Serengeti boys future ya Tanzania

Serengeti boys future ya Tanzania

keydu

Senior Member
Joined
Jan 3, 2017
Posts
124
Reaction score
190
06a978a50ccc11b8cbafe4bda55c3633.jpg

-Tanzania Kwa sasa macho na masikio yote yapo Kwa Serengeti Boys Timu ya Vijana chini ya miaka 17 ambayo mwezi huu itashiriki michuano ya Africa chini ya miaka kumi na Saba (U17) itakayofanyika Gabon kuanzia may 14 Jumapili ya wiki Ijayo. Tanzania iliweka kambi Morroco na Jeshi la watu 30 na baadae ikaenda Cameroon kucheza mechi za kirafiki na Jumapili ya tarehe 7 wataenda Gaboni.

-Msafara wa watu 30 ni wachezaji 23 , bechi la ufundi 6 na Kiongozi wa TFF mmoja (1). Wachezaji 23 wa Serengeti Boys ni

MAKIPA (3)
-Ramadhan Awm Kabwili,
-Samwel Edward Brazio
-Kelvin Deo Kayego

MABEKI (7)
-Kibwana Ally Shomary
-Nickson Clement Kibabage
-Israel Patrick Mwenda
-Dickson Nickson Job
-Ally Hussen Msengi
-Issa Mudy Makamba
-Enrick Vitalis Nkosi.

VIUNGO (9)
-Ally Hamis Ng'anzi
-Mohamed Rashid Chombo
-Shabaan Zubery Ada
-Mathias Juan Juan
-Marco Gerald Gerald
-Nashon Kelvin Naftali
-Cyprian Cybenedicto Mtesigwa
-Assad Juma Ally
-Bakari Said Mussa

WASHAMBULIAJI (4)
-Muhsin Malima Makame
-Oscar Yohana Mkomola
-Ibrahim Abdallah Ali
-Abdul Hamis Suleiman

BECHI LA UFUNDI
-Bakari Shime (kocha mkuu)
-Oscar Mirambo (kocha msaidizi)
-Muharami Mohamed (kocha wa makipa)
-Kim Poulsen (Mashauri wa ufundi)
-Edward Evans (Mtunza Vifaa)
-Shecky Mngazija (Daktari wa timu)

KIONGOZI WA TFF
-Ayoub Nyenzi (M/kit wa Soka la Vijana)

SAFARI YA SERENGETI BOYS
-Timu hii ilianza kujengwa Tangu mwaka Juzi Golosoo Sports inakuletea mechi 20 za serengeti boys Tangu mwaka Jana Serengeti Boys imecheza mechi 20 zikiwa mechi za mashindano na mechi za kirafiki Katika mechi ishirini (20) mechi sita (6) zilikuwa za kufuzu kucheza michuano ya AFCON (U17), Michezo Mitano (5) ilikuwa ya michuano maalumu kule India ikijulikana Kama AIF Youth Cup na Mechi (9) ikiwa ni mechi za kirafiki . Katika mechi hizo 20 Serengeti boys imeshida mechi 13 imetoa sare mechi 5 na kufungwa mechi mbili 2 tu. Katika mechi 20 Serengeti boys imefanikiwa kufunga mabao arobaini na tatu (43) na imefungwa Mabao kumi na Sita (16)

-Zifuatazo ndio mechi 20 za Serengetiboys

MECHI ZA KIRAFIKI
1) Tanzania 2-1 Misri
-Mechi ya Serengetiboys dhidi ya Misri ilichezwa uwanja wa taifa na Serengetiboys ikashinda Kwa mabao mawili Kwa moja (2-1) mabao ya Tanzania yalifungwa na Cyprian Benedicto Mtesigwa na Ally Hussein Msengi

2)Tanzania 3-2 Misri
-Mechi ya marudiano ya kirafiki ilichezwa Tanzania Katika uwanja wa Azam Complex Pale Chamazi na Serengetiboys ikashinda tena kwa mabao matatu Kwa mawili (3-2) mabao ya Tanzania yalifungwa na Ibrahim Abdallah Ali mawili na Bocco Seleman.

MECHI ZA AIF YOUTH CUP (INDIA)
-Ilikuwa michuano maalumu iliyoandaliwa na shirikisho la Soka India ambao ndio wenyeji wa kombe la dunia mwaka ujao . Zilishiriki timu tano (India, Korea kusini, Malaysia, Marekani na Tanzania) kwenye kundi moja na Serengeti boys walishika nafasi ya tatu kwenye michuano hiyo.

