Uchaguzi 2020 Sera ya Majimbo ndio mkombozi wa Taifa

Uchaguzi 2020 Sera ya Majimbo ndio mkombozi wa Taifa

Umemaliza kila kitu boss
Salamu kwako Tundu Antiphas Lissu, Shalom,

Leo napenda kukwambia rasmi kuwa , Kura yangu iko kwako! Na hii ndo sababu yangu kuu ya kukupa kura!

Katika maisha yangu nimekuwa nikifanya utafiti sana juu ya dhana ya umasikini wa watanzania na Tanzania kwa ujumla, Moja ya sababu ambayo niligundua kwenye utafiti wangu ni kuwa Tanzania tuna mfumo mbovu sana wa utawala ambao vyovyote vile hatuwezi kuendelea kwa mfumo huu!

Mfumo huu ninaousema ni mfumo kuwa fedha zote za watanzania zinakusanywa na kuwekwa chini ya mtu mmoja( raisi ambayo yeye ndo anayeamua kuwa hizo fedha zigawanywe kivipi)

Madhara ya mfumo huu ni kuwa umeondoa uwajibikaji kwa wananchi na viongozi, umeondoa ubunifu kwa wananchi na viongozi na mwisho umepelekea tabia ya ombaomba na unafiki kwa wananchi na viongozi

Mfumo huu pia umechochea ufisadi wa kiwango kikubwa sana kwa wananchi na viongozi na kama Kuna mtu anabisha Leo hii aniambie maisha ya ukwasi wanayoishi maraisi wastaafu yametokana na nini???

Hapa Tanzania hakuna raisi mstaafu mwenye maisha ya utajiri wa kuwaida. Wengi wana utajiri mkubwa wa real estate, kilimo kikubwa na hata pia makampuni makubwa ya uzalishaji. Na kibaya ni kuwa vyote hivi huwa wanavipata wakiwa maraisi. Sababu ya haya yote ni kuwa tumekuwa na mfumo wa kuziweka fedha zote za nchi chini ya mtu mmoja.

Leo hii raisi ni kama Mungu hapa Tanzania. Kila aendapo watu ni kulia shida, awafanyie hiki na awaletee hiki, haya yote ni kwa sababu ya mfumo mbovu tulionao ambao umeondoa uwajibikaji na ubunifu kwa watanzania na viongozi wetu

Kwa nini Mfumo wa Majimbo ndo suluhisho wa haya yote?
1. Mfumo wa majimbo utafanya hela zote zinazokusanywa kwenye sehemu husika zitumike kwa matakwa ya wananchi wa sehemu husika mf. Kujenga barabara , hospitali, shule bora na huduma bora za Maji na umeme!! Hili litafanya wananchi wasiwe wajinga kwa viongozi wao na kamwe was iwe ombaomba na watu wa kujipendekeza kwa viongozi wao.

2. Mfumo wa majimbo utachochea ubunifu kwa wananchi kufanya shughuli mbalimbali bora za uzalishaji ili majimbo yao yakusanye fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo yao.

Kama jimbo husika linategemea kilimo basi wananchi wa hilo jimbo watafanya kilimo bora na watakifanya cha biashara ili wapate mapato mazuri ya kuendeleza jimbo lao kimiundombinu na Pia kimaendeleo. Hakuna sehemu watu watalala au kuwa wazembe na watakuwa wakali kwa viongozi wao kuwahamasisha wawe agressive kwenye kubuni miradi bora ya maendeleo kwa maendeleo yao.

Mfumo huu utatengeneza wananchi wanaojiamini na Kuwajibika kweli katika kutunza rasilimali zao ili ziwasaidie wao na uzao wao. Wananchi hawatakuwa wazembe na watawawajibisha kweli viongozi wasio wabunifu kwenye kutengeneza vyanzo vya mapato kwa sababu watakuwa wanajua bila vyanzo vya mapato bora na vya uhakika kwenye maeneo yao basi watakuwa nyuma kimaendeleo na hawataweza kunsurvive.

