Seneta John Methu Aitaka Serikali Ya Rais Ruto Kuweka Wazi “Scorecard” Ya Miaka Minne

Seneta John Methu Aitaka Serikali Ya Rais Ruto Kuweka Wazi “Scorecard” Ya Miaka Minne

Omu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
469
Reaction score
95
Seneta wa Nyandarua John Methu ameisukuma serikali ya Rais William Ruto kutoa hesabu kamili ya utendaji wake tangu ilipoingia madarakani mwaka 2022.

Methu amesema serikali haipaswi kupuuza ukosoaji kutoka kwa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kwa kumkumbusha tu kuwa aliwahi kuwa sehemu ya serikali. Badala yake, amesema serikali inapaswa kujibu ukosoaji huo kwa takwimu na ushahidi wa kile ambacho imefanikisha katika kipindi cha miaka minne.

Seneta huyo amehoji iwapo Wakenya wako katika hali bora zaidi leo ikilinganishwa na mwaka 2022, akitaja masuala kama gharama ya maisha, kodi, deni la taifa, afya, elimu na usalama kama maeneo yanayohitaji majibu kutoka kwa serikali.

Methu pia amehoji iwapo ukuaji wa uchumi unaotajwa na serikali unaonekana katika maisha ya Mkenya wa kawaida.

Kauli yake inakuja wakati serikali ikikaribia kutimiza miaka minne madarakani, huku siasa za 2027 zikianza kushika kasi.

Serikali ya Ruto ikitoa scorecard leo, Kwa maoni yako, Kenya iko katika hali bora kuliko ilivyokuwa 2022?
 

Attachments

  • images (17).jpg
    images (17).jpg
    28.4 KB · Views: 35
Back
Top Bottom