Sera ya kujitenga na masuala ya nchi nyingine "isolationism policy" ni zao la tabia za kibepari: Historia inayojirudia kimkakati Afrika

Sera ya kujitenga na masuala ya nchi nyingine "isolationism policy" ni zao la tabia za kibepari: Historia inayojirudia kimkakati Afrika

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,151
Reaction score
4,277
Mkakati wa kuhakikisha Afrika inakuwa tegemezi ni halisi kutokana na mipango mahususi iliyoandaliwa kwa muda mrefu na waliofukuzwa kama wanyonyaji au wakoloni. Kauli iliyotolewa na Rais Donald Trump inaonekana kubeba ukweli wa kutengenezwa kw sababu utegemezi wa nchi nyingi za Afrika na uvivu alioutaja wa viongozi wa Afrika siyo asili ya Afrika ila ni jitihada za makududi za kibinadamu kuhakikisha Afrika inatawalika.

Nyoka aliyelishwa na Afrika unga ameanza kuhitaji damu ni suala ambalo linafahamika haswaa. Kiongozi mkubwa huyu kutumika kuwakebehi viongozi wa Afrika ni sawa na Karl Peter angeamua kumkebehi Chifu Mangungo wa Msovero kusaini mkataba wa ulaghai ila hakufanya hivyo akijua sahihi ya Chifu Mangungo ni ulaji wake.
Asili inaonesha tunavyotegemeana katika mambo mengi kutekeleza kusudi la utu na uwepo wa binadamu ulimwenguni. Sidhani kama kujitenga na masuala ya jamii nyingine ya watu ndiyo utu na usalama wa watu Duniani.

Kauli hii ya kujitenga kutolewa na Kiongozi wa Taifa kubwa Duniani inaibua fikra za na kumbukumbu za kihistoria kuwa jambo kama hili lilishawahi kufanywa na Taifa hilohilo na madhara hayakuwa walengwa tu ila hata walengaji.

Dunia leo imeungana sana kisiasa, kiuchumi,kijamii, kiutamaduni na hata katika mawanda mengine kuliko kipindi chochote kile kuwahi kutokea. Kilo cha Afrika sauti yake Inaweza kuwa kelele kubwa Marekani. Hili siyo jambo la kushangaza katika zama hizi kutokana na utangamano jumuifu wa kijamii katika mawanda mapana.

Hili pia linatoa nafasi ya kuweza kubashiri uwezo na nguvu ya Taifa lenye nguvu " Super power" kuwa huenda kuna kinara mwingine anainuka hivyo mkubwa analinda hadhi yake nyumbani. Ni kama katika kundi la simba dume wengi ambapo simba kijana na shababi anataka kuchukua himaya.

Historia inapotukia lengo ni kufundisha, tusipojifunza tatizo siyo la historia.
 
Back
Top Bottom