keydu
Senior Member
- Jan 3, 2017
- 124
- 190
-Tanzania Kwa sasa macho na masikio yote yapo Kwa Serengeti Boys Timu ya Vijana chini ya miaka 17 ambayo mwezi huu itashiriki michuano ya Africa chini ya miaka kumi na Saba (U17) itakayofanyika Gabon kuanzia may 14 Jumapili ya wiki Ijayo. Tanzania iliweka kambi Morroco na Jeshi la watu 30 na baadae ikaenda Cameroon kucheza mechi za kirafiki na Jumapili ya tarehe 7 wataenda Gaboni.
-Msafara wa watu 30 ni wachezaji 23 , bechi la ufundi 6 na Kiongozi wa TFF mmoja (1). Wachezaji 23 wa Serengeti Boys ni
MAKIPA (3)
-Ramadhan Awm Kabwili,
-Samwel Edward Brazio
-Kelvin Deo Kayego
MABEKI (7)
-Kibwana Ally Shomary
-Nickson Clement Kibabage
-Israel Patrick Mwenda
-Dickson Nickson Job
-Ally Hussen Msengi
-Issa Mudy Makamba
-Enrick Vitalis Nkosi.
VIUNGO (9)
-Ally Hamis Ng'anzi
-Mohamed Rashid Chombo
-Shabaan Zubery Ada
-Mathias Juan Juan
-Marco Gerald Gerald
-Nashon Kelvin Naftali
-Cyprian Cybenedicto Mtesigwa
-Assad Juma Ally
-Bakari Said Mussa
WASHAMBULIAJI (4)
-Muhsin Malima Makame
-Oscar Yohana Mkomola
-Ibrahim Abdallah Ali
-Abdul Hamis Suleiman
BECHI LA UFUNDI
-Bakari Shime (kocha mkuu)
-Oscar Mirambo (kocha msaidizi)
-Muharami Mohamed (kocha wa makipa)
-Kim Poulsen (Mashauri wa ufundi)
-Edward Evans (Mtunza Vifaa)
-Shecky Mngazija (Daktari wa timu)
KIONGOZI WA TFF
-Ayoub Nyenzi (M/kit wa Soka la Vijana)
SAFARI YA SERENGETI BOYS
-Timu hii ilianza kujengwa Tangu mwaka Juzi Golosoo Sports inakuletea mechi 20 za serengeti boys Tangu mwaka Jana Serengeti Boys imecheza mechi 20 zikiwa mechi za mashindano na mechi za kirafiki Katika mechi ishirini (20) mechi sita (6) zilikuwa za kufuzu kucheza michuano ya AFCON (U17), Michezo Mitano (5) ilikuwa ya michuano maalumu kule India ikijulikana Kama AIF Youth Cup na Mechi (9) ikiwa ni mechi za kirafiki . Katika mechi hizo 20 Serengeti boys imeshida mechi 13 imetoa sare mechi 5 na kufungwa mechi mbili 2 tu. Katika mechi 20 Serengeti boys imefanikiwa kufunga mabao arobaini na tatu (43) na imefungwa Mabao kumi na Sita (16)
-Zifuatazo ndio mechi 20 za Serengetiboys
MECHI ZA KIRAFIKI
1) Tanzania 2-1 Misri
-Mechi ya Serengetiboys dhidi ya Misri ilichezwa uwanja wa taifa na Serengetiboys ikashinda Kwa mabao mawili Kwa moja (2-1) mabao ya Tanzania yalifungwa na Cyprian Benedicto Mtesigwa na Ally Hussein Msengi
2)Tanzania 3-2 Misri
-Mechi ya marudiano ya kirafiki ilichezwa Tanzania Katika uwanja wa Azam Complex Pale Chamazi na Serengetiboys ikashinda tena kwa mabao matatu Kwa mawili (3-2) mabao ya Tanzania yalifungwa na Ibrahim Abdallah Ali mawili na Bocco Seleman.
MECHI ZA AIF YOUTH CUP (INDIA)
-Ilikuwa michuano maalumu iliyoandaliwa na shirikisho la Soka India ambao ndio wenyeji wa kombe la dunia mwaka ujao . Zilishiriki timu tano (India, Korea kusini, Malaysia, Marekani na Tanzania) kwenye kundi moja na Serengeti boys walishika nafasi ya tatu kwenye michuano hiyo.
