Sera ya Kuwawezesha watanzania weusi ni ya lazima?

Issue sio ubaguzi ni uwezeshaji.

ishu ni ubaguzi katika uwezeshaji!.
awezeshwe nani?, KILA MTANZANIA ANAYEHITAJI KUWEZESHWA BILA KUJALI RANGI YAKE AU TUZINGATIE RANGI YA NGOZI YA MTU KABLA YA KUMUWEZESHA KILA ANAYEHITAJI KUWEZESHWA?
 
 
Mnaotetea "wazawa", tusaidieni kutuelewesha , labda mnapozungumzia mzawa, mna maana ya mtu wa namna gani?
1: Mtanzania mweusi bila kujali mahali popote alipozaliwa duniani?
2: Mtanzania yeyote aliyezaliwa Tanzania bila kujali rangi yake?
3: Mtanzania yeyote aliyezaliwa mahali popote ndani au nje ya Tanzania?
4: yeyote aliye Mtanzania?
 


Sera zote zilizowekwa baada ya uhuru zilikuwa na nia ya kumwinua mtanzania mweusi bila ya kumtenga mwingine. Shule zilizokuwa zikiwabagua zilitaifishwa na watu wote kupewa nafasi ya kusoma BURE. Biashara zilizokuwa zikimilikiwa kwa kiasi kikubwa na wasio weusi, zilitaifishwa, na watu weusi kuwekwa kuziendesha. Maghorofa yaliyokuwa yakimilikiwa na watu wasio weusi yalitaifishwa na watu weusi kupewa kipaumbele katika kupanga humo. Yote haya yalifanywa bila ya kuwa na sera ya uzawa maana ilijulikana ukimlenga mtanzania wa kawaida, sehemu kubwa mno itakuwa ni weusi. Sasa mtuambie, ni kipi kigeni ambacho sera yenu ya kibaguzi itafanya ambacho hakijajaribiwa kama sio kuhalalisha ubaguzi dhidi ya mtanzania mwenzetu?

Ubaguzi tunaujua pengine kuliko unavyodhani. Tumeushuhudia na tumebaguliwa.

Kwa taarifa yako yote hayo ya ma_skinhead, Jim Crow na mengineyo yalianza kwa sera ( imani) kama hizi unazozipigia debe. Wote hao walianza kwa kumtofautisha myahudi, mtu mweusi na kuwatwisha mizigo ya matatizo yao. Wayahudi walidaiwa kuwa hawachanganyiki na wengine, wanahodhi pesa, wanawadhulumu wengine kama vile sisi tunavyodai dhidi ya wahindi. Huko ulaya ya sasa, imani imejengeka kuwa watu weusi ndiyo wanoleta uhalifu, wanayang'anya kazi wazawa, wanaishi kwa kutegemea hela kutoka Social Services, wavivu, wachafu, wanawarubuni wanawake zao n.k. Ni imani hizi ndizo zinazowapa kiburi Skinheads kuwatosa weusi kutoka kwenye treni, kuwapiga wanapowaona n.k.

Mtikila alipoanzisha usemi wa Gabachori, vijana waliisha anza kutoa vitisho kwa wahindi! Leo mkipitisha sera hii ya kibaguzi, mnahalalisha dhana ya kuwa mhindi anahitaji kudhibitiwa. Ni hatua fupi toka hapo hadi ambapo vijana wataona ni halali yao kuchoma maduka yao na kuwapiga wakiwaudhi.

Hatuhitaji ubaguzi wa aina yeyote (positive au otherwise) katika nchi ambayo sisi ndiyo majority, sisi ndiyo tunaotawala, sisi ndiyo watendaji wakuu serikalini n.k. Huko mnakotaka twende ni slippery slope.

Amandla......
 
 

- Full Stop!
 
Sera ya uzawa kwa maana ya kuwapendelea weusi ni sera ya Kirundi ya miaka ya nyuma hukooo....ambayo iliwapendlea Watusi katika masuala ya elimu na biashara na kuwaacha Wahutu wakiwa watumishi wasiokuwa na hadhi.Hii ni aina ya ubaguzi ambayo Simba alitaka ifuatwe.

Simba aliona jinsi ilivyowainua Watusi wa huko kwao na akadhani itakuwa na matokeo mazuri hapa Tanzania.Ubaguzi wa aina yoyote ni ubaguzi tu.Ukianza kuwabagua watu kwa rangi zao au pua zao utakuwa unazalisha chuki.Baada ya vita na maafa Burundi iliachana na sera hiyo na sasa Warundi wote wana fursa ya kujiendeleza bila ubaguzi.


