Sensa swali hili ni muhimu sana kuliko swali la kufa, lakini mmelikwepa

Nimeulizwa unafuga Mbuzi,Ng'ombe hapana nikawajibu nafuga Nguruwe,Nyuki,Bata na Kambare wakabaki wanashangaa.

Hawa watu wa Sensa wamekariri wanafikiri kufuga lazima tufuge Mbuzi tena nikawaambia nafuga pia Mbwa kwaajili ya ulinzi na kitoweo.
 
Maswali hawayatungi hao waulizaji, wamepewa na mamlaka husika.
 
Moja ya mambo muhimu sana kwenye nchi wakati wa sensa ni serikali kujua wananchi wake wanakula milo mingapi kwa siku, nilitumai nitaulizwa lakini nikaulizwa kama nina tatizo la kiafya!

Ni vipi unamuuliza hali ya afya yake mtu ambaye hata kupata mlo mmoja kwa siku hana uhakika!

Bahati mbaya waliotunga maswali wao hupata milo minne kila siku, hivyo hawajui kitu kinachoitwa njaa.
Ndugu muwasilishaji.

Naomba nitofautiane na wewe kidogo, lakini pia nitoe elimu kidogo.

Sensa, sio utafiti unaoweza kutoa taharifa zote za kiuchumi na kijamii. Na kutokana na muda unaofanyika ni vigumu sana kutoa akisi ya maisha halisi ya mtanzania kwa kila nyanja.

Zipo tafiti nyingi zinazofanyika na zinazoakisi hali mbalimbali za kiuchumi na kijamii. Mojawapo ya tafiti inayotoa hali ya pato, gharama za maisha na Milo hufanyika kupitia utafiiti wa mapato na matumizi ya kaya (Households Budget Survey), utafiti huu hufanyika kila baada ya miaka minne na huhoji kaya kuhusu matumizi yake yote kwa siku na zoezi hili huchukua takribani siku 14.

Utafiiti wa mapato na matumizi ya kaya (Households Budget Survey) mara ya mwisho umefanyika mwaka 2017/2018 na ni utafiti ambao huwa unafanyika kwa muda wa mwaka mzima (Miezi 12), hivyo kuweza kupata takwimu sahihi na taharifa sahihi kuhusu kipato Cha mtu mmoja mmoja, Milo, pato la mtu mmoja mmoja na familia kwa ujumla.

Naimani nimejitahidi kutoa elimu kidogo

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Taharifa[emoji107]

Taarifa[emoji106]
 
Back
Top Bottom