Mfumo wa majimbo utafanya kama sehemu Kuna mbuga za wanyama basi wananchi wa maeneo husika wazitunze rasilimali kweli kwa sababu watajua kweli bila mbuga hizo utalii utakufa na hawatapata mapato ya kulipa mishahara wafanyakazi wao, kujenga barabara na mitaa bora, kuhudumia Bima za afya na madawa hospitali. Kwa iyo Kama jimbo litategemea utalii basi watautunza na kuuthamini kweli utalii.

Kama jimbo linategemea viwanda au biashara basi jimbo hilo litatunga Sera bora ili kuhamasisha uwekezaji mkubwa wa viwanda na biashara kwa sababu wananchi wa sehemu husika watajua bila hivyo basi hawawezi pata mapato ya kununulia dawa, kupata Maji safi na salama na kujenga barabara nzuri!

Kama jimbo husika linategemea kilimo na migodi basi wananchi wa viongozi wa maeneo husika wataumiza kichwa kuweka Sera bora katika hayo maeneo ili kuhakikisha zinawapatia mapato makubwa ya kufanya miradi ya maendeleo. Watu watajiona kweli kuwa wao ni sehemu sahihi ya maendeleo husika.

Imefika wakati watanzania lazima tuseme kuwa mfumo wa utawala wa Chama cha mapinduzi, umechochea sana ufisadi, umasikini, kujipendekeza, uzembe, ubabaishaji na kutowajibika kweli kwa Watanzania!!!

Mfumo huu wa sasa umefanya watanzania tudharauliwe na viongozi na kuendeshwa Kama watoto wadogo kuwa tusipowachagua watu wao basi tusahau maendeleo kwa sababu wao ndo wanaamua hela zetu wazigawe vipi!! Hii sio sawa kabisa

Mfumo huu wa sasa umesababisha watu kuwa ombaomba na watumwa kwenye nchi yao kuwa kila wakimuona Raisi basi wamnyenyekee kama Mungu n kumuomba hiki na kile. Kama Raisi tunaomba Maji, barabara, umeme na shule bora

Kwa maendeleo ya kweli ni lazima Watanzania tuamue kwenye uchaguzi huu kumchagua Tundu Antiphas Lissu ili atubadirishie mfumo.

Hamasisha watu wengi zaidi kumchagua Lissu na Chadema kwa maendeleo ya kweli ya Tanzania na Watanzania!

Sambaza kwa watu wengi zaidi waelimike pia!!

Asanteni!
Lord denning.
 
Hujui
Mkuu, umeongea madini Sana,

Nchi yetu INA Baadhi tu ya mikoa michache sana iliyo na utajiri wa rasilimali

Ukisha igawa kimajimbo, tayari umebariki utajiri wa Gesi usivuke kwenda mikoa mingine ispokuwa kibiashara, madini Nayo vilevile, mbuga za wanyama nazo hivyohivyo ziwanufaishe wa hukohuko, vivyo hivyo mapato yatokanayo na bandari zetu, sasa jiulize, Mapato yatokanayo na bandari Kwa mjibu wa Rais wa Lwanda, yanatosha kuendeshea nchi yake na ya Tanzania, utajiri huo wote uwe Tu mikoa ya Pwani pekee

Madini kule Geita, Kwa mjibu wa takwimu za Mapato ya Serikali 2019 yamevunja rekodi ya Mapato yote ya utalii Kwa miaka yote

Utajiri huo uwe Geita pekee, hawaoni kwamba, nchi yetu itawalazimisha watu wengi kukuingiza kwenye magenge ya kiharifu wakitafuta kitu
 
Mku
Sana, Yaani Lisu mmoja ni sawa na CCM wote nchi nzima. We hushangai wote wanajibu hoja za Lisu tu ndo ujue amewazidi sana kwa akili
U hii sasa nidharau ambayo itafanya Lissu arose kura yangu kabisa. Futa kauli.
 
Sifuti bali nakazia, AKILI ALIZONAZO LISU NI SAWA NA UCHANGANYE AKILI ZA WANA CCM WOTE, BARA NA VISIWANI....Swali dogo tu kudhibitisha kauli yangu, Uliona wapi mtu anavunja katiba alafu wabunge wake wanamshangilia na kumwita majina yote....Kama hao wabunge akili zao ndo zipo hivyo, vipi mwanachama wa kawaida
Mku

U hii sasa nidharau ambayo itafanya Lissu arose kura yangu kabisa. Futa kauli.
 