"Hata kama rangi ya ngozi yako ni nyeusi lakini una mawazo ya kikaburu, basi hatutokuonea haya!, kwani wewe ni kaburu tu!"-Mwalimu Nyerere alitamka haya baada ya Simba and Company kutaka kuleta sera za uzawa...
 
Wadau ,wachangiaji wengi hapa wanalinganisha uzawa na ubaguzi, versus uwezeshaji wa waTanzania.Nafikiriri hii argument ukiichukua namna hii in three dimensions si rahisi kupata jibu la matatizo yetu waTanzania.
Ubaguzi utabaki kuwa ubaguzi dhambi ambayo tumeikana siku nyingi.
Hata hivyo suala la uwezeshaji wa watanzania litabaki kuwa pale pale.Hatuna mjomba wa kutuendeleza,kama tulijaribu tukashindwa ni vema tuka analyse tulishindwa wapi na tundelee wapi katika kuwawezesha watanzania.
Admitting to failure and doing nothing anbout it is much worse, nikama kukubali kurudi utumwani kwa sababu ati umeshindwa kujiendesha .We must try, we may fail, but we must try again.
 

Sera zinatakiwa kuwalenga Watanzania wote bila kujali rangi zao ama asili zao,Watanzania ambao ni maskini na wanahitaji kuwezeshwa ili wajikwamue.

Kwa kuwa tatizo linalotuumiza vichwa ni umasikini wetu ni vema tukalenga kila mtu ambaye ana akili timamu na ana haja ya kufanya kazi kwa bidii katika nyanja anayoipenda basi awezeshwe kwa kupewa mtaji wa kuanzia kama ni bishara au kilimo.

Sera za mabenki zibadilike ili wanyonge nao waweze kupata mikopo na wafanye shughuli zao kwa usimamizi mzuri ili waweze kulipa mkopo na kuendeleza shughuli hizo.

Sera za aina hii zisinaglie rangi ya mtu bali uwezo wake wa kusimamia na kuongoza shughuli zake.
 
The government as an institution of the people should work for all people, policies devised and laws enacted should not in anyway discriminate against people based on their color,ethinicity or religion. therefore there must be an equal opportunities to all, and incase there is a need to help any group within the society, the help should be provided to all who are in need without discrimnating against them based on their color ethinicty or religion.

The premise that "we are just trying to help blacks not discriminating other people" is wrong, because the human need has no color, the notion that you are helping a poor blackman and at the same time refusing to help the poor "hindiman" even though both are Tanzanians, IT IS WRONG!

You can not exclude people and then expect them to be inclusive. what will a poor Indian man be proud of Tanzania if Tanzania itself dont want to give him a hand to lift himself from a pit of poverty. how will he be willing to fight for Tanzania to defend it?

IF RACIALISM IS A DISCRIMNATION BASED ON THE COLOR OF THE SKIN THEN HOW CAN DISCRIMNATION BASED ON THE COLOR OF THE SKIN BE NOT RACIALISM?
 
