Sera ya Kuwawezesha watanzania weusi ni ya lazima?



Hata Mengi amewezesha kwanza ndugu zake..angalia Elitiira, Benjamen, yaani wana pesa chafu!

Sasa mimi nikiwa na kiwanda changu nisiwape kazi kwanza ndugu zangu?
 

Hapo ndo ninakubali Mzee ES, siyo Sam Original wala FMES sauti ya umeme, aliposema kwamba "viongozi wetu ni reflection yetu sisi wenyewe".....
 
Hata Mengi amewezesha kwanza ndugu zake..angalia Elitiira, Benjamen, yaani wana pesa chafu!

Sasa mimi nikiwa na kiwanda changu nisiwape kazi ndugu zangu?

Well said,
Ndio maana tunasema, serikali ya Tanzania iwawezeshe watanzania.
Si serikali ya USA, UK, INDIA au KENYA itakayowawezesha watanzania bali ni serikali ya Tanzania.
 

Asante sana Mwita Maranya,wanaofikiria kwamba kuna haki sawa kwa wote dunia hii waende Bombay, London Beijing au hata hapa Nairobi kufungua biashara,Watakutana na vizingiti kibao!!
Mtu wa roho juu atafikiria ni ubaguzi, hapana ni wananchi wa nchi ile tu kwanza wanaofikiriwa na serikali zao kabla ya wageni.
Hivi tujiukize ni kwa nini kuna wimbi la wageni kutoka nchi hizo hizo kuomba uraia?.Ni kwa sababu wanataka kufaidika na rasilmali za kibiashara za nchi hii kama wazawa wenyewe.
 
 
.....sera za kibaguzi kama hizi za kuweka sera kwa kuangalia rangi ni kujirudisha nyuma tuu na ubaguzi ndio chanzo cha matatizo mengi katika jamii,sasa sijui kwanini tunataka kurudi huko? ubaguzi wa aina yeyote hauna nafasi katika free society ndio maana Mtikila na sera zake za magabacholi na Iddi Simba na uzawa wake wote waliishia kuanguka na kuwa obsolete!
 

"Hata kama rangi ya ngozi yako ni nyeusi lakini una mawazo ya kikaburu, basi hatutokuonea haya!, kwani wewe ni kaburu tu!"-late Mwl.Nyerere
 
hatuwezi kuendelea kuukumbatia mfumo wa kutubagua wazawa kwa kisingizio cha kuwabagua wao , wakati tayari wao wanatubagua. Cha msingi hapa ni wazawa kuwezeshwa ili waweze kuboresha hali zao, kuliko kugeuka omba omba ndani ya nchi yao. [/SIZE]

...just to the point & more specific,naomba unitajie sera yeyote Tanzania inayo mbagua mtu mweusi/mzawa au sera yeyote inayomweka mtu mweusi/mzawa in disadvantage position ya kushindwa kuendelea/kuboresha hali yake?
 
 
Fundi Mchundo,
Miaka ya 90 alikuwepo Mkurugenzi mmoja wizara ya elimu ya juu kama sikosei Ogondieki. Huyu bwana alikuja pale Arusha Tech. tukamlalamikia kwa nini UDSM hawatutaki sisi Mafundi mchundo tukasome pale? Jamaa akasema kuwa UDSM wanajitegemea na wao hawana uwezo wa kuwalazimisha. Ila akasema kuwa "...tutawasaidia kutafuta shule nchi za Ulaya Mashariki.." Ndiyo maana miaka hiyo ya 90 unakuta wanafunzi 300 wanakwenda Russia. Katika hao unakuta idadi kubwa sana ni vijana waliotoka vyo vya ufundi.
Unaweza kumuita Ogondieki M-BAGUZI? Mwite, ila waliofaidika na mpango huo leo hii wako wengi tu Tanzania na wakifanya kazi nyingi tu kusukuma mbele Tanzania na zaidi ya hapo ni kuwa hao jamaa na ndugu zao, maisha yao yamebadilika sana.
Acheni kuita watu wabaguzi. Haya ndiyo yaleyale ya "ukipigwa shavu moja, basi weka la pili.." Watanzania weusi wengi hadi leo wako tayari kufanya hivyo kwani dini na CCM inawaambia. Tunachosema ni kuwa hii idadi ipungue.
Huyu Mwarabu mwenye wajomba weusi, sijui nikuambie nini. Ila kutokana na kuwafahamu Wasudan, Wamisri, Ethiopia nk mara nyingi mnatabia ya kujiita Weusi au waafrica mkiwa na sisi. Mkishakuwa na waarabu mnaanza kusema "hao mipingo". Sikujui hivyo siwezi kukuhukumu wewe ni wa aina gani. Ila uongo mbaya ndugu yangu, wewe na hako ka weupe kako, tukaenda kijijini fulani huku Sikonge, mie ntalala peke yangu ila wewe UTAGOMBANIWA. Hii tayari tosha kusema "mwenzetu una nafuu..."
 
