Serikali, CCM na Polisi wanapaswa kujiuliza kwa nini wananchi wakiona askari polisi anashambuliwa hawatoi msaada?

Police ndo majambazi na wanyang'anyi wakubwa.
Ukweli ni kwamba kuna police wameua ili kunyang'anya watu vitu walivyo navyo na kusingizia kwamba walikuwa majambazi. Kesi za namna hiyo dhidi ya polisi zipo.

Polisi wakikusimamisha wajue una fedha nyingi, eidha watakuambia mugawane, au watakuua na kusingizia ilikuwa mpambano wa kurushiana risasi na majambazi na wengine walikimbia. Watakuwekea bunduki eneo la tukio maana wanazo nyingi tu huko vituoni wanazunguka nazo ili kuwawekea watu waliowaua ushahidi wa uongo kwamba walikuwa majambazi waliuwawa wakirushiana risasi.

Angalia kwamba katika visa vyote vya polisi na "majambazi" kurushiana risasi, wanaokufa ni "majambazi" tu, hutakaa usike polisi kauwawa au kujeruhiwa, utafikiri kwamba wanaporushiana risasi na "majambazi" risasi za majambazi zinageuka kuwa maji!

Karibu 70% ya polisi watafanya "ujambazi" na hata kuua watu fursa inapojitokeza. Ni wachache sana walionyooka. Na wengi wa polisi walionyooka huuwawa kwa kuogopa watawachongea wenzao, na hili tatizo halipo polisi tu, kuna chombo kingine cha usalama kimetajwa kuuwa wenzao wanaohisi watatoa siri ya uharifu wa ndani na kuwachomea wenzao. Dunia hii ina watu waovu sana.
 
Juzi hapa kulikuwa na tukia la askari Polisi mkuu wa kituo cha polisi Mwanakwerekwe, Zanzibar, akishambuliwa hadharani, na wananchi wakishangilia japo waliona askari alikuwa amezidiwa (angalia picha hapa chini).

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharib, amewalalamikia wananchi kwamba walishuhudia tukio hilo lakini hawakutoa msaada wowote, na hata wengine walishangilia kuona mkuu wa polisi huyo akipewa kipigo.

Sasa hili ni jambo la kufikirisha sana. Si mara ya kwanza kunapotokea polisi kuuwawa au kushambuliwa wananchi wanashangilia au kutoa kauli za kejeli zinazoonyesha hawasikitishwi na kufa au kushambuliwa kwa polisi.

Tunajua si kitendo cha uungwana kushangilia kifo cha binadamu, lakini ni CCM na Polisi wenyewe wamesababisha hili. Wamejitakia wenyewe. Ni ujumbe tosha kabisa kwa serikali kwamba wananchi hawawaoni tena askari kama wapo kwa jukumu la kuwatumikia wananchi, bali kuwatumikia "mabwana" wao wa utawala wa CCM dhidi ya wananchi.

Polisi siku zote wamekuwa wakifanya kazi kwa kujipendekeza kwa utawala wa CCM, bila kufuata miongozo ya kazi zao. Polisi hawafanyi kazi tena kwa mujibu wa kanuni za polisi bali kwa maagizo toka juu, hata wakijua kwamba hayo maagizo toka juu yanakiuka haki za wananchi. Imefikia mahali wananchi wanaona kuwa askari polisi ni namna fulani ya utumwa kwa serikali ya CCM, kama kupewa "limbwata" hivi na chama tawala. Polisi wamepewa jina la PoliCCM.

Tumeshuhudia mara nyingi sana hata wanapoagizwa kuwakamata watu wa vyama vya upinzani, polisi wengine huomba msamaha kwamba wameamriwa toka juu na wanafanya hivyo si kwa utashi wao au kwa kuwa kuna sheria zimevunjwa. Kuna tetesi polisi hata wameambiwa watunge kesi za uongo dhidi ya watu, kuwabambikia kesi, na wanafanya hivyo bila kusita.

Tumefikia mahali watu mitaani wanasema mie nikikuta polisi anashambuliwa na mnyama au watu siwezi kabisa kumsaidia, kwa sababu polisi nao wamekuwa kama wanyama. Wengine wanasema siwezi hata siku moja kumpangisha polisi nyumba yangu. Wengine wanasema mwanangu akichumbiwa na polisi namkana. Haya ndio yaliyotokea Zanzibari. Wananchi wamefikia kutukana na kuwaita Polisi mbwa wa CCM. Kwa nini?

Sasa polisi ifikie mahali mjiulize, huu ndio uhusiano mnaotaka kujenga na wananchi, wa kuchukiwa kiasi cha wananchi kushangilia vifo vyenu? Mnafikiri ni nini kimewafikisha wananchi mahali hapo?