Ehhh Wajameni,
Naona kuna watu humu wagumu kuelewa. Hatujasema mtu mwingine asiendelezwe. Hatujasema uanza ubaguzi wa Mrema wa Gabacholi. Hatujasema Mhindi anyimwe Mkopo, misaada na takataka zote. Hapa tunasema juu ya kitu kidogo sana.
Watu weusi wengi wako chini sana. Sasa mara nyingi duniani Wahindi husaidia wahindi. Waarabu husaidia waarabu. Mzungu husaidia Mzungu. Sasa sisi mipingo nani atusaidie? Mengi anaajiri Wachaga wengi kuliko kabila jingine. Sababu ni kwamba kwanza ni wengi anawafahamu, ndugu zake, jirani, rafiki nk. Sasa sisi Mipingo wengi tumezungukana wenyewe kwa wenyewe na UMASIKINI wetu.
Ukienda nchi nyingi za Ulaya, high technology nyingi zinafundishwa vyuo vya kijeshi. Huko unakuta wanachagua watu wao tu na wewe hata uwe Mchanganyiko, huwezi kuingia huko ndani. Kuna siku naangalia kiwanda cha BMW, kiwanda kizima sehemu ya designing, hakukuwepo mtu mweusi, Mu-asia wala mchangayiko. Wote Wazungu na Wageruman. Hao unakuta hata chuo walichosoma hakijulikani. Kila nchi lazima iwe na siri zake. Huwezi ukawa umejianika uchi uchi tu. Lazima na sisi tuwe na CHUMBANI kwetu ambako ni zaidi ya Ikulu. Sehemu kama pale Nyumbu, palitakiwa kuwa pameendelezwa na kuwa na chuo kimoja kikubwa sana.
Tunaposema kuwa mtu mweusi awe mfanyabiashara, simaanishi kuwa kila Mtanzania awe tajiri na mfanya biashara. Ningelifurahi kuwa kwa kuanzia watafutwe vijana wenye kuonekana na talent ya kufanya biashara. Waanzishiwe secondary yao itakayokuwa ni ya JESHI (Hapa mgeni hapendwi na unajua tena siri ya jeshi kama mtu akiuliza) na huko iwe ni kufundishwa kufanya biashara tangu wakiwa wadogo. Wafundishwe jinsi inavyotakiwa kuwafundisha na watoto wao baadaye tangu wakiwa wadogo. Kama kila mkoa tukipata vijana 20 kila mwaka, na wakarudi na mawazo mapya, ujanja wa kufanya biashara nk, basi baada ya miaka 10, tutakuwa na MATAJIRI wafanya biashara WEUSI wakubwa sana, wakishindana na Wahindi, Wazungu, Wachina nk. Huko maishani wataachwa washindane na wengine bila upendeleo wowote. Hawa watakuwa mfano wa wengine weusi. Watatoa ajira. Ikibidi ndiyo wawe hata OWNERS wa ATCL, TRC, Mabenki ya Tanzania nk kwa masharti kuwa hawawezi kuuza share zao bila ya kuijulisha serikali. Ikifikia Mikoani wamefika vijana kama 200 yaani mradi uwepo kwa miaka 10, hiyo shule inaweza kufungwa na kuanza kuangalia jinsi hawa vijana wanavyoshika uchumi wa Tanzania kidigokidogo. Kama huko njiani wataanza kuingia ushirikiano na Wahindi, Wazungu, nk it is well and good.
Ukitaka kusema kutengeneza Matajiri weusi kama 1,000 huku wakiwa wafanya biashara ni UBAGUZI, ok. Call me Mbaguzi. Ila ubaguzi wangu ni ule anasema nyani "Ubaguzi positive". Na ikionekana kuwa mipingo wengi wanaendelea vizuri, basi unaweza kukipanua hiki chuo na kukifanya chuo cha biashara na watu wengi wakaja kusoma ila unapunguza baadhi ya vitu maana huwezi kugawa kila kitu dunia hii.
 
Badala ya kulalama dhidi ya wenzetu, tujifunze kutoka kwao. Wakati tunalalamika kuwa hatuna uwezo wa kujikwamua, tunaendelea kuendekeza michango isiyo na manufaa kwa jamii. Kama tungetumia muda na resources tunazoweka kwenye harusi, kitchen party, kuvunja vikao, kubarikiwa watoto, misiba ( si kuuguza) n.k. tungekuwa mbali. Tuko tayari kukaa na kuingia gharama ya vikao vya mwaka mzima ili kuhakikisha kuwa mwanetu anaoa au kuolewa kwa mbwembwe! Mapesa yote tunayokusanya tunapelekea kuhakikisha kuwa waalikwa na wasio alikwa wanakunywa na kusaza. Ni mara chache sana sehemu ya michango hiyo imepelekwa katika kuwawezesha mahurusi katika maisha yao mapya. Tukijitahidi ni kafriji lakini hata siku moja hatusemi hizi ni ada ya shule ili ujiendeleza, mtaji wa kununua/kupanga sehemu ya kufanyia biashara. Hapana, sisi ni kunywa na kula tu! Mara ngapi tumeweka vikao vya kuwatafutia ada watoto wetu? Mara ngapi tumekaa vikao vya kuchangia tiba ya mwenzetu? Hata hapo tukikaa kuchangia tiba, michango yake hata siku moja hailingani na ile ya kwenye harusi!

Mara ngapi sisi tulionazo tumejenga madarasa au kuezeka shule zilizo jirani yetu? wa ngapi katika sisi tulioenda katika vituo vya watoto yatima na ku-adopt mmoja wao? Ni wangapi, huko tunakotoka tumefanya juhudi za kuleta tofauti katika maisha yao? Wangapi, tukiwa likizo, tunajitolea kutoa ushauri, kufundisha, kujenga bure kwa wale tuliowazidi?