...just to the point & more specific,naomba unitajie sera yeyote Tanzania inayo mbagua mtu mweusi/mzawa au sera yeyote inayomweka mtu mweusi/mzawa in disadvantage position ya kushindwa kuendelea/kuboresha hali yake?

Mfumo uliopo sasahivi ndio unaowanyima wazawa fursa za kujiletea maendeleo.
Kwa mfano watu waliondolewa Bulyanhulu kwa mtutu wa bunduki na wengine kufukiwa ardhini ili kumpisha muwekezaji. The same applies to North Mara, Geita Gold Mine n.k. Je wazawa na taifa kwa ujumla tumenufaikaje na migodi hiyo?maisha ya wakazi wa kahama/kakola/Geita/Tarime/Nyamongo na maeneo jirani na hiyo migodi ni magumu kweli kweli.Kila siku hawa wawekezaji wanadai wanapata hasara, je nani mzawa anayethibitisha au aliyewekwa kulinda maslahi ya taifa ndani ya migodi hiyo?Je huoni kama ungekuwepo utaratibu au sera ya kuwawezesha wazawa waliokuwa wanaishi maeneo hayo yenye migodi, wangeweza kuingia mikataba na hawa wawekezaji ili wafaidike na rasilimali za nchi yao?
 
...just to the point & more specific,naomba unitajie sera yeyote Tanzania inayo mbagua mtu mweusi/mzawa au sera yeyote inayomweka mtu mweusi/mzawa in disadvantage position ya kushindwa kuendelea/kuboresha hali yake?

Koba,
Hivi vitu MILELE haviandikwi ila hufanywa. Tumeandika mambo mengi huko nyuma yanayoweza kumsaidia Mzawa wa Tanzania (wengi wao weusi na ndiyo masikini saana) kuboresha maisha yao.

