Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu amewasimamisha kazi Mtendaji wa kijiji cha Nyamililo Wilayani Sengerema Mariamu Mgunda, pamoja na mwenyekiti wa Kijiji hicho Mateso Shibayi na kuwaweka ndani kwa kosa la kuchangisha kwa nguvu fedha za ujenzi wa jengo la Zahanati.
Mariamu Mgunda ambaye ni mtendaji wa kijiji cha Nyamlilio wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza pamoja na mwenyekiti Mateso Shibayi.
Agizo hilo amelitoa akiwa ziarani mkoani humo, baada ya wananchi kulalamikia mambo wanayofanyiwa na viongozi hao ikiwamo kukamata mifugo kwa kushindwa kutoa mchango.
Baada ya malalamiko hayo, Ummy ameagiza watendaji wote wa vijiji na kata nchi nzima wasichangishe fedha kwa wananchi bila kibali kutoka kwa mkuu wa wilaya husikia.
Akijibu malalamiko hayo, mtendaji Mariamu Mugunda amesema michango hiyo walikubalina na wananchi kupitia vikao vyote vya kijiji hicho na hajaenda kinyume na utaratibu.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Robert Gabriey amesema atafanya uchunguzi juu ya tuhuma hizo na atakayebainika atafikishwa Mahakamani