Serbia imezishika nchi za Magharibi pabaya

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Ikumbukwe kuwa mnamo mwaka 1999 nchi zilizo chini ya NATO wakiongozwa na Marekani ziliishambulia na kuiharibu vibaya sana nchi ya Serbia (wa iliyokuwa Yugoslavia ya zamani). Nchi za magharibi zilikuwa zinalitetea jimbo la KOSOVO lililokuwa linataka kujitenga na Serbia. Uvamizi huo ulifanikisha KOSOVO kujitenga na kutambuliwa na nchi za magharibi.

Sasa nchi za magharibi zinaitaka Serbia kuunga mkono vikwazo vya nchi za magharibi dhidi ya Urusi na zinaitaka pia Serbia ilaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Sasa Serbia imeziambia nchi za magharibi zianze kwanza kuiomba msamaha kwa kuwa ziliivamia nchi yake (kama urusi alivyoivamia ukraine), na pia zitangaze kutokuitambua KOSOVO ili kuonesha zinaheshimu mamlaka ya kitaifa ya Serbia. Kinyume na hapo zikome kutaka kuifanya serbia kama askari wake wa miguu dhidi ya vita vyao na Urusi!!

Every time American or other Western officials call on Belgrade to impose sanctions on Russia, Vulin says he asks them when they would do the same over the violation of Serbia’s territorial integrity.

If you want to stick to territorial integrity and sovereignty as the most important principle of international politics… start with Serbia.
 
Mkuu hii mada ina uchoyo wa ukweli, Nato ziliingia kijeshi pale Kosovo kwa sababu ya majeshi ya Serbia yalikuwa yanafanya mass murders kwa minority wenye Imani ya kiislaam,hawa walikuwa wanauliwa kisa Imani zao za kidini,mada za ukweli ni safi zaidi kuliko kuweka hizi mada zenye nusu uongo na kutumia lugha kama za mhariri wa gazeti la uhuru sio Safi.
 
Yakwako pia uliyathibitisha,au umesimamia propaganda za beberu America na washirika wake,kumbuka hata Iraq alinyongwa Sadaam Kwa propaganda ovu za beberu America Kwa kisingizio Cha silaha za mass destruction 🤔
 
Mkuu hii mada ina uchoyo wa ukweli, Nato ziliingia kijeshi pale Kosovo kwa sababu ya majeshi ya Serbia yalikuwa yanafanya mass murders kwa minority wenye Imani ya kiislaam,hawa walikuwa wanauliwa kisa Imani zao za kidini,mada za ukweli ni safi zaidi kuliko kuweka hizi mada zenye nusu uongo na kutumia lugha kama za mhariri wa gazeti la uhuru sio Safi.
Hizi ni sababu tu walizotumia mabeberu kuhalalisha uvamizi wao na wala hazina ukweli kwa kiasi wanachotaka tuamini. Kama walikuwa na mgogoro wa kidini basi ni mambo ya ndani ya nchi yaliyopaswa kusuluhishwa kwa njia ya amani na siyo kuingilia uhuru wa ndani! Unataka kuniambia mgogoro unaofukuta sasa Loliondo na ngorongoro unaweza kuwa sababu ya halali mataifa mengine kutushambulia ili kuwatetea wamasai? Hivi duniani hapa mgogoro wa kidini ulikuwa KOSOVO peke yake?
 
Mkuu hii mada ina uchoyo wa ukweli, Nato ziliingia kijeshi pale Kosovo kwa sababu ya majeshi ya Serbia yalikuwa yanafanya mass murders kwa minority wenye Imani ya kiislaam,hawa walikuwa wanauliwa kisa Imani zao za kidini,mada za ukweli ni safi zaidi kuliko kuweka hizi mada zenye nusu uongo na kutumia lugha kama za mhariri wa gazeti la uhuru sio Safi.
Ulitaka Marekani watumie sababu gani kuhalalisha uvamizi wao? Maana Iraki walisema kuna silaha za maangamizi, Libya walisema Ghaddafi gaidi anaua watu nk. Usiwaamini sana Wamarekani, waongo wakubwa!
 
Mkuu hii mada ina uchoyo wa ukweli, Nato ziliingia kijeshi pale Kosovo kwa sababu ya majeshi ya Serbia yalikuwa yanafanya mass murders kwa minority wenye Imani ya kiislaam,hawa walikuwa wanauliwa kisa Imani zao za kidini,mada za ukweli ni safi zaidi kuliko kuweka hizi mada zenye nusu uongo na kutumia lugha kama za mhariri wa gazeti la uhuru sio Safi.
Toka lini NATO wakawa na mahaba na waislam?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ikumbukwe kuwa mnamo mwaka 1999 nchi zilizo chini ya NATO wakiongozwa na Marekani ziliishambulia na kuiharibu vibaya sana nchi ya Serbia (wa iliyokuwa Yugoslavia ya zamani). Nchi za magharibi zilikuwa zinalitetea jimbo la KOSOVO lililokuwa linataka kujitenga na Serbia. Uvamizi huo ulifanikisha KOSOVO kujitenga na kutambuliwa na nchi za magharibi.

