. Kwenu nyie wakina Mkono, Tenga, IMMA ni bora mara kumi ya Issa Shivji kwa sababu tu ni wazawa!
FM,
Hapa ndipo unapotosha mjadala,hatujasema kuwa watanzania wenye asili ya uhindini wabaguliwe, kinachotakiwa ni kuwawezesha watanzania wazawa ili nao waweze kufanikiwa ingawa hawawezi kuwa wote, kama ilivyo sio watanzania waasia wote wenye hali nzuri.Lakini ni ukweli usiopingika kuwa watanzania weusi wengi ndio wana hali mbaya kiuchumi na kimaendeleo.Najua wapo weusi wachache wamefanikiwa sasa hiyo isiwe kigezo kuwa mbona mengi amefanikiwa na yeye atahitaji kuwa empowered.Hapa tunazungumzia kundi kubwa la watu walio nyuma sana kimaendeleo na kiuchumi.Na kwa kufanya hivyo haitakuwa na maana kuwa tunawabagua waliofanikiwa, lengo litakuwa kuwawezesha hawa wanyonge ili waweze kupiga hatua pasipo kuathiri hao waliofanikiwa.
Na labda nikukumbushe kuwa hao akina rakesh rajani, Prof. Issa shivji tayari wao ni watu waliofanikiwa wako kundi moja na akina mzee mengi na wengineo, kwahiyo hawahitaji kuwa empowered.
Suala la Mkono, IMMA, Tenga kuwa bora kuliko akina Shivji ni mawazo yako na mtazamo wako tu lakini hakuna mahali popote tumesema hivyo.
Na hata hivyo hao wote ni watu ambao wamefanikiwa iwe ni kwa njia ya haki au kwa haramu(kitunambacho hatukijadili hapa), maana najua wabongo wengi tuna bifu na utajiri wa mkono na ufisadi wa deep green ikihusishwa na IMMA.
Hivi fundi nikuulize swali, mbona hampigi kelele kupinga akina mama kupewa upendeleo kwa kupewa viti maalum vya ubunge na udiwani?mbona hampigi kelele kupinga akina mama kupewa upendeleo ili waweze kusomea kozi za uhandisi na sayansi vyuo vikuu baada ya kuonekana kuna uhaba wa wataalam wanawake kwenye nyanja hiyo???na ni kwa nini basi mgeuze suala muhimu la kuwawezesha wazawa maskini kuwa ni ubaguzi???mnataka waendelee kuwa maskini milele.Kama wewe umefanikiwa haina maana kuwa lazima na wengine wahangaike kama wewe ili wafanikiwe, watu wametofautiana uwezo, ndio sababu hata marehemu JKN alianzisha utaratibu wa kiweka viwango tofauti vya ufaulu kwenda shule za sekondari ili kuwainua wale walio kuwa nyuma kielimu, na ndipo na sie tuliokuwa tunachunga ng'ombe huko porini serengeti tukapata nafasi za kusoma hadi hivi leo tumeweza kujua kubofya kwenye key board na tukasomeka.