Senzo: Soka la Tanzania nimejifunza kufanya kazi mazingira hayakuruhusu kuwa huru 100%

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Akizungumza Jana kwenye mkutano wa CAF Jijini Arusha, aliyekuwa CEO wa Klabu ya Yanga African Senzo Mbatha, amesema kuwa katika maisha yake ya soka nchini Tanzania, amejifunza kufanya kazi katika mazingira ambayo hayana uhuru kwa asilimia kubwa.

"Kwa soka la Tanzania nimejifunza kufanya kazi kwenye mazingira ambayo hayakuruhusu kuwa huru kwa asilimia 100%".

"Lakini siyo kwa njia mbaya kwasababu vitu vinafanyika kwa namna fulani, kwahivyo unapaswa kujifunza hayo mazingira, ukitaka kuleta kitu ni lazima ujifunze namna ya kufanya hivyo".

"Siku ambayo Tanzania inatenganisha siasa na weledi wa uendeshaji, soka litanyanyuka mara mbili ya hivi sasa". Senzo Mbatha

Screenshot_20220811-135103~2.jpg
 
Baada ya Wallace Karia, Kibuyu Kingine Kimelia Kwenye Mkutano Wa CAF.

Kwahivyo hapa anatanabaisha kuwa siasa ndo zimemuweka kando, na si zile bhah bhah za matatizo ya kifamilia Afrika Kusini.
Mimi huwa nabaki nawashangaa watu ninaowaheshimu wanaposhindwa kuelewa vitu vidogo vidogo na kuleta ushabiki wa kitoto. Hapo Senzo amefumba nini hadi ujifanye mweupe kiasi hicho?
"Siku nchi ikitenganisha siasa na michezo, mpira utakwenda mbali sana". Hili ni geni halionekani kwenye soka la nchi hii jinsi wanasiasa wanavyojaribu kuteka soka kwa manufaa yao ya kisiasa? Ni nchi gani uliwahi kusikia kiongozi wa soka wakati wa uchaguzi mkuu wa kisiasa anasimama na kumponda mmoja wa Wagombea kama alivyofanya Karia kwa Tundu Lissu mwaka 2020?
Siku ya Yanga day mgeni rasmi makamu mwenyekiti wa Chama tawala, siku ya Simba day mgeni mashuhuri katibu wa itikadi na uenezi wa Chama tawala na vikorombwezo kibao vya kichama. Badala ya kiendeleza soka viongozi wa soka wanaendeleza itikadi za vyama vya siasa!
 
Mbona Mwerevu anajua comment ipo wazi..!

Hapo tumewawekea bayana kuwa amejitenga na siasa, wale walioshindwa kung'amua mambo haya, wengine tushajua kitambo.

Unazungumza vitu ambavyo kila kukicha tunakemea, kuwa hata haya mambo ya Wazee wa Yanga kutaka kumuona Rais Samia, hayana afya kwenye medani ya soka

Juzi tu, nimeandika Uzi kuhusu Kinana kuwa mgeni rasmi, baadhi ya Yanga walipingana na hoja yangu kuwa hayaepukiki haya eti vilabu hivi ni vya Serikali.

Umeongea kitu ambacho tunakifanya
 
Kumbe Senzo kashiriki kwenye mkutano mbona hawa vibaka wake wanalalama kuwa hawajaalikwa? Senzo wakati anaondoka alisema yeye atabaki kuwa mwananchi daima, hivyo madai ya viongozi vilaza wa Yanga kuwa hawajaalikwa hayana msingi,ni upuuzi mtupu.
 
Makolo yalivyo hayana akili yanatafsiri maneno ya senzo kuwa ni kijembe kwa yanga. Yamesahau kuwa senzo kawahi kuwakimbia na wao 😂😂😂
 
Mbona Mwerevu anajua comment ipo wazi..!

Hapo tumewawekea bayana kuwa amejitenga na siasa, wale walioshindwa kung'amua mambo haya, wengine tushajua kitambo.

Unazungumza vitu ambavyo kila kukicha tunakemea, kuwa hata haya mambo ya Wazee wa Yanga kutaka kumuona Rais Samia, hayana afya kwenye medani ya soka

Juzi tu, nimeandika Uzi kuhusu Kinana kuwa mgeni rasmi, baadhi ya Yanga walipingana na hoja yangu kuwa hayaepukiki haya eti vilabu hivi ni vya Serikali.

Umeongea kitu ambacho tunakifanya
Ni kweli huwa unakifanya ndo maana najiuliza Leo kimekupata nini. Kitendo cha kuwasogeza wanasiasa kwenye soka si muda mrefu kitawafukuza wawekezaji na mtarudi kwenye ufadhili, kitu ambacho CCM wanakiombea sana. Hii ya vilabu kuwa na uwezo wa kujiendesha msidhani inafurahiwa na wanasiasa. Angalia majina ambayo Singida Big stars wanamuita Mwigulu, mlezi, mdhamini, mfadhili tena eti wanamuomba.
 
Na ndio maana Simba na Yanga kamwe hazitakuja kumilikiwa na MO Wala GSM
 
Back
Top Bottom