Sifuti bali nakazia, AKILI ALIZONAZO LISU NI SAWA NA UCHANGANYE AKILI ZA WANA CCM WOTE, BARA NA VISIWANI....Swali dogo tu kudhibitisha kauli yangu, Uliona wapi mtu anavunja katiba alafu wabunge wake wanamshangilia na kumwita majina yote....Kama hao wabunge akili zao ndo zipo hivyo, vipi mwanachama wa kawaida
Ikulu upinzani utisikiatu. Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM na si hawa akina Lissu. Kama alivyi jaribu Lowasa. Wakipatikana kama 4 prominent figures wakatoka mazima CCM hapo inawezatoka mapema. Lakini si kwa sasa.
Kwa hiyo akili kubwa ipo CCM kama mlivyo mwamini Lowassa ndani ya siku 2 mkampa kugombea urais.
 
Ikulu upinzani utisikiatu. Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM na si hawa akina Lissu. Kama alivyi jaribu Lowasa. Wakipatikana kama 4 prominent figures wakatoka mazima CCM hapo inawezatoka mapema. Lakini si kwa sasa.
Kwa hiyo akili kubwa ipo CCM kama mlivyo mwamini Lowassa ndani ya siku 2 mkampa kugombea urais.
Sikukatalii, maana hata Malawi walikuwa wanaamini kama ww, mwisho wa siku hawakuamini macho yao
 
Mimi mkazi wa Songea Kitai, nilikuwa naumia sana kuona katika eneo letu ndipo yanapatikana makaa ya mawe yanayolisha karibu viwanda vyote nchini, na mengine yanasafirishwa kwenda Rwanda, Uganda, Burundi na Kenya na kuingizia nchi mamilioni ya pesa. Chakusikitisha barabara katika eneo letu ni Mungu tu ndo anajua, Yaani inafika kipindi cha mvua magari yanashindwa hata kupita kwenda kupakia makaa, barabara ni mbovu, eti suluhisho wameona matipa ndo yaende kupakia huko migodini yalete mjini ndo yapakiwe kwenye magari na kusafirishwa.

Kinachoniuma ni kuwa pamoja na mamilion tunayoingiza, pia sisi ni wakulima wakubwa, tuna lisha nchi na kuingizia mamilioni, isitoshe kuna uvuvi katika ziwa Nyasa vyote hivi vinaingiza mamilioni, lakini tunashindwa kujengewa barabara , Maji safi ya kunywa kwetu ni ndoto, hospital paka uende mjini, umeme tunauona tukienda mjini.

Naamini hii Sera ya majimbo kwamba kile kinachopatikana sehemu kilete maendeleo kwanza eneo lile husika ingekuwa imeanza siku nyingi basi wakazi wa Kitai tungekuwa kama calfonia,.

Kuna maeneo hapa Tanzania yatakuwa kama ulaya, ndio maana nchi kama Afrika kusini miji yake karibu yote imeendelea. Fikiri jimbo la Iringa lingekuwaje nafkiri kama Durban, Mtwara wana gesi, wana korosho, wana uvuvi wangekuwa kama Chicago. Moshi, Arusha, Mwanza, Mbeya sijui yatakuwaje.

Kwa kifupi hii Sera kwangu Mimi ndio Sera rahisi zaidi ya kuleta maendeleo kwa kurudisha mamlaka ya matumizi ya pesa kwa wananchi wa eneo husika. Wao ndo wanaamua tufanye nini na hii pesa yetu. Nafkiri hii ingekwepo chato wasinge amua kujenga uwanja wa ndege, Bali wangetumia zile pesa kwa jambo lenye manufaa zaidi ya uwanja. Pia wananchi wasingenunua ndege bali hiyo hela wangefanyia jambo lenye manufaa zaidi.

Pia Sera ya majimbo itapunguza mtu mmoja kuwa na maamuzi ya nchi nzima na kufanya aabudiwe kama mungu. Maana asingekuwepo mtu wa kusema msimchagua Fulani sileti maendeleo kwenu. Maana maendeleo yatakuwa yanaamuliwa na wananchi wenyewe na si kama ilivyo sasa amabapo pesa zote za nchi nzima zinakusanya sehemu moja alafu rais ndo anapanga afanye nini na hizo pesa. Matokeo yake ndo tunaon mtu anajiamulia tu sijui ajenge uwanja wa ndege, sijui anunue ndege, anaona pesa nyingi paka nyingine anaona bora agawe barabarani.

