Uchaguzi 2020 Sera ya majimbo sio ya CHADEMA, ilipendekezwa kwenye rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba

Uchaguzi 2020 Sera ya majimbo sio ya CHADEMA, ilipendekezwa kwenye rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba

Mzee Warioba bado ninamkubali sana , natamani mara nyingi ajitokeze asimamie na kutetea ukweli aliousimamia kiu ya Watanzania kupata Katiba wanayoihitaji.
Toka alivyopigwa na bashite, hawezi kufungua mdomo
 
RASIMU YA KATIBA na UANZISHWAJI wa CHADEMI kipi kilitangulia? Tokea kuanzishwa kwake CHADEMA wamekuwa wakitaka Serikali ya Majimbo
 
Can u put the quotation yenye kusema unavyosema au ni tafsiri yako
 
Sera hiyo ilikuwepo CHADEMA kabla ya mchakato wa katiba mpya.

Ila Kama kwenye rasimu y awariob ailitokea ni maoni tu ya wananchi yameendana na sera ya CHADEMA ya mda.

Swala ambalo naliona. Ni kwamba inanidhihirishia kwamba chadema ni Chama Cha demokrasia, kwa wananchi.
Kwani sera zao ziliendana na zimekua ziliendana na Yale ambayo wananchi kwa wingi wanayapendekeza, au kuyahitaji.

Naamini chadema hufanya uchunguzi ya nini iwe, au ziwe agenda zao kwenye Uchaguzi au kwenye kuunda sera.

. Tatizo ni CCM wanavyo ipotosha sera hii. Mfumo unaotumika Sasa ndio wa kikoloni kwani wakuu wa mikoa hawateuliwi na wanachi. Hata kama tunabaki na mikoa, tuondoe wakuu wa mikoa tubaki na mameya tu. Watatosha.
 
Mbali na kwenye Rasimu ya Warioba, sera hii pia aliinadi Mbowe wakati akigombea urais 2005 ilikuwepo kwenye ilani ya Chadema kipindi hicho.

All in all ni sera nzuri inayo rejesha mamlaka kwa wananchi kuchagua viongozi wanao wataka na kujiwekea utaratibu wa namna ya kuendesha serikali ya jimbo lao kulingana na fursa na rasilimali za eneo husika katika kujiletea maendeleo.

Ccm lazima waipinge kwa sababu itaondoa utawala unao wafavor kama vile MaDc, MaRc, wakurugenzi nk ambao huteuliwa na rais na ndio wanatumika kuibeba ibaki madarakani pamoja na kuwa imechokwa kila kona.
Na wanapinga kwa hoja dhaifu
 
Kumbuka 2010 mliitangaza hii sera ya majimbo, je rasimu ilikuwa imeshaanza kutafutwa?
Hiyo ni sera yenu tika zamani wakati mbowe anagombea 2005
 
CCM walitaka kutupotosha, asante kwa kuiweka hii hoja sawa!!
 
Mfumo wa majimbo ndio unaotakiwa kwa dunia ya sasa na ndio njia rahisi ya kuondoa udikteta.

Angalia sasa hivi jinsi ambavyo kabila moja walivyopewa uteuzi mwingi wa ma-dc na tena teuzi nyingi sana zinaenda kanda ya ziwa na hakuna wa kuguna.

Kwenye majimboism hakuna kabisa huu ujinga, viongozi wote wa juu katika jimbo wanachaguliwa na wananchi na kuwajibika moja kwa moja kwao.
 
Back
Top Bottom