Matokeo ya Serengeti boys India
3) USA 1-1 Tanzania
-mechi ya kwanza Tanzania walitoa sare ya bao moja kwa moja (1-1) bao Serengeti boys lilifungwa na kiungo Mohamed Rashid

4) India 1-3 Tanzania
-Mechi ya pili na wenyeji India Serengetiboys Wakashida Kwa mabao matatu Kwa moja mabao ya Serengeti boys yalifungwa na Maziku Amani, Nickson Clement Kibabage, Asad Juma Ally

5)Korea kusini 2-2 Tanzania
-Mechi ya tatu kwenye mashindano walipambana na Korea kusini na Serengetiboys Boys wakapata sare nyingine ya mabao mawili Kwa mawili (2-2) mabao ya Serengeti boys yakifungwa na kiungo Assad Juma Ally, na Mshambuliaji Maulid Lembe Ambaye hayupoo na timu Kwa sasa baada ya umri wake kuwa umezidi miaka 17.

6)Malaysia 2-2 Tanzania
-Mechi dhidi ya Malaysia ikiwa ndio mechi ya mwisho kwenye makundi Serengetiboys ikatoa sare ya mabao mawili Kwa mawili (2-2) kwa mabao ya kiungo Hatari Assad Juma Ally, na Mshambuliaji Yohana Oscar Mkomola.

Msimamo Ukawa hivi
Timu. P W D L F A GD Pts
1-U. S. A 4 2 2 0 7 2 5 8
2-Korea Kusini 4 1 3 0 5 2 3 6
3-Tanzania 4 1 3 0 8 6 2 6
4-Malaysia 4 0 2 2 5 9 -4 2
5-India. 4 0 2 2 3 9 -6 2

-Baada ya hapo aliyeshika nafasi ya kwanza akacheza na aliyeshika nafasi ya pili kutafuta bingwa wa mashindano, aliyeshika nafasi ya tatu akacheza na aliyeshika nafasi ya nne kutafuta mshindi wa tatu.

7)Tanzania 3-0 Malaysia
-Hii ilikuwa mechi ya kumtafuta mshindi wa tatu baada ya Tanzania kumaliza Katika nafasi ya tatu na Malaysia wakimaliza Katika nafasi nne naTanzania walishinda Kwa mabao matatu Kwa bila kwa mabao ya Mohamed Rashid, Shabaani Zubery Ada, Muhsin Malima Makame. Na kuwa washidi wa tatu wa mashindano hayo. Huku Korea kusini wakiwa mabingwa kwa kushinda mabao mawili Kwa moja.

MECHI ZA KUFUZU AFCON (U17)-2017

8)Tanzania 3-0 Shelisheli
-Mechi ya kwanza uliochezwa Dar na Tanzania ikashinda Kwa mabao matatu Kwa bila (3-0)
Wafungaji Serengetiboys
-Shaban Zubery Ada
-Ibrahim Abdalaah Ali
-Ally Hussen Msengi

9)Shelisheli 0-6 Tanzania
-Mechi ya marudiano kule kwao wakafungwa mabao sita Kwa bila (6-0) na kutolewa Kwa Jumla ya mabao tisa kwa bila (9-0)
Wafungaji Kwa Serengeti boys
-Assad Juma Ally
- Mohammed Abdallah
- Hassan Juma
- Issa Juma 2
-Yohana Oscar Mkomola

10)Afrika kusini 1-1 Tanzania
-Bao la Serengeti Boys lilifungwa na Yohana Oscar Mkomola mechi iliyochezwa Afrika kusini

11)Tanzania 2-0 Afika Kusini
mechi ya marudiano ilichezwa Tanzania uwanja Azam complex na Serengetiboys ikashinda Kwa mabao mawili Kwa bila (2-0) na kuitoa Afrika kusini Kwa Jumla ya mabao (3-1)
-Wafungaji Kwa upande wa Serengetiboys ni
-Mohamed Rashid
-Muhsin Malima Makame

12)Tanzania 3-2 Congo Brazzaville
-Mechi ilichezwa uwanja wa taifa Serengetiboys ikashinda Kwa mabao matatu Kwa mbili mabao ya Serengetiboys yalifungwa na Yohana Oscar Mkomola Alifunga mawili na nahodha Issa Abdi Makamba

13)Congo Brazzaville 1-0 Tanzania
-Mechi ya marudiano kule Congo Serengetiboys ilifungwa goli moja kwa bila na kuwa imetolewa Kwa bao la ugenini baada ya aggregate ya mabao matatu Kwa matatu (3-3)

-Congo Brazzaville waliondolewa na CAF baada ya kubainika kumchezesha mchezaji aliyezidi umri wa miaka kumi na Saba. na Tanzania kupewa nafasi hiyo.

