Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,677
Nimefurahishwa sana na sera ya Chadema ya, uhuru, haki, na maendeleo. Ila binafsi ningependa kama ingeweza kusomeka, kuondoa udikteta, kuleta haki, na uhuru. Udikteta, kukosekana kwa haki na uhuru, ndo mambo yaliyokithiri kwenye utawala wa Magufuli kwa miaka mitano iliyopita.
Kwanini uhuru na haki? Kuna siri kubwa na uhusiano kati ya uhuru, haki, na maendeleo, na ndio haswa chimbuko la maendeleo ya nchi za ulaya na America.
Hivyo basi, ukiweza kuwa na uhuru na haki, ni lazima uwe na maendeleo. Mfano kwa sasahivi, kuna malalamiko mengi ya kukosekana haki kwa wafanyabiashara.
Hii imepelekea wengi kukosa uhuru wa kuwekeza na kuzalisha huduma na bidhaa. Unakuwa na uoga, kwamba ukifungua duka la tatu pale, TRA kesho wapo mlangoni kwako, matokeo yake mawazo ya kupanuka kibiashara yanadumaa na hivo hata rate ya maendeleo inakuwa inapungua.
Kukosekana huko kwa haki, uhuru na udikteta wa wazi, umekuwa ni mwiba mkali wa maendeleo ya nchi hii.
Ntazidi kuwasihi CHADEMA waendelee kushikilia na kuhubiri kuleta uhuru, haki na kutokomeza udikteta nyemelezi.
Kwa mahali nchi ilipofika, hivi vitu vyote CCM wanajisifu navyo vitakuwa si kitu kama kutakosekana uhuru, na itakuwa ni ngumu sana nchi kupata maendeleo halisi ambayo yatagusa maisha ya wananchi.