Sensa swali hili ni muhimu sana kuliko swali la kufa, lakini mmelikwepa

Sensa swali hili ni muhimu sana kuliko swali la kufa, lakini mmelikwepa

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
21,741
Reaction score
26,735
Moja ya mambo muhimu sana kwenye nchi wakati wa sensa ni serikali kujua wananchi wake wanakula milo mingapi kwa siku, nilitumai nitaulizwa lakini nikaulizwa kama nina tatizo la kiafya!

Ni vipi unamuuliza hali ya afya yake mtu ambaye hata kupata mlo mmoja kwa siku hana uhakika!

Bahati mbaya waliotunga maswali wao hupata milo minne kila siku, hivyo hawajui kitu kinachoitwa njaa.
 
Ukichunguza kwa makini haya maswali ya sensa yamelenga kitu tofauti kabisa ila yamepewa jina la sensa tu.
Maswali yameegemea kwenye kutafuta vyanzo vipya vya mapato! Muda si mrefu majibu yatapatikana tu.

Unamiliki pasi ya mkaa, unamiliki redio, unamiliki kuku, unamiliki jembe trekta, unamiliki.

Ila na 2025, tutaelewana tu.
 
Fisiemu na walamba asali hawana muda na mambo kama hayo. Hii nchi inaharibiwa na wajinga wachache tu.

Hilo swali ni muhimu sana kwa nchi yenye kujali watu wake na ambayo asilimia kubwa ya watu wake ni masikini kama hii
 
Hoja yangu imeanzia pale nilipoulizwa aina ya CHOO ninachotumia, nilijiuliza kwanini wanataka kujua ninachotoa tumboni lakini hawataki kujua niingizacho tumboni!
Kwa wasiojua, ni kwamba matumizi ya choo ni kwa ajili ya kukificha kitokacho tumboni na si vinginevyo, sasa ndani ya mlo mmoja(kama utapatikana) kwa siku nitatoa nini?
 
Fisiemu na walamba asali hawana muda na mambo kama hayo. Hii nchi inaharibiwa na wajinga wachache tu.

Hilo swali ni muhimu sana kwa nchi yenye kujali watu wake na ambayo asilimia kubwa ya watu wake ni masikini kama hii
Serikali inaona aibu kutokana na wananchi wengi siku hizi wanakula mlo mmoja kwa siku kama utapatikana, hii inamaana wananchi wengi hawana uhakika wa mlo ila wanaendelea kukamuliwa tozo.
 
Serikali inaona aibu kutokana na wananchi wengi siku hizi wanakula mlo mmoja kwa siku kama utapatikana, hii inamaana wananchi wengi hawana uhakika wa mlo ila wanaendelea kukamuliwa tozo.
Ni kweli kabisa wananchi tunakamuliwa sana hadi kupata chakula imekuwa shida. Ukiomba hela sh. 20,000 ndugu akutumie kwa mfano, kuja kukufukia mkononi unakuta sh. 10,000 serikali ya awamu ya sita na kampuni la simu wameshaigawana na kufanya sh. 30,000 imtoke mtoa msaada.
 
Moja ya mambo muhimu sana kwenye nchi wakati wa sensa ni serikali kujua wananchi wake wanakula milo mingapi kwa siku, nilitumai nitaulizwa lakini nikaulizwa kama nina tatizo la kiafya!

Ni vipi unamuuliza hali ya afya yake mtu ambaye hata kupata mlo mmoja kwa siku hana uhakika!

Bahati mbaya waliotunga maswali wao hupata milo minne kila siku, hivyo hawajui kitu kinachoitwa njaa.
Swali hili lipo HBS na DHS kwa sensa haiwezekani
 
Ukichunguza kwa makini haya maswali ya sensa yamelenga kitu tofauti kabisa ila yamepewa jina la sensa tu.
Kwanza sensa yenyewe imevurugwa.mpaka leo hii watu kibao hawajahesabiwa na tatizo ni maccm hayataki kushauriwa.zoezi hili lilitakiwa kufanya watendaji wa mitaa na vitongoji ambao ndo haswa wanawajua watu wao.sensa hii ni ya hovyo kuliko sensa zote zilizowahi kutokea.ccm inatakiwa kuondolewa madarakani haraka sana.wabunge wa ccm hawatusaidii.Tuanze upya kwa kuwafuta wabunge wote wa CCM twende na upinzani.
 
Kwa sababu zipi za msingi haliwezekani, kama haliwezekani kwanini wameweka swali linalohusu CHOO wakati choo kinahusiana na kitokacho tumboni! Bila kula choo hakina matumizi.
angalia maswali ya sensa hata za kabla ya uhuru hili swali huwa linaulizwa. tunayaita traditional census questions. kila nchi hapa Africa swali hili huulizwa. Lina maana nyingi sana kiafya
 
angalia maswali ya sensa hata za kabla ya uhuru hili swali huwa linaulizwa. tunayaita traditional census questions. kila nchi hapa Africa swali hili huulizwa. Lina maana nyingi sana kiafya
Sasa kwanini serikali imelikwepa wakati swali hili huonesha hali halisi ya uchumi wa nchi kuliko maswali yote mengine!
 
Back
Top Bottom