Wananchi wawe HURU kuamua hatima yao kwenye majimbo yao ikisimamiwa na serekali kuu.
Ukiona mtu anabeza Sera ya majimbo, huyo ni MKOLONI MWEUSI. Maana mfumo huu tulio nao bado unamapungufu mengi sana kama vile ukabila na ukanda . Angalieni kwa sasa viongozi wote wa taasisi za umma ni wakutoka kanda ipi? Sio uchochezi bali ndo ukweli.
Mpaka tunaambiwa musiponichagulia mmbuge wa ccm siwaletei maji, nakwamba kila jimbo alipo mpinzani maendeleo ananyimwa kwa maksudi kisa ni waupinzani. Mfumo wa Majimbo hautakua na huo upuuzi na upendeleo wakijinga kama tunavoona sasa.
Majimbo yataleta ushindani wa maendeleo kwa kasi kubwa kuliko sasa. Angaliene maeneo ambayo yanapendelewa kimaendeleo kwa sasa ni Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha. Kwani Mbeya na miji mingine hawahitaji flyover, hawahitaji taa za barabarani? Yote haya yanashindika kwa sababu ya mfumo tulio nao. Nchi hii ni kubwa mno, majimbo yataleta urahisi wakiutawala.
Eti majimbo yataleta utawala wawazungu. Hoja yakipuuzi na kitoto kweli hii. Mbona hata sasa tunakimbiza ma bakuli kwa wazungu? Inamaana hawaoni hilo? Mbona ccm walisha tuuza kitambo kwa wazungu.
CCM ndo waliingia vimkataba vyaajabu vya madini, tuseme vya raslimali yetu yote. Wao ndo wametufikisha hapa. Leo magufuli anatekeleza kwa kiasi kilio cha wapinzani, wanajiona analeta ukombozi. Kiukweli ni kwamba kwavile sio jadi ya ccm kuleta maendeleo, ndo maana wanashindwa kupanga vipaumbele vya maendeleo, vizuri wanaishia kuumiza wanchi.
CCM inajua kua wamechelewesha maendeleo wenyewe, ndo maana utaona mtu anashangaa na kupiga makelele na ka flyover ka Mfugale na Ubungo interchange. Vitu vidogo vingefanyika miaka mingi ilio pita.
Hela ccm na serekali YAKE walikua nazo, ila wizi na kujilimbizia mali viongozi. Leo wanatuamisha ni malaika! Lol!
Majimbo yatafuta umwinyi wakujimilikisha nchi unao fanywa na Rais. Rais ndo kila kitu na ndo anakugawia hela na ndo anaamua kipi kifanyike na wapi? Ndo maana yeye anamua tuu kujenga uwanja wa ndege kwao, wakati watumishi nyongeza hamna, akakurupuka kununua ndege, akakurupuka kujenga Reli na Bwawa la Nyerere wakati wananchi wanaumia bila kuwashilikisha.
Majimbo yataleta fikra chanya na kufutilia mbali ule upuuzi wa NDIYOOOOO! BUNGENI unaofanywa na ccm, ule ukiritimba wa wabunge kuunga mkono kila jambo na kupitisha kila Matumizi, sheria, kanuni kwa Nia ovu pasipokujua kwamba watawala wa leo ni wapinzani wakesho, the same sheria zitakuja kuwaumiza hata wao wakiwa wapinzani.
Majimbo, yatakuja kuleta ufanisi zaidi kwa kila nyanja na anae ogopa mfumo wakiutawala wa majimbo, kama nilivyosema, ni mkoloni mweusi na Mnufaika mkubwa wa utawala wa ccm.
Tuwe wakweli, anaye tetea ccm muangalie kwa umakini wadhifa wake ndani ya serekali na chama. Utagundua ni mnufaika mkubwa wa ccm na uogozi wake.
Hata Kamuzu Banda wa Malawi, Moi wa Kenya, Mobuto wa Zaire, Bokasa wa Afika ya Kati, Peter Botha wa Afrika ya Kusini, Adolf Hitler wa Ujerumani, walikua na wapambe, hata Benito Mussolini wa Italy alikua na wapambe, hata Joseph Stalin wa USSR Siku hizi Russia alikua na wapambe. Kwahio watu waina hiyo hawakosekani, wote wanakua wanufaika wakubwa wa chama tawala.
Wote twajua utawala wa miaka 5 wa Magufuli umekua kandamizi kweli kweli. Lakini wengine hapa jamvini wanaongea na kutoa mada utafikiri alikua anaishi Nje ya nchi hajui kilichokua kina fanyika.
Hitimisho, mfumo wakiutawala wa majimbo ndo suluhu kuu na chachu ya ushindani wa maendeleo ndani ya nchi. Tusidanganyane huu mfumo wa sasa umefeli. Tulianza na mfumo wa ujamaa kwa miaka 25 ukafeli 1984, tukaanza mfumo wa sasa 1985 chini ya Mwinyi. Imepita miaka 35, umefika wakati tujaribu mfumo mwingine ili tuone tutapigaje hatua ya maendeleo haraka zaidi. Let us be dynamic!
Kama watu hatuwezi kuwa na mfumo usiokua na tija kiutawala tukaukumbatia daima. Ndiyo, wanao nufaika nao kama ilivokua kwa ujamaa, watakua wagumu kuuacha na kukumbatia mfumo mpya wa majimbo.
Mfumo wa majimbo ni mzuri sana na unawapa wananchi mamlaka yakuongoza na kuamua maendeleo ya jimbo lao na huleta wivu wa maendeleo kwa hali ya juu.
Tumeona kila mmoja kua mtumwa wakutaka kuja na kuishi Dar es Salaam na sasa Dodoma. Tunahitaji miji mingi na ustawi wa taifa kimaendeleo. Na mpinga Sera ya Majimbo halitakii meema taifa letu na ni mtu anaye jali tumbo lake tuu.
KILA MFUMO WAKIUTAWALA UNA FAIDA NA CHANGAMOTO ZAKE. ILA KWASASA MFUMO WA SASA WAKIUTAWALA UNAONEKANA KUA NA CHANGAMOTO ZAIDI KULIKO FAIDA TUKILINGANISHA NA UTAWALA WA MFUMO WA MAJIMBO.