Originally Posted by Sikonge
Nafikiri hapa watu wanachanganya mambo.
Tuseme sehemu zenye machimbo Tarime. Watu wanahamishwa na serikali kwa nguvu au kupewa PESA ili wahame kupisha uchmbaji wa dhahabu. Serikali yetu (hapa ndiyo inalalamikiwa kuwa haiendelezi Weusi) inatoa mfano wa ovyo kabisa. Wao kama Wasomi inatakiwa watoe mfano na kuwafundisha watu biashara. Kwangu mie ilitakiwa kufanya hivi kwamba, serikali kuwasaidia Wananchi kuingia mkataba na Wachimbaji. Wanahakikisha mikataba na Wachimbaji inafanyika na yenye faida kwa wananchi. Hayo maeneo yanabaki bado ya wenyeji, wageni wanayakodisha kwa hela nzuri tu. Serikali inakuwa inakusanya kodi tu na hizo pesa nyingine sijui wanaziitaje. Serikali kwa kufahamu UJINGA wa Weusi wengi, inaweka SHERIA kali kuwa Mgeni hawezi kununua ardhi. Sasa tuseme Barick akija na kusema kanunua hilo eneo, serikali iseme NO. Mwisho wa siku, wakulima hao wataanza kupata mwanga jinsi MAMBO yanavyokwenda. Watajua kuwa kumbe usiingie kichwa kichwa.
Kuna zile film za GOD MUST BE CRAZY. Yule Mzee nasikia film ya kwanza walivyomlipa pesa basi akaangalia yale makaratasi na akayutupa. Film ya tatu akawa kajua dola ni nini na akadai alipwe zaidi. Cha muhimu kwa watu hawa ni kwamba, wengi inabidi kuwafundisha nini maana ya kuwa na pesa kubwa. Kule kwetu walikuwa wakipata pesa za tumbaku, wanapata kichaa. Ukiwafundisha na kuanza kuwapata mwanga nini cha kufanyia hizo pesa, Duniani hakuna mtu mjinga.
Kwa kumalizia niseme kwamba, inaposemwa KUMSAIDIA MTANZANIA MWEUSI, sidhani ina maana ya kumpendelea tu. Kumuwezesha KIFIKRA hilo ndilo linatakiwa kwanza. Hawa watu wakiandaliwa na kupewa mwanga, watakuwa wazuri tu. Tatizo hata viongozi wetu hili hawalijui. Hata kama wakilijua bado wanalifanya bila MAANDALIZI. Hela za Kikwete si zimeliwa tu na wajanja? Hata kama zisingeliwa, huko kijijini, mjomba akizipata tu anaongeza mke wa pili.
Ukisikiliza history za Wayahudi, hawa kwa kutumia ma RABIN, huandaa watu wao mapema sana kibiashara. Wana nyimbo, funy story, misemo nk mingi tu inayomfumbua macho Myahudi katika dunia hii. Je Mtanzana anaambiwa nini? KWenye Dini ndiyo tunapotezwa kabisa. Methali zetu ndiyo hizo, Haraka haraka haina...., kawia ufike, mtaka cha uvunguni........ Kazi ipo.
 

Sasa unaona suluhisho ni kuunda sera zinazopendelea "wazawa" tu au kuhakikisha kuwa tunakuwa na sera zinazowapa watu wote fursa sawa na sheria zinazomlinda kila mtu bila upendeleo wa aina yoyote ile....?
 

Sikonge umetoa mfano mmoja mzuri sana.Nadhani fundi ano mchundo ama la anaufahamu mchundo ulivyo hadi kaamua kujiita jina hilo.Vijana wengi sana wa FTC wameweza kujiendeleza hadi kuwa na PhD kwa kupitia scholarship za russia ilihali UDSM iliwakataa.Lakini sasahivi UDSM imebadili muelekeo na inawasomba wengi kwelikweli.Na hayo ndio mabadiliko tunyoyahitaji ili kuwawezesha hawa wabongo ambao wameachwa nyuma kiuchumi.
Ukweli ni kwamba tunaposisitiza kuwezeshwa wazawa weusi tumejaribu kuona kuwa ndilo kundi ambalo kwa kiasi kikubwa limeachwa nyuma kiuchumi ukilinganisha na makundi mengine.Na hao wenzetu anaowazungumzia fundi kwa namna moja ama nyingine wana viji-connection na nchi nyingine kama india na pakistani.Na jambo la msingi hapa sio kuwazibia hao wenzetu ambao tayari wako vizuri, kinachotakiwa hapa ni kuwawezesha watanzania wazawa ambao wameonekana kuachwa nyuma kimaendeleo na kiuchumi ndani ya nchi yao.Hapo hakuna ubaguzi fundi ni suala la kuwavuta hawa walioachwa nyuma.
 
Sasa unaona suluhisho ni kuunda sera zinazopendelea "wazawa" tu au kuhakikisha kuwa tunakuwa na sera zinazowapa watu wote fursa sawa na sheria zinazomlinda kila mtu bila upendeleo wa aina yoyote ile....?

