Septemba 7 liandaliwe Tamasha la 4R za Mama awamu ya Pili. Tundu Lissu aachiwe kama sehemu ya uzinduzi

Septemba 7 liandaliwe Tamasha la 4R za Mama awamu ya Pili. Tundu Lissu aachiwe kama sehemu ya uzinduzi

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Bado tunaweka Mambo Sawa!

Tunajua 4R zilishafeli! Lakini kujikwaa sio kuanguka.

Muda wa kuonyeshana nani mkubwa umeshaisha. Tumeshaona Mkubwa ni nani.
Sasa Watibeli tunasema ni muda wa mkubwa na mdogo kuwa kitu kimoja. Masuala ya kutunishiana muda wake umeisha.
Tunajua Mungu ndiye Mkubwa kuliko, yeye ana uwezo na mamlaka isiyoisha. Yeye ndiye anaweza kuonyesha ubabe bila mipaka na muda wote autakao.

Inatosha! Na sisi Watibeli tumeona hivyo. Na Mungu kaona hivyo.
Inatosha!

Serikali, Rais na vyombo vya Dola. Mnaweza kuandaa awamu ya pili ya 4R siku ya tarehe 7 septemba bahati nzuri itakuwa ni jumapili. Siku hiyo viongozi wa dini na viongozi wa serikali watazindua awamu ya pili ya 4R katika muelekeo wa uchaguzi.

Chadema wapewe nafasi ya kushiriki. Wakikataa waachwe, wasilazimishwe. Tundu Lisu aachiwe.

Ikiwezekana apewe nafasi ya kuongea aongee na media zote ikiwemo TBC. Kama ataendelea na msimamo wake na hulka yake siyo tatizo ndani ya taifa.
Asindikizwe na Polisi mpaka nyumbani ikiwezekana.

Apewe mualiko najua hatakuja lakini apewe.

Msitunishiane misuli. Hasa uliyemkubwa.

Sisi watibeli tutawapa mbinu ya kulifanya tukio la siku hiyo kuwa lenye tija kwa taifa.

Hatuwezi kuishi maisha ya kuviziana viziana wakati sisi ni ndugu. Ujumbe huo upo bila ya sildi, kwani utendekaji wake ni kuanzia sasa mpaka mwezi ujao.

Na Mungu Mkuu mwenye Mamlaka yote awabariki. Na ujumbe huu usipuuzwe kwani ndani yake unamaana yenye nguvu ya kulisimamisha taifa letu. Na kinyume chake ni kweli.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikonmaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Kwahiyo hawakubalie wahuni?

Awakubalie kufanya nini?
Lisu anachopigania ni Haki lakini haki ambayo wakati wake haujafika.

Wahuni wanachokifanya ni HAKI kwa wakati huu kwa sababu wananchi hawataki Haki, uhuru, demokrasia, na wanaabudu masanamu.

Ulitaka Mungu awape Maisha mazuri watu wasiojua thamani ya uhuru, demokrasia, kuabudu utu badala ya pesa, kuheshimu tabia njema badala ya hadhi na cheo?

Tupo sehemu salama Mkuu.
.kumbuka hata Wahuni ni watu wa Mungu ambao mara nyingi hutumiwa na Mungu kuwanyoosha watu waliomuasi Mungu
 
✊🏿✊🏿
 
Bora waongee maana kuwapigania wajinga ni Kazi ngumu Sana mkuu

Ukisoma Kisa cha Waisraeli walivyokuwa Misri kuna wanaharakati wengi walitokea wakitaka kuwakomboa waisraeli watoke Misri kabla ya ujio wa Musa.

Mojawapo ya wanaharakati hao walitoka kwa Wana wa Efraimu. Moto uliwawakia kisawasawa
 
Kwa kuwa ameanza kukiri kwamba gerezani pabaya, hata wakimuachia ni sawa.

Lengo la magereza ni kwamba mtu ajutie kuwa huko. Lengo limetimia
 
Back
Top Bottom