Serikali, CCM na Polisi wanapaswa kujiuliza kwa nini wananchi wakiona askari polisi anashambuliwa hawatoi msaada?

Police ndo majambazi na wanyang'anyi wakubwa.
Ukweli ni kwamba kuna police wameua ili kunyang'anya watu vitu walivyo navyo na kusingizia kwamba walikuwa majambazi. Kesi za namna hiyo dhidi ya polisi zipo.

Polisi wakikusimamisha wajue una fedha nyingi, eidha watakuambia mugawane, au watakuua na kusingizia ilikuwa mpambano wa kurushiana risasi na majambazi na wengine walikimbia. Watakuwekea bunduki eneo la tukio maana wanazo nyingi tu huko vituoni wanazunguka nazo ili kuwawekea watu waliowaua ushahidi wa uongo kwamba walikuwa majambazi waliuwawa wakirushiana risasi.

Angalia kwamba katika visa vyote vya polisi na "majambazi" kurushiana risasi, wanaokufa ni "majambazi" tu, hutakaa usike polisi kauwawa au kujeruhiwa, utafikiri kwamba wanaporushiana risasi na "majambazi" risasi za majambazi zinageuka kuwa maji!

Karibu 70% ya polisi watafanya "ujambazi" na hata kuua watu fursa inapojitokeza. Ni wachache sana walionyooka. Na wengi wa polisi walionyooka huuwawa kwa kuogopa watawachongea wenzao, na hili tatizo halipo polisi tu, kuna chombo kingine cha usalama kimetajwa kuuwa wenzao wanaohisi watatoa siri ya uharifu wa ndani na kuwachomea wenzao. Dunia hii ina watu waovu sana.
 
Kwa sababu polisi ni washirika wa CCM katika wizi wa kura
 
Hua nafurahia Sana nikishuhudia askari anachezea kichapo kikali namna hiyo hata akiuliwa sijali ni washenzi Sana hawa viumbe hawana utu hata kidogo hua wanaona kama wanamiliki Tanzania yote kwa kuvaa vile visale vyao, Piga mbwa hao washenzi kabisa wanyama wa porini
 
MKuu, askari ni askari akivaa uniform, akizivua ni binadamu wa kuhurumiwa sana
 
MKuu, askari ni askari akivaa uniform, akizivua ni binadamu wa kuhurumiwa sana
Kama hujawahi kupigwa matukio na hao wapumbavu ni rahisi kuwahurumia, lakini mimi Sijawahi na wala sitawahi kua na huruma na askari hata kwa bahati mbaya
 
Wezi, vibaka..majambaz, wauaji. Elimu ndogo. Interviews ni mbio na urefu unakula kazi
Basi ndio maana tuna matatizo mengi sana na polisi. Wanafurahia sana kuumiza watu, hilo ni tatizo kichwani. Mental cases
 
Wananchi wana wivu tu.
 
Wananchi wana wivu tu.
Wanawaonea wivu polisi, kwa kitu gani hasa? Nafasi yao ya kupokea rushwa, matumizi yao ya nguvu kupita kiasi, kusingizia na kumbakia watu kesi? Mie imefikia mahali naona kama watu ambao siku ya kiama hawana nafasi kabisa ya kupita ni pamoja na polisi (wengine ni TRA, wanasiasa, Tanesco, madereva wa bodaboda na daladala, TTCL internet, nk)
 
Polisi hana urafiki!... Polisi hana undugu!... Polisi hana ujamaa!...

Mimi iwe bahati mbaya, ama kwa makusudi....nikikuta polisi anapambana na Nyoka...... Mimi namsaidia nyoka!...maana najua nyoka Atakuwa anaonewa tu Bure!
 
Hizi ni thread nilizitoa siku nyingi sana watu wakaona natania!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…