Matokeo ya Serengeti boys India
3) USA 1-1 Tanzania
-mechi ya kwanza Tanzania walitoa sare ya bao moja kwa moja (1-1) bao Serengeti boys lilifungwa na kiungo Mohamed Rashid
4) India 1-3 Tanzania
-Mechi ya pili na wenyeji India Serengetiboys Wakashida Kwa mabao matatu Kwa moja mabao ya Serengeti boys yalifungwa na Maziku Amani, Nickson Clement Kibabage, Asad Juma Ally
5)Korea kusini 2-2 Tanzania
-Mechi ya tatu kwenye mashindano walipambana na Korea kusini na Serengetiboys Boys wakapata sare nyingine ya mabao mawili Kwa mawili (2-2) mabao ya Serengeti boys yakifungwa na kiungo Assad Juma Ally, na Mshambuliaji Maulid Lembe Ambaye hayupoo na timu Kwa sasa baada ya umri wake kuwa umezidi miaka 17.
6)Malaysia 2-2 Tanzania
-Mechi dhidi ya Malaysia ikiwa ndio mechi ya mwisho kwenye makundi Serengetiboys ikatoa sare ya mabao mawili Kwa mawili (2-2) kwa mabao ya kiungo Hatari Assad Juma Ally, na Mshambuliaji Yohana Oscar Mkomola.
Msimamo Ukawa hivi
Timu. P W D L F A GD Pts
1-U. S. A 4 2 2 0 7 2 5 8
2-Korea Kusini 4 1 3 0 5 2 3 6
3-Tanzania 4 1 3 0 8 6 2 6
4-Malaysia 4 0 2 2 5 9 -4 2
5-India. 4 0 2 2 3 9 -6 2
-Baada ya hapo aliyeshika nafasi ya kwanza akacheza na aliyeshika nafasi ya pili kutafuta bingwa wa mashindano, aliyeshika nafasi ya tatu akacheza na aliyeshika nafasi ya nne kutafuta mshindi wa tatu.
7)Tanzania 3-0 Malaysia
-Hii ilikuwa mechi ya kumtafuta mshindi wa tatu baada ya Tanzania kumaliza Katika nafasi ya tatu na Malaysia wakimaliza Katika nafasi nne naTanzania walishinda Kwa mabao matatu Kwa bila kwa mabao ya Mohamed Rashid, Shabaani Zubery Ada, Muhsin Malima Makame. Na kuwa washidi wa tatu wa mashindano hayo. Huku Korea kusini wakiwa mabingwa kwa kushinda mabao mawili Kwa moja.
MECHI ZA KUFUZU AFCON (U17)-2017
8)Tanzania 3-0 Shelisheli
-Mechi ya kwanza uliochezwa Dar na Tanzania ikashinda Kwa mabao matatu Kwa bila (3-0)
Wafungaji Serengetiboys
-Shaban Zubery Ada
-Ibrahim Abdalaah Ali
-Ally Hussen Msengi
9)Shelisheli 0-6 Tanzania
-Mechi ya marudiano kule kwao wakafungwa mabao sita Kwa bila (6-0) na kutolewa Kwa Jumla ya mabao tisa kwa bila (9-0)
Wafungaji Kwa Serengeti boys
-Assad Juma Ally
- Mohammed Abdallah
- Hassan Juma
- Issa Juma 2
-Yohana Oscar Mkomola
10)Afrika kusini 1-1 Tanzania
-Bao la Serengeti Boys lilifungwa na Yohana Oscar Mkomola mechi iliyochezwa Afrika kusini
11)Tanzania 2-0 Afika Kusini
mechi ya marudiano ilichezwa Tanzania uwanja Azam complex na Serengetiboys ikashinda Kwa mabao mawili Kwa bila (2-0) na kuitoa Afrika kusini Kwa Jumla ya mabao (3-1)
-Wafungaji Kwa upande wa Serengetiboys ni
-Mohamed Rashid
-Muhsin Malima Makame
12)Tanzania 3-2 Congo Brazzaville
-Mechi ilichezwa uwanja wa taifa Serengetiboys ikashinda Kwa mabao matatu Kwa mbili mabao ya Serengetiboys yalifungwa na Yohana Oscar Mkomola Alifunga mawili na nahodha Issa Abdi Makamba
13)Congo Brazzaville 1-0 Tanzania
-Mechi ya marudiano kule Congo Serengetiboys ilifungwa goli moja kwa bila na kuwa imetolewa Kwa bao la ugenini baada ya aggregate ya mabao matatu Kwa matatu (3-3)
-Congo Brazzaville waliondolewa na CAF baada ya kubainika kumchezesha mchezaji aliyezidi umri wa miaka kumi na Saba. na Tanzania kupewa nafasi hiyo.
