Sensa kufanyika bila watu kuwepo nyumbani haitaathiri zoezi?

Sensa kufanyika bila watu kuwepo nyumbani haitaathiri zoezi?

bulabo

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2015
Posts
628
Reaction score
780
Nawaza kama siku ya sensa haitakuwa siku ya mapumziko, Je zoezi la sensa litaenda vizuri kweli? Nawaza kitofauti kwamba endapo watu hawatabaki nyumbani hasa hasa watumishi ambao baadhi ya familia hawana mtu anayebaki nyumbani hii imekaaje kupata taarifa za familia husika.

Hii siku waifanye iwe siku ya mapumziko ili serikali ifanikishe zoezi hili. Siku moja kubaki nyumbani sio kitu kibaya kwa sababu kama tunabaki nane nane ambazo hazina hata impact kubwa why not SENSA ambayo itatupa data za kufanya tathimini kama taifa.

Me nashauri siku hiyo watu wawepo nyumbani maana kumuacha msichana wa kazi au mtoto itakuwa issue kupata data za mhm kama elimu n.k
 
Kama tarehe 23 August ni siku ya kazi basi hii serikali ni kichaa. House girl ambaye umemleta juzi kutoka Iringa ndiye ajibu maswali zaidi ya 50 likiwemo hali ya uzazi na matatizo ya afya ya kifamilia.
 
Back
Top Bottom