Ni muhimu kuwapa upendeleo huo ili waweze kukabiliana na hali halisi iliyopo. Kwa sababu katika hali halisi iliyopo wazawa wameshindwa kupata mafanikio ya kiuchumi na kimaendeleo kutokana na mfumo uliopo. Sasa inahitajika nguvu ya kipekee ili kuweza kuwakwamua lakini wakati huo huo bila kuwaathiri hao waliofanikiwa. Ndio maana tunasema wazawa wanahitaji kuwa empowered.
 
Fundi Mchundo,
Mkuu wangu ni lazima tuwe wakweli tunapojaribu kushinikiza hoja hapa. Huyo mwanzilishi wa hoja hii ya WAZAWA mh. Idd Simba asili yake ni Burundi, hivyo weusi wake pekee hauwezi kumpa nafasi ya kumwezesha kutoa madai haya bila kuwa ametazama mbali zaidi..Tusichukue njia za mkato kuna maana zaidi ya kusema mzawa ama mweusi hivyo tusitumie neno kwa neno kutafsiri hoja.. inakuwa kama tunatafuta makosa ya kiuandishi au tunajaribu kupotosha maana na malengo ya mada nzima.

Binafsi, naamini mzawa ni Mtanzania mwenye asili na nchi hii iwe kwa kizazi kwani kuna Waarabu Washihiri wamefika Tanzania toka enzi za majahazi ya pepo za monsoon, sijui karne ya kwanza!.. duh!.Na pengine wameishi Tanzania kablka hata nusu ya makabila mengine yahaja immigrate Tanzania. na tatu kubwa kuliko yote nchi yetu inaitwa Tanzania sio Tanganyika tena hivyo kuna kila watu wenye rangi tofauti..Hivyo mkuu ondoa mawazo machafu yanayojengwa na tukate issue pale penye mwelekeo mzuri ya kuelewa nini kinahitajika.

Hivyo usichanganywe na matumizi ya neno mweusi, zaidi ya kuwa mzawa anayehitaji kuwezeshwa kiuchumi. Binafsi nimeweza kuchambua pumba na kutoka na mchele ambao ndio mawazo yangu yanakolenga.. Kupinga weusi ni muhimu uje na hoja inayoweza kuonyesha wazi kwamba hakuna haja ya kumwezesha mtu mweusi..
Unapotumia neno sera ambayo inamweka mweusi ktk disadvantage position ni muhimu kuelewa kwamba kutokuwa na sera inayomwezesha ndio sababu ya mada hii..
Kama mzazi ukishindwa kumwesha mtoto wako kufika shuleni ambayo ni kilometre 10 kwa madai kwamba hakuna mtu aliyemzuia kutembea wala barabara hazikufungwa kumzuia kwenda shule ni moja ya kukaa majukumu ya uzazi (Uongozi). Dhahiri serikali kwa mfano huu huwapa ride wageni kwenda shule na pengine kifuko cha lunch kutokana na kifuta jashoi kinachotoka upande wa pili..

Wanachoomba wananchi ni kwa viongozi wetu kuwatazama wazawa kama watoto wao wenyewe, hawakatazwi kumlea mtoto mwingine wa nje kwa haki sawa na huyu aliyepo, lakini wakumbuke huyo mtoto wanayemlea ana baba na mama yao ambaye hulipa child support ile unayoona kifuta jasho (10%), na ndio sababu wewe unampa nafasi zaidi ya mwanao mwenyewe wa kumzaa, hiki ndio kilio cha Watanzania.

Maendelo ya mtu, jamii yeyote au nchi yanatokana na kuwezeshwa, masharti rahisi kwa wote iwe wageni ama wananchi wake kukata elimu, ajira. uwezo wa mikopo kufungua biashara na hata kama hawana idea ama vision ya maisha yao wenyewe unaweza kuwapa ushauri na nguvu ya kwenda kukopa benki..Leo hii mwekezaji toka nje anapewa tax excemption kirahisi tena hadi Corporate tax kuwekesha nchinilakini raia inakuwa mvinde kupata nafuu ile ile. sasa hapa hakuna ubaguzi mbona hatuwaoni wao kwa rangi zao kuwa wanapewa nafuu ambayo mtu mweusi haipati isipokuwa kwa mbinde na baadhi tu ya biashara tena walizochagua wao! Mzungu hana mipaka na nakuhakikishia hata hao waliofungua viduka Airport wamepewa tax execemption lakini ukienda wewe machinga utaambiwa lipia kodi..