Wenzetu yote haya (kupeana mitaji n.k.) wanafanya kwa jamii yao. Kwa nini tusiwaige badala ya kutaka serikali yetu wote iwatilie kauzibe?

Uwezo wa kujikomboa tunao na wala hatuhitaji upendeleo. Tunachohitaji ni kufungua macho na kuanza kujiamini katika tunachokifanya. Ni hicho tu.

Amandla......
 

Hivi leo Tanzania kuna UBAGUZI? Jibu ni hakuna. Sasa nikashika kundi la vijana na kuwapa KALUFUNDI ka kufanya biashara pamoja na mtaji kidogo kama Mkopo inakuwa ni UBAGUZI? Nimembagua nani? Mwisho wa siku ni SERIKALI yenyewe itaamuwa nani akasome na nani asisome. Ni kama ilivyokuwa Tabora Girls na Boys. Kuna vijana maalumu walikuwa wakisoma hapo. Mna maana Nyerere alikuwa Mbaguzi siyo? Kuna watu hapa neno UBAGUZI wanali-copy na ku-past kila sehemu. Hebu tuondoleeni hizi habari zenu mnazotaka kutupandikiza. Kama twataka kuendelea lazima tujifunze KUUMA na KUPULIZA. Mataifa yote duniani yanafanya hivyo. Hii hutakuta imeandikwa POPOTE. Ila wanafanya. Sisi tukifanya basi eti tumekuwa WABAGUZI. Kwa taarifa yenu ni kuwa kama leo akionekana Mhindi au Mwarabu au Mzungu anataka kugombea Urais na final wanafika na Lowassa au Mramba au ......... basi milele lazima ujuwe kwamba NTAMCHAGUA NGOZI NYEUPE. Si kwamba ntamchagua kwa ngozi yake, ila kwa matendo yake.
Muda UFIKE sasa Tanzania ile iwe na BALANCE. Hii kitu ya kutokuwa na BALANCE siku moja inaweza ikalipuka. Hapo na ubaguzi wenu mnaoukataa mtaona kumbe ulikuwepo. Siku moja atakuja Mswahili, mwenye maneno matamu kama Obama au Hitler aseme jinsi Wahindi, Waarabu na Wazungu walivyoshika Tanzania. Atatoa na mifano kibao. Kitakachofuatia kila mmoja wenu anakijua. Hii BALANCE itakuja zuia upupu kama huu. Sasa kama hamtaki basi SUBIRINI. Mrema aligusia na jambo likanyamaza. Si kuwa limekufa ila lipolipo linaiva taratiiiibu likisubiri kama JIPU siku moja LIPASUKE.
 

Fundi,
hapo ndipo nasema unajaribu kupotosha mjadala.Hatujasema popote kwamba hao waliofanikiwa wawekewe kauzibe hata kidogo, wataendelea kujipambanua kama kawaida. Halafu unajadili hii mada kama vile hakuna wazawa ambao ni weusi na wana hali bora, badala yake unajaribu kulazimisha kuwa tunawabagua weupe.
Hivi fundi unataka kutuambia kuwa hao wazungu unaotaka tujifunze kutoka kwao hawaoi na kuolewa?unataka kutuambia kwamba tatizo la watanzania ni elimu?hawajasoma?unataka kutuambia kuwa hao wote waliofanikiwa kiuchumi wamesoma sana kuliko hao waswahili wasiofanikiwa?haiwezekani hata kidogo.
Fundi, je ni mara ngapi hao wenzetu waliofanikiwa wamekwenda kwenye hivyo vituo vya watoto yatima na ku-adopt walau mmoja?madona si katoka zake marekani akaja ku-adopt mnyasa na bado mkamshutumu baba wa mtoto?
Suala la kuchangia harusi, misiba, kitchen party, vipaimara n.k vinafanywa na kila mtu awe anazo au hana.Sasa kama mtu anaoa au anaolewa wanajamii wenzake wakaamua wamsaidie angalau friji ili apate maji ya kunywa ya baridi wewe unaona nongwa?Tunapozungumzia uwezeshwaji lazima tuangalie ukweli wa mambo tusiishie kutoa mifano ambayo inaendelea kutufunika macho, tusijikite katika nadharia wakati hali halisi inaonyesha watanzania wengi ni maskini wa kutupwa.
Je unaweza kujua ni wakulima wangapi wameweza kukopesheka kutoka katika taasisi zetu za kifedha?je ni watu gani wanaoendelea kuhangaika na kilimo cha jembe la mkono huku wakitegemea kudra za mwenyezi Mungu alete mvua
ndipo wapate angalau mavuno ya kuwakidhi kwa kipindi kifupi?ni akina nani wanaofaidika na mikopo kutoka taasisi za fedha kama sio hao hao waliofanikiwa?je huoni kuwa kuna umuhimu wa kuwawezesha hawa wakulima wasiokopesheka ili wajinasue kutoka lindi la umaskini?Ulishawahi kuwaona hao wenzetu wako barabarani wanaombaomba?Juzi juzi hapa katibu tawala wa mkoa wa Dodoma aligoma kuwapokea ombaomba waliokuwa wamerudishwa dodoma toka dar es salaam, huoni kuwa watu kama wale wanahitaji kusaidiwa?na hukuona kuwa wote walikuwa mipingo kama anavyosema sikonge?
Swali la mwisho kwenu mnaopinga wazawa kuwezeshwa, je mmefanya nini kuwasaidia au kuwawezesha hao wenzenu wasiokuwa na uhakika wa mlo hata mmoja?au kwakuwa mmefanikiwa mnataka muendelee kuwa peke yenu ili muendelee kusujudiwa?
 