MECHI ZA KIRAFIKI

14)Tanzania 3-0 Burundi
-Mechi hii ilichezwa Bukoba ikiwa ndio maandalizi ya AFCON baada ya Tanzania kupewa tiketi ya kushiriki michuano hiyo mabao ya Serengeti boys yalifungwa na Muhsin Malima Makame, Nickson Clement Kibabage, na Yohana Oscar Mkomola Kwa penati.

15)Tanzania 2-0 Burundi
-Baada ya kufugwa mabao matatu Kwa bila Burundi wakarudiana tena na Serengeti Boys wakala mbili bila mabao ya Serengeti boys yalifungwa na nahodha Issa Abdi Makamba, na Mshambuliaji Abdalaah Ibrahim Ali

16)Tanzania 2-2 Ghana
-Baada ya mechi na Burundi Vijana wakarejea Dar na kucheza na Ghana Katika uwanja wa taifa mchezo mgumu Kati ya mechi ngumu mpaka dakika ya tisini Serengetiboys walikuwa nyuma ya Mbao mawili Kwa bila ndani ya dakika kumi za nyongeza Serengetiboys wakapata mabao mawili ya kusawazisha kupitia Kwa kiungo Matata Assad Juma Ally, na Muhsin Malima Makame

17)Gabon 1-2 Tanzania
-Baada ya mechi dhidi ya Ghana Serengetiboys wakaenda Morroco kuweka kambi ya mwezi mmoja wenyeji wa michuano ya Africa mwaka huu Gabon wakawafuata kucheza mechi za kirafiki mechi ya kwanza wakala 2-1 Kwa goli la Nashon Kelvin Naftali, pamoja na lile la kujifunga baada ya kona iliyopigwa na Asad Juma Ally .

18)Gabon 1-2 Tanzania
-Wenyeji wa michuano hiyo Wakaomba mechi ya marudiano ya Serengeti boys wakala tena mbili moja (2-1) Kwa mabao ya Assad Juma Ally, na Abdul Hamis Suleiman

19)Cameroon 0-1 Tanzania
-Serengetiboys wakatua Cameroon kucheza mechi za kirafiki Cameroon pia ni mojawapo ya timu shiriki za mashindano ya AFCON (u17) 2017 Ingawa wako kundi tofauti na Tanzania mechi ya kwanza wakafungwa goli moja kwa bila (1-0) bao hilo likifungwa na kiungo ally Hamis Ng'anzi Dakika ya 36.

20)Cameroon 1-0 Tanzania
-Serengeti Boys wakarudia tena na Cameroon Hapa serengeti boys ikafungwa goli moja kwa bila na hii ikiwa ndio mechi ya mwisho ya kirafiki na Jumapili ya tarehe Saba watafika Gabon tayari Kwa mashindano

>Mabao 43 ya Serengeti boys yamefungwa na wachezaji kumi tisa (19) kwenye mechi 20 Kati ya wachezaji kumi na tisa (19) ni wachezaji sita (6) hawapo na timu Kwa sasa sababu ya umri, majeruhi na nk wachezaji hao ni Bocco Seleman goli moja, Mohamed Abdalaah magoli (2) Maziku Amani goli moja, mwingine ni Maulid Lembe goli moja, Hassan Juma goli moja pamoja na Issa Juma goli moja .

>Wachezaji Wanaongoza Kwa ufungaji kwa mechi 20 ni
1)-Yohana Oscar Mkomola -6
-Assad Juma Ally -6
2)-Muhsin Malima Makame -4
3)-Issa Abdi Makamba -3
-Mohamed Rashid -3
-Ibrahim Abdalaah Ali -3
4)-Ally Hussein Msengi -2
-Nickson Clement Kibabage -2
-Shabani Zubery Adda -2

-(Wengine wakiwa wamefunga goli moja moja)

RATIBA YA AFCON 2017
-Serengeti Boys wataanza May 15 dhidi ya Mali, mechi ya pili watacheza na Angola may 18 na mechi ya mwisho itakuwa May 21 dhidi ya Niger.
NB:check full time table Kwa picha

-Baada ya mechi za kwenye makundi timu mbili za juu zitafuzu kucheza nusu fainali pia zitakuwa zimekata tiketi ya kushiriki kombe la dunia India mwakani.
 
Mikakati ya muda mfupi.tunahitaji kuja na mifumo itakayowezesha vijana wadogo kujifunza na kielewa kitu kinaitwa organized football/tenniss/basketball n.k.ndo linalomsumbua hashim thabit
 
Naona future kwa vijana hawa...weka picha zao...ikiwezekana umri,uzito,urefu n.k
 
Mbona kombe letu tu hilo.
Kwa rekod hizi bado sioni timu ya kututisha hapo kwenye kundi letu.
Mungu bariki Tanzania.
 
