Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Tarehe 23 Agosti ni siku rasmi ya kuanza zoezi la kuhesabu idadi ya Watu waliopo ndani ya mipaka ya nchi yetu. Zoezi hili limeandaliwa kwa umakini mkubwa tena kwa muda mrefu hivyo kutoa nafasi ya kufanya majaribio mbalimbali na kutatua changamoto na hata kuweka utaratibu mzuri wa kuliendesha zoezi hili la Sensa ya watu na makazi kisasa zaidi.
Serikali imewekeza bajeti kubwa kwenye eneo hili na kizuri zaidi ni kutoa nafasi ya ajira za muda kwenye zoezi hili ambapo makarani walipata mafunzo muhimu ili kufanikisha zoezi hili.
Zoezi limeanza na tumeambiwa na waandaaji kwamba litachukua siku saba mfululizo tangu kuanza kwake. Hivyo kinachoendelea mtaani sasa ni ukusanyaji wa taarifa za watu na makazi kwenye maeneo mbalimbali. Lakini kama tufahamuvyo, kila jambo linalopangwa na wanadamu lina pande mbili yaani mafanikio na changamoto.
lengo la uzi huu ni kuisaidia Serikali kusikia kutoka kwa wananchi endapo kuna changamoto zozote wanazokumbana nazo kwenye hili zoezi. Ninaamini kwamba watendaji mbalimbali wanapitia humu na inawezekana kupitia thread hii wakapata kufahamu nini kinajiri na hatua za haraka kurekebisha kasoro hizo zikachukuliwa.
Ninawasilisha changamoto moja kutoka Kata ya Toangoma wilaya ya Temeke niliyoipata usiku huu kupitia kwa rafiki aliyepo eneo hilo.

- Wakazi wa eneo la NSSF Estate wanalalamikia kwamba karani wa zoezi hilo ambaye ni mkazi mwenzao amewakabidhi vijana wa mtaani wasio na mafunzo wala vitambulisho kusambaza karatasi za kukusanya dodoso la wakazi kila nyumba ya eneo hilo
- Karani huyo hajatoa maelekezo namna ya ujazaji wa form hizo za kukusanya taarifa binafsi za mkazi
- Kuna uwezekano taarifa zitakazotoka eneo hilo zisiwe sahihi kama serikali inavyotarajia