Serena Williams amefunga ndoa na mwanzilishi mwenza wa Reddit Alexis Ohanian katika harusi kubwa iliojaa mbwembwe za aina yake ya mwaka huu.
Nyota akiwemo Beyonce, Kim Kardashian na Eva Longoria walikuwa katika harusi hiyo iliofanyika katika eneo la New Orleans siku ya Alhamisi.
Sherehe hiyo ilikuwa na wageni 200 katika orodha ya wageni kulingana na vyombo vya habari.
Eneo moja kubwa la mji lilifungwa kwa sherehe hiyo ambayo ilifanyika katika kituo cha Contemporary Arts Center.
Wageni wengine ni pamoja na nyota Caroline Wozniack, Kelly Rolland ,Ciara, La La Anthony na muhariri wa jarida la Vogue Anna Wintour kulingana na gazeti la daily mail.
Limeripoti kwamba harusi hiyo iligharimu dola milioni 1 huku wageni wakiagizwa kutoingia na simu zao kutokana na mkataba na jarida la Vogue.
View attachment 632724
Serena alijifungua mtoto wao wa kwanza wa kike Alexis Olympia, miezi miwli iliopita.