Sasa nchi za magharibi zinaitaka Serbia kuunga mkono vikwazo vya nchi za magharibi dhidi ya Urusi na zinaitaka pia Serbia ilaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Sasa Serbia imeziambia nchi za magharibi zianze kwanza kuiomba msamaha kwa kuwa ziliivamia nchi yake (kama urusi alivyoivamia ukraine), na pia zitangaze kutokuitambua KOSOVO ili kuonesha zinaheshimu mamlaka ya kitaifa ya Serbia. Kinyume na hapo zikome kutaka kuifanya serbia kama askari wake wa miguu dhidi ya vita vyao na Urusi!!

Every time American or other Western officials call on Belgrade to impose sanctions on Russia, Vulin says he asks them when they would do the same over the violation of Serbia’s territorial integrity.
WaSerbia hawa hawa waliofanya genocide dhidi ya waislamu wakiBoznia ? Hebu nenda kasome history ujue ubaya WA hawa watu
 
Mkuu hii mada ina uchoyo wa ukweli, Nato ziliingia kijeshi pale Kosovo kwa sababu ya majeshi ya Serbia yalikuwa yanafanya mass murders kwa minority wenye Imani ya kiislaam,hawa walikuwa wanauliwa kisa Imani zao za kidini,mada za ukweli ni safi zaidi kuliko kuweka hizi mada zenye nusu uongo na kutumia lugha kama za mhariri wa gazeti la uhuru sio Safi.
We jamaa bwana eti mauji ya alaiki, hivi kule Iraq walipata zile silaha?
 
WaSerbia hawa hawa waliofanya genocide dhidi ya waislamu wakiBoznia ? Hebu nenda Jason's history ujue ubaya WA hawa
Hivi kuna taifa lenye ubaya kuzidi Marekani duniani? Marekani ni taifa pekee lililowahi kutumia silaha za nyuklia dhidi ya taifa lingine (dhidi ya Japan), Marekani ilidanganya kuwa Sadam Hussein wa Iraq ana silaha za maangamizi, na wakatumoia kisingizio hicho kuishambulia Iraq na kuua makumi elfu ya raia wasio na hatia hadi Sadam Hussein akakamatwana kunyongwa!! Marekani hiyo hiyo iliishambulia Libya ya Gadafi na ikawadanganya na kuwarubuni walibya waasi dhidi ya kiongozi wao Gadafi ikiwadanganya kuwa Gadafi akiondoka watakuwa na maisha mazuri. Gadafi alikamatwa na kuuawa lakini LIbya ndo hiyo hadi leo haitawaliki na vita vya wenyewe kwa wenyewe bado vinaendelea!Hilo Taifa ovu kama Marekani leo haliwezi kujigeuza na kuwa mwalimu wa kufundisha na kusimamia haki za binadamu wakati yenyewe ni mharibifu na mvunjaji mkubwa wa haki za binadamu!! Serbia wako sahihi sana kuwatolea nje!!
 
Mkuu hii mada ina uchoyo wa ukweli, Nato ziliingia kijeshi pale Kosovo kwa sababu ya majeshi ya Serbia yalikuwa yanafanya mass murders kwa minority wenye Imani ya kiislaam,hawa walikuwa wanauliwa kisa Imani zao za kidini,mada za ukweli ni safi zaidi kuliko kuweka hizi mada zenye nusu uongo na kutumia lugha kama za mhariri wa gazeti la uhuru sio Safi.
Kwahiyo wewe Una waamini false flag USA !? Mpaka Leo hujui kuwa hao ni wapishi wazuri wa propaganda na wanapo taka kufanya mambo Yao kwaajili ya maslahi Yao Huwa Wana tumia dini kama Moja ya silaha zao Kwa kuwa brain wash watu , Nyie sindio mlikuwa mnasema Osama ana pigania dini ya mungu , kumbe ni CIA agent
 
WaSerbia hawa hawa waliofanya genocide dhidi ya waislamu wakiBoznia ? Hebu nenda kasome history ujue ubaya WA hawa watu
Kuna nchi inayo ongoza Kwa kufanya hayo kama USA na NATO!? Wameua watu wangapi na wengine wakiwa acha homeless huku wengine wakiwa vilema !?
 
Back
Top Bottom