Senzo kuhamia Yanga ni hatari kuliko Morrison kuhamia Simba

Senzo kuhamia Yanga ni hatari kuliko Morrison kuhamia Simba

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kwa vyovyote vile Morrison ni mchezaji tu wa timu asiye na nidhamu na kazi yake, lakini Senzo ni taasisi.

Senzo ana Mambo yote ya club ya Simba mabaya na mazuri kifuani mwake, ambayo sasa ni rasmi yanaweza kufika mikoni mwa mwajiri wake mpya.

Wasiwasi yangu ni Yale mabaya (Kama yapo) yaliyofanya thimba ibebe vikombe vyote
 
Kama kweli yuko professional kama tunavyoambiwa hakuna wasiwasi.

Ila kama ameshindwa kufanya kazi na Simba, Yanga nao hatawezana nao.

Hizi timu ni dugu moja, swahili sana.
Mara nyingi mke ulivyompata ndivyo atakavyoondoka kwako pia. Kama ulimpatia baa ataondokea baa pia, Kama ulimpatia kwenye kwaya ataondokea kwenye kwaya pia kama ataendelea na kwaya.

Yanga isikenue sanaaa, kama vile Simba wasivyotakiwa kukenua kwa Morrison pia, bundi ni bundi tu rangi sio hoja.
 
Mara nyingi mke ulivyompata ndivyo atakavyoondoka kwako pia. Kama ulimpatia baa ataondokea baa pia, Kama ulimpatia kwenye kwaya ataondokea kwenye kwaya pia Kama ataendelea na kwaya...

Soka la Tanzania ni la kijinga sana, CEO anakuwaje hana clause kwenye contract inayomzuia kujoin competitor!

And then, inaonekana jamaa mkataba ulikuwa umeisha na Simba ni kama walikuwa wanasuasua kumpa mkataba mpya
 
Senzo kama Senzo hana uwezo wa kuizuia Simba bali anaweza kuiendeleza Yanga.

Senzo siyo solution ya Yanga kufika ilipo Simba msimu huu. It's a process. Kumbuka Simba ilishaanza kufanikiwa before Zenzo.

Anyways mchawi mkubwa kwenye soka ni pesa tu hususan bongo.
 
Hizi mambo za bongo nitaanza kufuatilia tukianza kutoboa kimataifa constantly.

Yaani angalau hata vilabu viwili viwepo kwenye game za FIFA au PES la sivyo nitakua nasoma vioja vyao kama hivi kisha napita.
 
Senzo ana Mambo yote ya club ya Simba mabaya na mazuri kifuani mwake, ambayo Sasa Ni rasmi yanaweza kufika mikoni mwa mwajiri wake mpya. Wasiwasi yangu Ni Yale mabaya (Kama yapo) yaliyofanya thimba ibebe
Na mimi naomba niulize. Je, Senzo kama angeamua kutoa siri za Simba akiwa huko huko Simba kama CEO, nini kingemzuia? Kwa lugha nyepesi, je, ili Senzo atoe siri za Simba, ni lazima ahame? Kwa hiyo mimi sioni tofauti ya hatari iwapo Senzo awepo au alazimike kwanza kuhama Simba, ni uamuzi wake tu atoe au asitoe siri
 
Senzo kama Senzo hana uwezo wa kuizuia Simba bali anaweza kuiendeleza Yanga.

Senzo siyo solution ya Yanga kufika ilipo Simba msimu huu. It's a process. Kumbuka Simba ilishaanza kufanikiwa before Zenzo.

Anyways mchawi mkubwa kwenye soka ni pesa tu hususan bongo.
Duniani kote
 
Senzo hana ubavu wa kuitingisha simba kwa sasa anapokwenda anahitaji muda na pesa kuifanya yanga kuwa nzuri ndani na nje ya uwanja
 
Kwani kuendesha club proffesinal Kuna Siri yoyote? Kikubwa NI pesa ya kutekeleza mpango kazi wa timu. Uendeshaji wa club proffesinal kila kitu kunakuwa wazi kuanzia mipango ya usahiri, mishahara na hata malengo ya msimu wa timu. Hawa watendaji Kama senzo ni wasimamizi na washauri tu wa mipango ya club.

Hakuna Siri zozote ambazo unaweza sema Arsenal wakizijua Basi wataihujumu Man utd. Labda huko kwa yanga ambako bado wanaendekeza ushirikina ndio wanafikiri kuendesha timu kwa usiri.

Kama yanga hawana mpango makakti mzuri na fedha za kuwekeza ili kuutekeleza mpango mkakati wao, wasifikiri senzo atawasaidia kuwa moja ya timu Bora afrika. Walichokishindwa kwa sevilla hawatakipata kwa senzo.
 
Na mimi naomba niulize. Je, Senzo kama angeamua kutoa siri za Simba akiwa huko huko Simba kama CEO, nini kingemzuia? Kwa lugha nyepesi, je, ili Senzo atoe siri za Simba, ni lazima ahame? Kwa hiyo mimi sioni tofauti ya hatari iwapo Senzo awepo au alazimike kwanza kuhama Simba, ni uamuzi wake tu atoe au asitoe siri
Watakujibu, lakini wanaume vibamia Siri zao zinatoka baada ya taraka kutoka
 
Kwani kuendesha club proffesinal Kuna Siri yoyote? Kikubwa NI pesa ya kutekeleza mpango kazi wa timu. Uendeshaji wa club proffesinal kila kitu kunakuwa wazi kuanzia mipango ya usahiri, mishahara na hata malengo ya msimu wa timu. Hawa watendaji Kama senzo ni wasimamizi na washauri tu wa mipango ya club...
Kulikuwa na wimbi la timu kususia kuingia vyumba vya kubadilishia nguo, unalifahamu hili?
 
Yule Amekuja Kufanya Kazi
Kinachotafutwa Ni Pesa Tu, Hata Thobias Kifaru Wa Mtibwa Akipanda Dau Anakwenda
Kinachoiuma thimba sio kingine Ila kwenda Yanga. Hii Ni sawa na timu kudhaminiwa na Tigo kwenye ligi inayodhaminiwa na Vodacom. Hata kinachoiuma Yanga Ni Morrison kwenda Simba, angeenda Mtibwa isingekuwa issue kubwa
 
Hakuna hatari yoyote hapo! Kaamua tu mwenyewe kuchagua upande wa Yanga basi wacha aende. But awe makini tu katika kuchagua nani wa kumsikiliza kati ya GSM na Yanga Taasisi.
 
Back
Top Bottom