Fundi Mchundo na Sikonge ninyi mwanena, hiyo sio ubaguzi na ndio uwezeshaji unaoangaliwa hapa. Ubunifu katika kuwezesha ni kuona jinsi gani tunaweza ongeza kauwezo ka baadhi ya watu kusonga mbele, kama ilivyofanywa hapo nyuma kidogo, zilipoanzishwa shule maalumu, NAYO wengine wataita UBAGUZI??????????.
Basi tuwe na vikundi kulingana na karama zao tuviendeleze ili jamii nzima ifaidike.
 

FM,
Haya ninayoandika muda wote si wenzetu wanafanya hadi kesho? Wana vyo vyao vya kijeshi, hospital za jeshi ambako hata Rais anatibiwa? Tz ilikuwa iwe Lugalo ila siku hizi hata Kikwete anaikimbia. Sasa na sisi tukiwa na kisehemu chetu kama wanavyofanya wenzetu hiyo ni dhambi? Si unasema tujifunze kutoka kwao?
Kuhusu kufanya SHEREHE badala ya kusaidia mipango ya maendeleo, nafikiri nililiandika jana kuwa Wananchi wapatiwe shule. Ukiwapa tu hela kama zile za Kikwete basi Wataowa wake wengine na kuweka LCD ukutani.
Nataka niseme tena na tena "Hakuna anayesema serikali iweke KAMZIBE". Mambo yawe kama yalivyo. Ila Mipingo kadhaa au wapate upendeleo fulani wa KUJIFUNZA kufanya biashara. Huu upendeleo USIENDE kwa kuwazibia wengine. Huu upendeleo HAUTAGUSA WATZ wote. Hivyo utaona kuwa Hata baadhi ya mipingo hawatafaidika na mpango huo moja kwa moja. Ila ukifanikiwa basi hao watakaokuwa wamesoma watasaidia kubadili tabia ya Mipingo wengine. Kila mtu ana dream kuajiriwa tu Tanzania. Ifike wakati mtu anaota kufanya biashara.
Kama serikali ikitaka, itafanya na HAKUNA atakayejua hata kama hii kitu kinafanywa kwa upendeleo. Ili kuwaridhisha Watu kama nyie basi wanaweza chukua Wahindi Wawili na Waarabu wawili ili mtu akiuliza waseme tuna hadi Wahindi na Waarabu hapa. MMERIDHIKA?
FM, kama ungelijua mie hasa lengo langu la hizi shule KUBADILISHA TABIA ZA WATANZANIA. Ukiwabadilisha na wakaacha hizi party, minuso, ngoma na sherehe za kila aina na wakaanza kuchangia mipango ya maendeleo, basi nina uhakika tungelifika mbali. Juzijuzi nimechangia harusi ya mdogo wangu na baada ya siku mbili tatu watoto wa kaka yangu hawana ada basi imebidi nikope na kulipa hela zaidi ya mara 20 ya pesa nilizolipa kwenye harusi. Haya usiniambie mie, mie nayafahamu. Ila ndugu zetu wengine wanayafahamu? Utawaambiaje? Serikali inaweza tumia uwezo wake kubadili huu MNYORORO wa kushindana "Harusi yao imetumia milioni ...... ila yetu ilikuwa kali zaidi maana tumetumia mara mbili zaidi..."

