Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Watu wawili wamejeruhiwa na fisi sehemu mbalimbali za miili yao katika Kijiji cha Nyamabano, Halmashauri ya Buchosa Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza wakati wakiteka maji kwenye lambo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi leo Oktoba 4, Ofisa Mtendaji kijiji hicho, Mathias Njoluli amesema tukio hilo liketokea Jumamosi Oktoba 2, saa 12 jioni.
Amewataka waliojeruhiwa kuwa pamoja na Samson Mkumbo (70) na Jonas Onesmo (15) wote wakazi wa Kijiji hicho na wamelazwa hospitari teule ya Walaya ya Sengerema kwa Matibabu zaidi.
Njolilu amesema fisi huyo hadi sasa hajulikani ametolea wapi na kwamba wananchi wanaendelea na msako wa kumsaka fisi huyo waweze kumwangamiza.