Hakuna yeyote tajiri Ulaya ambaye anatembea na cash kufanya biashara zake wote wanawezeshwa na benki hizi na ndio maana serikali zao zimefikia maamuzi ya stimulate uchumi wa nchi hizo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wananchi wanaweza kukopa benki kuendesha biashara zao. Tazama mabillioni ya Kikwete yamepelekwa saccos na bado wananchi wanapata taabu kubwa kuzipata fedha hizo hata zile walizoweka wenyewe kujiandisha uanachama. Meaning Saccos wame invest fedha za wananchi sijui wapi haziwezi kutoka hadi zi mature wakati wananchi wenyewe hawana record wala taarifa ya jinsi fedha zao zinavyozaa ama kufa.

Pengine swala kubwa kwa wapinzani lingekuwa mnataka serikali imwezeshe mwananchi VIPI!...maanake tunaposema kumwezesha mzawa ama mtu mweusi pekee haitoshi...
 

Aisee wewe ni mtu hatari sana na natumaini haupo katika nafasi yoyote ya kuweza kutunga sheria ama sera unazozipigia debe hapa maana tutadumbukia katika shimo la chuki na ubaguzi usio na nafasi katika jamii yoyote ile iliyostaarabika!!
 
Kama Mtanzania mweusi ndo kigezo cha uzalendo ..je utaelezeaje uzalendo wa Issa Shijvi na kumlinganisha na wezi wa EPA ambao wengi wao wana ngozi nyeusi??

Nini maana ya Mtanzania mzawa Mweusi? Maana Regnaldi Mengi naye ni mzawa mweusi pia! Je pia naye tuna nuia kumkomboa kwa kumpa fursa?

Hii hoja inaweza kuashiria ubaguzi!
 

Sikonge Mkuu. Unachanganya vitu. Hapa tunazungumzia ubaguzi wa rangi. Huyo Ogondieki angesema ni mafundi mchundo wanaotoka sehemu fulani au wa rangi fulani ndiyo pekee wangepewa nafasi ya kwenda kusoma nje, ningemwita mbaguzi. Nyinyi mngesema wawezeshwe watanzania wote wasio na uwezo bila kujali rangi, dini au jinsia, ningewaunga mkono. Kutanguliza kwenu uzawa au weusi kama kigezo ndiko ninakopinga. Kwa nini mtoto wa Mengi apendelewe kwa sababu tu ni mweusi wakati mtoto wa mvuvi wa kishihiri anyimwe upendeleo kwa sababu tu babu wa babu yake alitokea Yemen?

Halafu unamhukumu kijana wa kiarabu kwa upumbavu wetu wa kuenzi vilivyo vyeupe? Mbona hata katika makabila fulani, mahari inapimwa kutokana na rangi ya binti? Haya ni mapungufu yetu na kamwe hatuwezi kuwalaumu wengine kwa hili. Ndiyo, ni wao ndiyo waliotufundisha kuwa kilicho cheupe ni bora lakini miaka zaidi ya 40 baada ya kuondoka kwao ni lazima tujiulize kwa nini bad tunaona hivyo! Hata hii sera yenu ina muelekeo huo huo. Tunajiona hatuwezi kushindana na walio weupe zaidi bila kupewa upendeleo. Mimi hiki nakipinga kwa nguvu zote. Nimeshindana nao na wengi nimewashinda. Sihitaji nipendelewe ili nijijue kuwa hatupishani kitu. Sihitaji kukubalika na mhindi, methiopia, mwarabu ili nijione kamili kama vile yeye asivyo nihitaji mimi ili kulegitimise uutu wake.

Amandla......
 

Hii hoja ni ya kibaguzi, fullstop.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…