MECHI ZA KIRAFIKI
14)Tanzania 3-0 Burundi
-Mechi hii ilichezwa Bukoba ikiwa ndio maandalizi ya AFCON baada ya Tanzania kupewa tiketi ya kushiriki michuano hiyo mabao ya Serengeti boys yalifungwa na Muhsin Malima Makame, Nickson Clement Kibabage, na Yohana Oscar Mkomola Kwa penati.
15)Tanzania 2-0 Burundi
-Baada ya kufugwa mabao matatu Kwa bila Burundi wakarudiana tena na Serengeti Boys wakala mbili bila mabao ya Serengeti boys yalifungwa na nahodha Issa Abdi Makamba, na Mshambuliaji Abdalaah Ibrahim Ali
16)Tanzania 2-2 Ghana
-Baada ya mechi na Burundi Vijana wakarejea Dar na kucheza na Ghana Katika uwanja wa taifa mchezo mgumu Kati ya mechi ngumu mpaka dakika ya tisini Serengetiboys walikuwa nyuma ya Mbao mawili Kwa bila ndani ya dakika kumi za nyongeza Serengetiboys wakapata mabao mawili ya kusawazisha kupitia Kwa kiungo Matata Assad Juma Ally, na Muhsin Malima Makame
17)Gabon 1-2 Tanzania
-Baada ya mechi dhidi ya Ghana Serengetiboys wakaenda Morroco kuweka kambi ya mwezi mmoja wenyeji wa michuano ya Africa mwaka huu Gabon wakawafuata kucheza mechi za kirafiki mechi ya kwanza wakala 2-1 Kwa goli la Nashon Kelvin Naftali, pamoja na lile la kujifunga baada ya kona iliyopigwa na Asad Juma Ally .
18)Gabon 1-2 Tanzania
-Wenyeji wa michuano hiyo Wakaomba mechi ya marudiano ya Serengeti boys wakala tena mbili moja (2-1) Kwa mabao ya Assad Juma Ally, na Abdul Hamis Suleiman
19)Cameroon 0-1 Tanzania
-Serengetiboys wakatua Cameroon kucheza mechi za kirafiki Cameroon pia ni mojawapo ya timu shiriki za mashindano ya AFCON (u17) 2017 Ingawa wako kundi tofauti na Tanzania mechi ya kwanza wakafungwa goli moja kwa bila (1-0) bao hilo likifungwa na kiungo ally Hamis Ng'anzi Dakika ya 36.
20)Cameroon 1-0 Tanzania
-Serengeti Boys wakarudia tena na Cameroon Hapa serengeti boys ikafungwa goli moja kwa bila na hii ikiwa ndio mechi ya mwisho ya kirafiki na Jumapili ya tarehe Saba watafika Gabon tayari Kwa mashindano
>Mabao 43 ya Serengeti boys yamefungwa na wachezaji kumi tisa (19) kwenye mechi 20 Kati ya wachezaji kumi na tisa (19) ni wachezaji sita (6) hawapo na timu Kwa sasa sababu ya umri, majeruhi na nk wachezaji hao ni Bocco Seleman goli moja, Mohamed Abdalaah magoli (2) Maziku Amani goli moja, mwingine ni Maulid Lembe goli moja, Hassan Juma goli moja pamoja na Issa Juma goli moja .
>Wachezaji Wanaongoza Kwa ufungaji kwa mechi 20 ni
1)-Yohana Oscar Mkomola -6
-Assad Juma Ally -6
2)-Muhsin Malima Makame -4
3)-Issa Abdi Makamba -3
-Mohamed Rashid -3
-Ibrahim Abdalaah Ali -3
4)-Ally Hussein Msengi -2
-Nickson Clement Kibabage -2
-Shabani Zubery Adda -2
-(Wengine wakiwa wamefunga goli moja moja)
RATIBA YA AFCON 2017
-Serengeti Boys wataanza May 15 dhidi ya Mali, mechi ya pili watacheza na Angola may 18 na mechi ya mwisho itakuwa May 21 dhidi ya Niger.
NB:check full time table Kwa picha
-Baada ya mechi za kwenye makundi timu mbili za juu zitafuzu kucheza nusu fainali pia zitakuwa zimekata tiketi ya kushiriki kombe la dunia India mwakani.