Naona future kwa vijana hawa...weka picha zao...ikiwezekana umri,uzito,urefu n.k
Hivyo vitu kungekuwa na special thread kwa ajili ya serengeti boys ndio ingependeza ntalifanyia kazi na kuandaa kikosi kizima
 
Hivyo vitu kungekuwa na special thread kwa ajili ya serengeti boys ndio ingependeza ntalifanyia kazi na kuandaa kikosi kizima
yafaa kuwekwa...kiukweli watanzania wengi tunategemea bahati katika kila jambo na tunahisi mambo yanatokea tu...ukweli ni kuwa mambo yanaundwa....tuiunde serengeti boys kwa training,na hata kwa sifa pia.
 
Kuna link yoyote ya mazoezi au mechi zao?kama hamna kwa nini wadau wa IT wasitutengenezee??
 
Hakuna kitu hapo na wala hatuna Timu hivyo tusipoteze muda humu na kuanza ' kudanganyana '. Hii Timu huko Gabon haifiki popote mpaka Rais wa TFF Jamal Malinzi atakapoacha ' Unafiki ' wake. Mali watatufunga kisha Angola watafuata kutupa Kipigo na mwishoni kabisa Niger watatuchumbia Kaburi na hatutoki na hata point moja huko Gabon. Wenye kuujua vizuri mpira nadhani watakuwa wamenielewa sana. Timu haina competent Coach na Bakari Shime anafundisha kwa ' kubahatisha bahatisha ' tu ile Kiuwezo ni ' mtupu ' sana.

Hata hivyo nisiwakatisheni ' tamaa ' Watanzania wenzangu endeleeni tu kujipa moyo na matumaini ili siku tu ziende ila tusisahau tu kwamba FIFA Rankings za jana Uganda ni ya 72, Kenya ni ya 78, Rwanda ni ya 108 na Tanzania ni ya 138. Serengeti Boys haina chochote na tusihadaike na ushindi katika mechi zao za Kirafiki dhidi ya Gabon na Cameroon.
 
Kwahiyo mkuu hizi mechi wanazoshinda wanazinunua???
 
Wamefanya vizuri sana sana ila ushauri wangu, Wasipelekwe Bungeni kuchangiwa au kupongezwa, tutakua tumeroga, atakayeamini aamini
 
CC Moderators @mods.naombeni huu uzi muutengenezee uwe serengeti boys special thread ili wadau wa serengeti boys tupate kupeana update kwenye uzi mmoja
Ahsante
 
Kwahiyo mkuu hizi mechi wanazoshinda wanazinunua???

Waliocheza nao walikuwa ' hawakazi ' kama Wao ili kuhakikisha hawapati ' majeruhi ' wa ' kizembezembe ' ili waje ' kuumbuka ' pindi michuano ikianza. Ili uamini haya maneno yangu subiri wiki ijayo ' ngarambe ' hiyo ya Gabon ikianza ndipo utajua kuwa kuna Watu tumeanza kuichambua hii mipira zamani sana na tunaijua vile vile. Nawashangaa mno Watanzania jinsi ' mnavyojitumumua ' kwa kuwa na matuamini ya hii Timu Serengeti Boys. Yaani kabisa tuwafunge Mali kisha Angola na Niger? Kwa Timu yetu ipi? Na yenye maandalizi yapi? Ina Kocha wa aina gani? Hivi Bakari Shime ni Kocha kweli wa kuifanyia makubwa Tanzania huko Gabon?

Watanzania bhana!
 
Picha limeshaanza, tayari wamedroo na bingwa mtetezi. Leo wanacheza na Angola.

Mpaka hapo wamekuprove wrong!
 
Waliocheza nao walikuwa ' hawakazi ' kama Wao ili kuhakikisha hawapati ' majeruhi ' wa ' kizembezembe ' ili waje ' kuumbuka ' pindi michuano ikianza. Ili uamini haya maneno yangu subiri wiki ijayo ' ngarambe ' hiyo ya Gabon ikianza ndipo utajua kuwa kuna Watu tumeanza kuichambua hii mipira zamani sana na tunaijua vile vile. Nawashangaa mno Watanzania jinsi ' mnavyojitumumua ' kwa kuwa na matuamini ya hii Timu Serengeti Boys. Yaani kabisa tuwafunge Mali kisha Angola na Niger? Kwa Timu yetu ipi? Na yenye maandalizi yapi? Ina Kocha wa aina gani? Hivi Bakari Shime ni Kocha kweli wa kuifanyia makubwa Tanzania huko Gabon?

Watanzania bhana!
Tayari tuna point 4 kutoka kwa hao ulio wataja
 
Back
Top Bottom