PreGE2025 Serikali acheni kumtumia Mwamposa kutafuta uhalali wa kudhibiti na kufungia mitandao ya kijamii

PreGE2025 Serikali acheni kumtumia Mwamposa kutafuta uhalali wa kudhibiti na kufungia mitandao ya kijamii

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Cute Wife

Platinum Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
3,054
Reaction score
8,449
Wakuu,

Sasa mnaanza kumtumia tapeli Mwamposa kutafuta namna ya kufungia mitandao ya kijamii! Eti watanzania waanze kutumia mitandao ILIYOPIMWA! Mnataka kupitisha agenda ya kuanza kuchunguza watu na kudhibiti mambo ambayo watu wanaona!

Eti watanzania waanze kutumia mitandao ya kijamii ambayo ni ya kiswahili, ya kizalendo😒😒, kwakuwa tunakaa kwenye chungu na tunajitosheleza kwa kila kitu?! Huwezi kuwa na akili ukaongea huu upumbavu.

Pia soma Pre GE2025 - Mwamposa ataka kuwe na TBS ya mitandao ya kijamii kuchuja maudhui, asema inafanya watu kuwa wavivu

Yaani watu wawili wanaotumia mitandao vibaya basi nchi nzima izuiwe kutumia mitandao ya kijamii! Halafu unaanzaje kupangia watu matumizi ya bando zao?

Soma Pia: Mwamposa awaasa baadhi ya Watanzania wabadili mtindo wa maisha na kuachana na uvivu unaowafanya kupoteza muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii

Hawa wavivu umeanza kuwaona sababu ya mitandao ya kijamii? Wakati Nyerere anapiga vita maadui watatu ikiwemo uvivu kulikuwa na mitandao ya kijamii? Embu tutoleni hizi takataka bana.

Dunia inakimbizana na maendeleo ya teknolojia sisi tunatumia nguvu kubwa kuididimiza na kila namna ya kuidhibiti, halafu mnakuja kushangaa kwanini wawekezaji wanakimbia nchini wakati kila leo mnakuja na upuuzi kama huu!

Acheni hizi propaganda za kipuuzi, haki ya kupata taarifa ni ya kikatiba, hiki mnachokifanya hakikubaliki.

 
Utashangaa, Kwa namna watu wanavyofanya biashara zao mitandao, kutafuta fursa za kielimu, kiuchumi kupitia mitandao .


Litatokea Bichwa la Waziri Mmoja, aamue kufungia mitandao ya kijamii
Si ndio, na wanatumia wapumbavu kama hawa na misikule yao kupitisha ajenda zao. Kwahiyo mtu akitengeneza trend yake ya ndoa feki basi hiyo inahalalisha kufungia mitandao ya kijamii?!
 
Back
Top Bottom