Series (Special thread)

Mwaka huu nimeanza na burudani ya kutosha nimeshaangalia series na movies zifuatazo
Last kingdom
Squid game 2
Back in action
Dirty money
Night agent 2
Shogun
Vagabond
Presumed innocent
Power
Power book 2 ghost
 
Series ambazo zimewahi nikosha sana
1. White collar
Series hii namhusu Neal Caffrey (Matt Bomer), mwizi mwenye ujanja na mtaalamu wa kufanyiza vibandi, ambaye anashirikiana na Peter Burke (Tim DeKay), mpelelezi wa FBI aliyemkamata. Baada ya kukimbia gerezani kumtafuta mpenzi wake, Kate (Alexandra Daddario), Neal anapata mkataba wa kusaidia FBI kukamata wahalifu wenzake kwa kubadilishana uhuru wake . Ushirikiano wao hauna mwiko: Peter anajaribu kumfanya Neal kuwa mtu mzuri, huku Neal akitumia nafasi hiyo kufichua siri za kifo cha Kate na kufuata "sanduku la muziki" lenye hazina ya Vita vya Kidunia vya pili .

2. Person of interest
"Person of Interest" ni series inayomhusu mtaalamu wa kompyuta Harold Finch na mtu wa zamani wa kikosi maalum cha CIA John Reese wanaounda timu ya kufichua uhalifu. Wanaotumia utabiri wa kompyuta kwa mfumo aliounda finch kuzuia uhalifu kabla haijatokea. Wakati wanakabiliana na matatizo na maadui wa ndani, wanabaini mpango wa kisiri wa serikali, mashirika ya ujasusi, na makundi ya uovu wenye lengo la kuingilia faraghaza watu na kuathiri usalama wa taifa, na maswala ya kibinafsi wakati wanapigania haki na usalama wa umma.

3. Revolution
Series ya Revolution ni hadithi inayofuata maisha ya familia ya Matheson baada ya dunia kukumbwa na matatizo ya kimuundo ambayo inasababisha kutokuwepo kwa umeme. Baada ya miaka kumi na tano ya kukosekana kwa umeme, familia hiyo inagundua kwamba binti yao, Charlie Matheson, anamiliki kipande muhimu cha ufunguo wa kurejesha umeme duniani.
Kupitia safari yao ya kutafuta majibu na kupigana na serikali ya kimabavu inayotawala, familia ya Matheson inakabiliana na hatari kubwa na kukutana na watu mbalimbali wanaopigania uhuru. Wanakutana na mashujaa na maadui, na wanazingatia kufufua utaratibu wa kawaida duniani.

Chini ni series ambazo hazikuwa kunivutia kulingana na muendelezo wa maudhui kuwa mrefu sana kulinganisha na tamthilia nyingine zenye maudhui ya kufanana,mission kukamilika baada/.wisho wa series ingawa idea za movie ni nzuri lakini hazikunivutiq
1. Prison break
2. Money heist
 
Nashauri ziwekewe highlights kidogo ili atakae vutiwa nazo akaangalie ,jina pekee linaweza lisitoshe kumfanya mtu kupenda jina la series
 
Revolution waliicancel sijui kwanini
 
Hizo nimeziona zote kasoro hiyo White Collar.

Ila mzee umeidharau sana PB kwa kuiweka huko chini.
 
Hii Tyrant nayo ina season 2 za moto sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…