Sera mpya ya faragha ya WhatsApp inavyowafukuza wateja

Sera mpya ya faragha ya WhatsApp inavyowafukuza wateja

Majibu ya huyo Admin wa telegram ni balaa.

By the way! Sioni kama hii ishu kwangu ina impact yeyote kwa sababu hata wakinijua kwani mimi naficha kitu gani?

Unakuta mtu hana lolote eti nae kabebwa na upepo wa faragha! Ujinga tu.
 
Manaongea sana lakini practically nani anawaza privacy policy tofauti na nyie wajuaji[emoji23][emoji23].
 
Kuna advantage ya Data collection ..inakuwa rahisi kwa customized ads kufikia ..kwa upande wangu sioni tatizo kabisa..kuhamia mitandao mingine kuna challenge ya kupata watu unaofahamiana nao
 
😀😀 wafanyabiashara wajanja sana, ss nikiongea na ww ukaongea kuna tofauti gani na normal call au whatsapp call?
Hujaelewa! Yaani hiyo feature ina work kama vile conference, kama ushawahi tumia Zoom Meeting utakua unaelewa! Em nambie whatsapp wana hii feature wapi???
 
Nilidhani wajanja ambao ni wasomi wangeachana na hii kitu lakini nimeona maprofesa wakiendelea kutumia whatsapp na kutoa taarifa mbalimbali kwa wanafunzi kama test nk..., wanafunzi whatsapp ndio imekuwa njia kuu ya kutumiana document mbalimbali za masomo.
Ni rahisi kumkuta mtu ana whatsapp bila telegram, but ni vigumu kumkuta mtu ana telegram bila whatsapp.
 
Whatsap itabaki kuwa whatsap kwangu, wachukue tu hayo madude wanayoyataka, kuna apps nyingi zipo kwenye simu zenu zinatumia hizo faragha bila wewe kujua.
 
Nimepakua hiyo signal wiki jana na nikaona contact list yangu kuna watu 5 tuu,
Muda mwingine najaribu kufikiria mimi naficha nini zaidi? I love you? Daah
 
Hakuna kama telegram kwa sasa. Toleo jipya lina "voice chat" hii ni kama radio call mnachat live kabisa na sio mpaka urecord afu utume hapana unaongea na mwenzako anaongea. Nineipenda sana hii
Hio si ni sawa na voice call tu au ipoje?
 
Njia nzuri ya kuficha taarifa zako ni kuacha kabisa kutumia mitandao, kinyume na hapo wala usijaribu kujifichaficha kwenye mitandao mingine kama signal nk.....biashara zinachezwa na wajuvi "life favors only prepared mind"
 
Kilichowaponza Whatsapp ni kuwa 'Honest', ki uhalisia Hakuna Mtandao wa kijamii wa Dunia ya Kwanza Usiofanya kitu wanachofanya Whatsapp. Walichofanya Whatsapp/Fb ni kukueleza tu kua Taarifa zako tutazitumia kibiashara, Je unafahamu mitandao mingine inatumia vipi taarifa zako? Njia rahisi ya Kulinda Faragha zako mtandaoni ni Kutokutumia Mtandao kabisa.
Kama alivyofanya Osama, alirudi stone age ndio maana iliwachukua muda mrefu sana kumpata
 
Hii Inshu yaweza kuwa pigo Kwa Zuckerberg, Tangu Mtaalamu Musk aponde hio sera mpya na kushauri watu watumie Signal App, wengi washaanza kuilalamikia WhatsApp.

Ukiangalia Musk ni mtu mkubwa sana(sasa hivi yupo Juu pale ya Mabilionea) kitu kidogo tuu atakachosema kinaondoka na lundo la watu..

Kuachana na hilo, hawa jamaa kama wana bifu fulani hivi la chini chini.
Zuckerberg ana mambo ya kise.nge sana. Ameona kama dunia yote ya social network ni yake.. akijichanganya anaporomoka na ndio nafasi ya mitandao mengine ya kijamii kupanda.. yenye uhuru
 
Back
Top Bottom