A
Anonymous
Guest
Serikali ya Tanzania haijawahi kuwa serious na kazi zake hata siku moja nimeshangaa sasa utaratibu uliopo hapa Kivukoni Ferry (Dar es Salaam) ukitaka kwenda kupanda Panton kuvuka kwenda Kigamboni.
Kwanza nikiri kuwa utaratibu uliowekwa kutumia kadi (N - Cards) ni hatua nzuri sana lakini hatua hii bila ufanisi hakuna la maana lolote, utaratibu kwa kadi hizi umewekwa kwa ajabu sana.
Mimi sio mvukaji wa mara kwa mara kwenda Kigamboni ile leo nimekuja kuvuka hapa na kukutana na hali ya ajabu, kwanza unatakiwa lazima uwe na kadi ndio uweze kuvuka vizuizi vya kuingia kusubiri Kivuko, ni hatua nzuri sana na ipo njema na napongeza.
Shida inakuja pale ambapo huna kadi na si mvukaji wa mara kwa mara utaratibu uliowekwa ni mbovu.
Kwanza upatikanaji wa kadi hizi ni shida ni majira ya Saa 10 jioni na tayari kadi zimeisha na Wahudumu wanakuambia hapo huwezi kupata tena hadi kesho. Swali nawauliza sasa navukaje?
Jibu lao ni la ajabu sana, wanakuambia mwombe mtu utumie kadi yake kisha umpatie TZS 200/-. Nawauliza kama nisipopata huyo wa kunisaidia hiyo kadi nafanyaje? Jibu lao ni jepesi sana wewe omba watakubali tu.
Wakati huo huo pembeni kuna mtu anauza kadi, mtu huyu ni nani? Ametoa wapi kadi hizi hadi na yeye anauza? Ni masuala ya kushangaza.
Serikali tukiamua kufanya jambo lenye tija basi tulifanye kweli sio kujaribu na kisha kutafuta mianya ya ubabaishaji.
Wezesheni watumishi wenu kuwa na kadi za kutosha na pia tafuteni utaratibu mzuri kwa watu ambao wao si wavukaji wa kila siku, wengine hutumia Panton mara moja kwa mwaka.