Tetesi: Seneti ya Marekani itajadili hali ya Kisiasa Tanzania wakati wowote mwezi huu, hapa CCM lazima wapoteane

Wao wakina nana watuingilie mambo yetu☹️☹️
 
Kama usemacho ni sahihi na kwamba wataalamu wa masuala mbalimbali ya kimataifa kama vile uchumi na kidiplomasia n. k wanathibitisha hilo basi tulianzishe mkuu.
Traore keshalianzisha, nchi zetu ni tajiri sana ila tumeuziwa woga na wazungu na vibaraka wao waliopo madarakani.
 
Sio kashauriwa vibaya...uwezo binafsi .... common sense ni kipengele tajiri.... anabaki kuunda vikosi vya mauwaji na kutesa watu wa Tanzania bara
 
Katika nchi kama Tanzania ambapo rais ni mungu mtu ni uongo kusema rais anashauriwa vibaya kwa sababu yeye anaweza akafanya chochote akipendacho na asifanywe chochote.

Hivyo haya maovu yanayofanyika sasa hivi dhidi ya wapinzani ni rais ndiye wa kulaumiwa kwa asilimia mia kwani yanafanyika kwa ridhaa yake mwenyewe kwani anaona ndio njia ya kumfanya aendelee kutawala.
 
shida inakuja pale kitima ameumizwa, maaskofu wote wamelalamika, watu wanatekwa na kesi ya Lisu, afu mkuu wa nchi anampongeza papa Leo kwa kuteuliwa. hivi unafikiri papa atamsikiliza nani kati yako na hao maaskofu?
Kumpongeza papa, huku wasaidizi wake unataka kuwaua, ni unafiki. Pongezi zake zinavuna laana badala ya neema.
 
Za ndaaaaaaani kabisa... Vipi huyo mpenyezaji wako naye ni mjumbe wa sennet au yuko mbagala?
HILO NDO SWALI LILIKUWA LINANISUMBULIA KICHWA, KWAMBA LEO HII MTU YUPO ANAPIGA DEBE STEND YA MAGUFULI HALAFU ANAPATA ZA NDAANI ZA MAREKANI (HV WANADHANI SENET YA MAREKAN NI KAMATI KUU YA CDM?)
 
Ukiwa na familia ukaanza kunyanyasa au ukaua mwanafamilia serikali itaiingilia Kati kuwa umefanya kinyume na haki za binadamu



Kwa Sasa tangu 2019,2020,2024 wananchi tumeteswa kwenye chaguzi zetu, Sasa Kama ambavyo serikali inaweza kumfurusha mwanafamilia mkatili, je bunge la Ulaya kosa lake lipo wapi wakisema wanayotendewa wananchi,hivi kupoteza au kuumizwa watu ni mambo mazuri?
 
Nkweli kabsaa mkuu, lakin shida inakuja kwamba tumejiandaa kwa hilo? Au ndo tumeshtukizwa?.
Hakunaga muda sahihi wa kujiandaa kwasababu maisha hayasimami, yanaendelea na mabeberu kila kukicha yana njia mpya ya kutubana, siku tukimpata wa kutuondoa ndo hapo hapo mambo yataanza..
Mwamba alishaonyesha njia ila hakukaza...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…