frenk julius
JF-Expert Member
- Dec 24, 2019
- 377
- 242
Tambua tuko uchumi wa kati..mbavu kabsa...Kwahiyo wewe unataka tuendelee na huu utawala uliodumu karibia miaka 60 viongozi wakiwa wanachezea kodi na rasilimali za nchi kwa ufisadi kama vile hizo rasilimali hazina wenyewe.
Sera ya majimbo ndiyo jibu la ufumbuzi wa tatizo la umasikini wa nchi yetu, hivi inawezekanaje nchi yenye rasilimali nyingi kama Tanzania kuwa katika orodha ya nchi masikini sana duniani halafu tuendelee na hizo sera za kumuachia mtu mmoja maamuzi ya rasilimali zetu zote, kwanini yeye ni Mungu halafu halazimiki kufuata ushauri wa mtu yeyote.
Majimbo ndiyo njia pekee ya kutukomboa kiuchumi, tatizo watu kudhania mikoa ndiyo majimbo ati miko mingine haina rasilimali sa kutosha sasa kama mikoa siyo majimbo hiyo hoja inakuwaje na nafasi.
Hivi European Union mtu akitaka kwenda kufanya kazi nchi Jirani kuna uthibiti gani tena zile ni nchi tofauti lakini watu wako huru kufanya kazi popote, halafu mtu mjinga kama wewe unakuja na hoja za kijinga ati watu hawataruhusiwa kutoka jimbo moja kwenda lingine, pumbavu kabisa wewe jaribu kusoma sera na kuielewe siyo unaandika mihemko yako
Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app