Pia hii Sera itapunguza ufisadi kwa kiasi kikubwa, maana wananchi watakuwa wanajua mapato na matumizi ya majimbo yao. Kama kuna ufisaidi mahali itakuwa rahisi kujulikana, tofauti na sasa ambapo CAG kasema kuna ufisadi wa Trillion 1.5 hazijulikani zilipo, ila serikali wanasema hakuna pesa iliyopotea na matokeo yake CAG akafukuzwa kazi kwa kusema ukweli. Pia tungekuwa tunajua kuwa tumenunua ndege kwa kiasi gani, tumejenga uwanja kwa kiasi gani tofauti na sasa ambapo gharama za ndege anajua mtu mmoja tu. Na gharama za uwanja anajua mtu mmoja tu Yaani yeye ndo mnunuzi, ndo dalali, ndo mtoa pesa, ndo mwandika mkataba, ndo msaini mkataba, ndo mwanasheria, ndo mhasibu, ndo daktari ndo kila kitu.

Faida za majimbo ni nyingi sana siwezi kuziandika zote, lakini nchi zote zenye mfumo wa majimbo karibu zote zimepiga hatua katika sekta ya maendeleo.

#LissuTumekuaminiTuvushe#
Umeeleza vizuri mngoni mwenzangu ila umeharibu kutaja hilo jina la Lissu
 
Sera ya majimbo ingetufanya tuendelee kwa kasi sana, kwa mfano Kule ruvuma rasilimali ni nyingi sana, Yale malori yanatoa makaa ya mawe Kule kitai na Nyasa yanalipa mapato mengi sana, yote yanapelekwa makao makuu hazina, huku barabara za mitaa kukwanguliwa mpaka rais aamue.sio sawa.
 
Ndo hicho kinachoniuma
Sera ya majimbo ingetufanya tuendelee kwa kasi sana, kwa mfano Kule ruvuma rasilimali ni nyingi sana, Yale malori yanatoa makaa ya mawe Kule kitai na Nyasa yanalipa mapato mengi sana, yote yanapelekwa makao makuu hazina, huku barabara za mitaa kukwanguliwa mpaka rais aamue.sio sawa.
 
Taja mikoa ya kanda ya kati nikutajie rasilimali na fursa walizo nazo.
Mkuu, hii Sera ni Nzuri Ukiwa katika Jimbo, ama mkoa wenye Resources nyingi na kutoshereza kujiletea maendeleo, swali langu ni kwamba, Kwa kuwa mikoa yenye utajiri wa lasirimali za kutosha huwenda zisifikie hata mikoa 8, hiyo mikoa mingine wataweza kuvumilia umaskini Wao uliopo ktk mikoa Yao ukiwemo mkoa wa Singida anakotokea Raisi wa mitandaoni?

Sera ya majimbo, ni Nzuri Sana mkiwa na eneo kuuubwa la nchi, nchi yetu ni ndogo na inaweza kulinganishwa na Jimbo moja tu la Taxes Maerekani, maana yake Ni kwamba, Jimbo la Taxes, utajiri ulio katika Baadhi ya maeneo yake, huufunika umaskini wa maeneo mengine yasiyokuwa na utajiri wa rasilimali

Je, hapa, mtaigawaje hii nchi ili kwamba, Kwa mikoa hiyo isiyozidi minane iingizwe kwenye hayo majimbo hata yasiyokuwa na kitu ili sasa kuumeza huo umaskini wa mikoa zaidi ya ishirini+

Hata ukasema uigawe kikanda, Naihofia kanda ya Kati, Kwa kuwa mikoa yake ni myeupe na inakuwaga na njaa sana
 
Wananchi wapi wameikataa?
Hawa wanaoitetea humu na wanaoishangalia katika mikutano ya Lissu sio wananchi?
Katika sera ambazo wananchi wamezikataa bayana, hii ni mojawapo, tena hii imehakikishwa hata na tume ya warioba. Kati ya failures za CHADEMA, ni hii policy.
Was never and will never be accepted in the near future. Not a campaigning issue at all, ingawa mwaka huu ni obvious wanashindwa.
 