Endeleeni kujipendekeza kwa utawala wa CCM, na kadiri mnavyofanya hivyo mjue mnazidi kuharibu uhusiano wenu na wananchi. Mambo huwa yanabadilika. Kuna siku hao mnaojipendekeza kwao hawatakuwapo na mtabaki na aibu na fedheha kubwa. Na fedheha hii wenzenu wanaipata hata sasa hivi pale wanapostaafu na kurudi mitaani kwa wananchi. Wanaona aibu hata kujumuika na watu wa kawaida.
Kwa sababu polisi ni washirika wa CCM katika wizi wa kura
 
Hua nafurahia Sana nikishuhudia askari anachezea kichapo kikali namna hiyo hata akiuliwa sijali ni washenzi Sana hawa viumbe hawana utu hata kidogo hua wanaona kama wanamiliki Tanzania yote kwa kuvaa vile visale vyao, Piga mbwa hao washenzi kabisa wanyama wa porini
 
MKuu, askari ni askari akivaa uniform, akizivua ni binadamu wa kuhurumiwa sana
 
Kama hujawahi kupigwa matukio na hao wapumbavu ni rahisi kuwahurumia, lakini mimi Sijawahi na wala sitawahi kua na huruma na askari hata kwa bahati mbaya
 
Wezi, vibaka..majambaz, wauaji. Elimu ndogo. Interviews ni mbio na urefu unakula kazi
Basi ndio maana tuna matatizo mengi sana na polisi. Wanafurahia sana kuumiza watu, hilo ni tatizo kichwani. Mental cases
 
Juzi hapa kulikuwa na tukia la askari Polisi mkuu wa kituo cha polisi Mwanakwerekwe, Zanzibar, akishambuliwa hadharani, na wananchi wakishangilia japo waliona askari alikuwa amezidiwa (angalia picha hapa chini).

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharib, amewalalamikia wananchi kwamba walishuhudia tukio hilo lakini hawakutoa msaada wowote, na hata wengine walishangilia kuona mkuu wa polisi huyo akipewa kipigo.

Sasa hili ni jambo la kufikirisha sana. Si mara ya kwanza kunapotokea polisi kuuwawa au kushambuliwa wananchi wanashangilia au kutoa kauli za kejeli zinazoonyesha hawasikitishwi na kufa au kushambuliwa kwa polisi.

Tunajua si kitendo cha uungwana kushangilia kifo cha binadamu, lakini ni CCM na Polisi wenyewe wamesababisha hili. Wamejitakia wenyewe. Ni ujumbe tosha kabisa kwa serikali kwamba wananchi hawawaoni tena askari kama wapo kwa jukumu la kuwatumikia wananchi, bali kuwatumikia "mabwana" wao wa utawala wa CCM dhidi ya wananchi.

Polisi siku zote wamekuwa wakifanya kazi kwa kujipendekeza kwa utawala wa CCM, bila kufuata miongozo ya kazi zao. Polisi hawafanyi kazi tena kwa mujibu wa kanuni za polisi bali kwa maagizo toka juu, hata wakijua kwamba hayo maagizo toka juu yanakiuka haki za wananchi. Imefikia mahali wananchi wanaona kuwa askari polisi ni namna fulani ya utumwa kwa serikali ya CCM, kama kupewa "limbwata" hivi na chama tawala. Polisi wamepewa jina la PoliCCM.

Tumeshuhudia mara nyingi sana hata wanapoagizwa kuwakamata watu wa vyama vya upinzani, polisi wengine huomba msamaha kwamba wameamriwa toka juu na wanafanya hivyo si kwa utashi wao au kwa kuwa kuna sheria zimevunjwa. Kuna tetesi polisi hata wameambiwa watunge kesi za uongo dhidi ya watu, kuwabambikia kesi, na wanafanya hivyo bila kusita.

Tumefikia mahali watu mitaani wanasema mie nikikuta polisi anashambuliwa na mnyama au watu siwezi kabisa kumsaidia, kwa sababu polisi nao wamekuwa kama wanyama. Wengine wanasema siwezi hata siku moja kumpangisha polisi nyumba yangu. Wengine wanasema mwanangu akichumbiwa na polisi namkana. Haya ndio yaliyotokea Zanzibari. Wananchi wamefikia kutukana na kuwaita Polisi mbwa wa CCM. Kwa nini?

Sasa polisi ifikie mahali mjiulize, huu ndio uhusiano mnaotaka kujenga na wananchi, wa kuchukiwa kiasi cha wananchi kushangilia vifo vyenu? Mnafikiri ni nini kimewafikisha wananchi mahali hapo?

Endeleeni kujipendekeza kwa utawala wa CCM, na kadiri mnavyofanya hivyo mjue mnazidi kuharibu uhusiano wenu na wananchi. Mambo huwa yanabadilika. Kuna siku hao mnaojipendekeza kwao hawatakuwapo na mtabaki na aibu na fedheha kubwa. Na fedheha hii wenzenu wanaipata hata sasa hivi pale wanapostaafu na kurudi mitaani kwa wananchi. Wanaona aibu hata kujumuika na watu wa kawaida.
Wananchi wana wivu tu.
 
Wananchi wana wivu tu.
Wanawaonea wivu polisi, kwa kitu gani hasa? Nafasi yao ya kupokea rushwa, matumizi yao ya nguvu kupita kiasi, kusingizia na kumbakia watu kesi? Mie imefikia mahali naona kama watu ambao siku ya kiama hawana nafasi kabisa ya kupita ni pamoja na polisi (wengine ni TRA, wanasiasa, Tanesco, madereva wa bodaboda na daladala, TTCL internet, nk)
 
Polisi hana urafiki!... Polisi hana undugu!... Polisi hana ujamaa!...

Mimi iwe bahati mbaya, ama kwa makusudi....nikikuta polisi anapambana na Nyoka...... Mimi namsaidia nyoka!...maana najua nyoka Atakuwa anaonewa tu Bure!
 
Hizi ni thread nilizitoa siku nyingi sana watu wakaona natania!
 
Back
Top Bottom