Kwa ufupi ni kwamba:-
1. Tutengenze kikundi cha MATAJIRI wafanya biashara MIPINGO. Hiki kiwe kikundi kidogo sana ukilinganisha na idadi ya Watanzania. Hapa ndipo nakubali kuitwa Mbaguzi, ila niite Mbaguzi POSITIVE.
2. Kubadili tabia za Watanzania. Hii ihusishe Watanzania wote hata kama ni Mzungu au Mhindi. Serikali iwe bega kwa bega kusaidia watanzania katika maisha yao. Ikibidi kupiga marufuku vitu visivyo na faida basi wafanye au hata kuweka LIMIT. Hapa inaingia sasa neno MZAWA. Mfano ni kusaidia kuweka mikataba na wachimbaji madini kwenye maeneo yao. Kuhakikisha watu hawa wanafaidi na wao keki. Ila sasa linakuja lilelile la mwanzo. Wakipata hela Mipingo patakuwa hapatoshi. Hapa sasa inakuja shule kwa WAZAWA wote bila ya kujali RANGI ili ukipata hayo mamilioni USIISHIE Mirembe Hospital au Kuyavaa MAWAYA na kugaia dada zetu vigari vyekundu.
 

Ndiyo. Tatizo kubwa la watanzania ni elimu.

Hakuna mtu anayepinga mtanzania asiye na uwezo kuwezeshwa. Tunachopinga ni huku kuwezeshwa kufanywa kwa misingi ya rangi kama ambavyo sera yenu ya uzawa inavyotaka kufanya.

Nimetoa mfano wa michango ya harusi n.k. ili kuonyesha jinsi priorities zetu zilivyokuwa warped. Tofauti na wengi wa wenzetu, mambo hayo wanayafanya kwa uwezo wake na pesa za ziada. Harusi ya mtoto wa Bill Gates hata siku moja haiwezi kufanana na ya Fundi Mchundo. Sisi tuko tayari kukopa, kubembeleza kwa watu tusiowajua ili mradi tu kwa siku moja na sisi tuonekane watu. Hao tunaowapigia kelele sasa hivi walianza biashara zao kwa mali kwa mali. Walienda jamatini kwao ambako wenye nazo katika jamii zao waliwasaidia kwa kuwapa mitaji na ushauri. Hawakuanzia kwa mikopo ya benki. La, hasha. Walidunduliza walicho nacho na kujibana hadi walipopata mafanikio. Kama vile ndugu zetu wachaga wanavyoanza kwa kupiga brashi viatu hadi kumiliki duka. Hawaendi benki hawa bali kwa juhudi zao na msaada wa jamii zao wanajiinua. Sasa sisi, maskini wa kutupwa ( maneno yako) tunampa friji bila kujali kama ana uwezo wa kulipia luku!

Nyinyi mnadai upendeleo ati bila ubaguzi wakti kigezo mnataka kiwe rangi! Kwa mtazamo wenu kama watanzania wawili watahitaji msaada basi bila shaka asaidiwe mweusi hata kama hatimizi masharti na ana historia ya kutolipa madeni yake!

Makabila mengi hayaombi ombi kwa vile kwa mtazamo wao ni heri kufa njaa kuliko kujidhalilisha kiasi hicho. Hata hawa unaowapigia kelele, ukienda walikotoka mababu zao utakuta wako omba omba. Mimi sioni sababu ya kumsaidia mtu aliyeamua kuomba omba kama njia rahisi ya kujipatia kipato. Wengine wana uwezo mzuri tu (ng'ombe n.k.) lakini wameamua kuomba!

Hata nikikuambia kuwa nimewahi kuwasaidia haitakusaidia kitu maana haunijui na hauna njia ya kuhakikisha nisemacho. Tubaki kwenye hoja.
 
Tatizo kubwa ni UMASIKINI wa nchi na watu wake wote.Kuonekana kwake kuwa weusi ndiyo waathirika zaidi na umasikini huo ni kwa sababu wao ni majority.

Kwa kuwa ni wengi basi hali ya uduni wa maisha inaonekana kwao zaidi.Ukiangalia mambo kwa mtazamo huo utakuwa unawaacha kando maskini wengine ambao kwa uchache wao unadhani hawana matatizo.
 
 
Sikimbii hoja. Mimi ni mmoja katika hao ambao wanatakiwa kuwasaidia wenzake kujitoa katika umasikini. Isipokuwa mimi simlaumu mtu mwingine yeyote kwa mapungufu yangu. Naamini kuwa ninapaswa kujirekebisha na si serikali inipendelee dhidi ya mwenzangu tuliotofautiana rangi!

Amandla......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…