Faye kisha mje mnipinge✍️
 
Back
Top Bottom