Mkuu, hii Sera ni Nzuri Ukiwa katika Jimbo, ama mkoa wenye Resources nyingi na kutoshereza kujiletea maendeleo, swali langu ni kwamba, Kwa kuwa mikoa yenye utajiri wa lasirimali za kutosha huwenda zisifikie hata mikoa 8, hiyo mikoa mingine wataweza kuvumilia umaskini Wao uliopo ktk mikoa Yao ukiwemo mkoa wa Singida anakotokea Raisi wa mitandaoni?

Sera ya majimbo, ni Nzuri Sana mkiwa na eneo kuuubwa la nchi, nchi yetu ni ndogo na inaweza kulinganishwa na Jimbo moja tu la Taxes Maerekani, maana yake Ni kwamba, Jimbo la Taxes, utajiri ulio katika Baadhi ya maeneo yake, huufunika umaskini wa maeneo mengine yasiyokuwa na utajiri wa rasilimali

Je, hapa, mtaigawaje hii nchi ili kwamba, Kwa mikoa hiyo isiyozidi minane iingizwe kwenye hayo majimbo hata yasiyokuwa na kitu ili sasa kuumeza huo umaskini wa mikoa zaidi ya ishirini+

Hata ukasema uigawe kikanda, Naihofia kanda ya Kati, Kwa kuwa mikoa yake ni myeupe na inakuwaga na njaa sana
Ni kutokujua kwako ndiko kunakudanganya kuwa mikoa ya kati ni maskini.

Kwa kuwa hii serikali imetekeleza sekta ya kilimo ndio maana unafikiria hivyo. Kilimo cha kisasa kikianzishwa kwenye hiyo mikoa wakawa wana-export mafuta ya alizeti na karanga kila moja atataka akaishi Singida au Dodoma.

Kwa aina ya serikali tuliyonayo mikoa hiyo itazidi kuonekana hivyo hivyo kama unavyoiona sasa wakati kiukweli ni mikoa tajiri ni hakuna mfano.

Zamani wakati wazungu wahamiaji walipohamia Marekani kutoka Ulaya hakuna jimbo walilokuta likiwa kame kama California lkn baadaye ndilo limekuja kuwa kielelezo cha Marekani leo.

Kwa mkakati na mpango chanya hakuna mkoa maskini.
 
DRC na Nigeria ni waganga wa ukabila.
Kumbuka pia USA, Brazil, Australia, Ujerumani na Canada ni wanufaika wa mfumo wa majimbo
Hii Sera imekuwepo muda mrefu sana ndani ya chadema, wakongwe waligundua kuwa haitapokelewa positively na wananchi, hivyo ilikuwa haijitokezi kwa kuwa ingeathiri sana umaarufu na kukubalika kwa chadema. Bahati mbaya chama kimevamiwa na wanaharakati waropokaji wamemwaga kila kitu hazarani. Kifupi sera hii ni mufilisi kabisa na ndiyo itawaharakisha kifo cha chadema kilichotabiriwa, tayari kutoka jana baada ya mgombea wa ccm JPM kuwatahadhalisha watanzania dhidi ya ubaguzi unaoshadadiwa na chadema, watanzania wameachwa na mshituko mkubwa kwamba nchi inaweza kugawanywa vipande vipande kama chadema wataingia ikulu. Kwa heri chadema tulikupenda lakini uzembe wenu umewaponza. Mlionywa kwamba Lissu ni mwanaharakati asiye na staha.

Sisi tunawaomba ccm waendelee kuwaelimisha wananchi wakati huu wa kampeni madhara makubwa ya sera hii, nchi ya DRC na Nigeria ni wahanga wa structure hii ya majimbo. Kuna majimbo tajiri sana na kuna majimbo maskini sana. Kuna msemaji humu kasema, how will chadema be able to distribute evenly the little available resources across the country. Waje pia na FORMULA ya kutushawishi kwamba ugawanaji wa faida ya madini ya kule Geita na Gesi ya Lindi na mtwara faida zake zitawafikiaje watu wa iringa, singida na Dodoma just to mention chache.

TUPE KULE HAYA MACHADEMA, YAANI MNASIKITISHA WASOMI NYIE
 
Back
Top Bottom