Mnyonge Mnyongeni Haki Yake Mpeni
Tunapoleta mada ni vema tulete mada ili wengi wajifunze kutatua changamoto zinazotukabili maishani mwetu na si kubeza upande mmoja wa muungano uonekani kama hauna maana, hii haijengi na haina maslahi kwa yeyote. Kusema kwamba ETI ushoga umezidi Zanzibar hivyo serikali ichukue hatua kali ni kichekecho!! Kwa hiyo Bara hakuna ushoga hivyo serikali isichukue hatua? Ila Zanzibar tu. Inawezekanaje kuna ukweli kwamba Zanzibar ushoga umezidi,je ina maana bara ushoga haujazidi? Siuji unatumia kigezo gani kusema kwamba Zanzibar ushoga umezidi!!?
Twende kwa takwimu - hebu chukua idadi ya watu Tanzania nzima ikiwemo Zanzibar, halafu chukua idadi ya watu Zanzibar pekee. Idadi ya watu Zanzibar nzima inakaribia idadi ya watu wa mkoa mmoja tu Tanzania bara.
Ukichukua idadi ya mashoga wote waliopo Tanzania Bara kwenye maeneo yanayo trend sana ushoga hasa miji mikubwa na maarufu kama Dar, Mwanza, Arusha, Morogoro, Tanga, Mara na Dodoma ukijumlisha idadi yao utakuta ni kubwa mara nyingi zaidi kuliko mashoga wote walipo Zanzibar.
Tunapozungumza ushoga Zanzibar kwa kweli tunazungumiza Unguja maana ndipo penye idadi kubwa ya watu kuliko mjini wowote Zanzibar kama nchi, ni kweli ushoga umeenea hasa maeneo ya mijini na kwenye viunga vya mahoteli yanayotembelewa zaidi na watalii. Lakini si sahihi kusema kwamba Zanzibar kuna mashoga wengi kuliko bara. Zanzibar wanaonekana wengi kwasababu ni padogo hivyo wanajikuta wanabanana hapo hapo. Unguja ni mji ndogo hivyo kila mtu anamjua mwenzake - ni rahisi kujuana. Lakini bara mashoga ni wengi zaidi ila wametapakaa kwenye eneo kubwa mno kuliko Unguja hivyo si rahisi kuwaona wengi kwa uwazi.
Wateja wakubwa wa ushoga kwa Zanzibar/Unguja ni watalii na raia wa kigeni wakaazi, wakati wateja wengi wa ushoga bara ni wenyeji/wabongo na wageni wachache - lakini kuna idadi kubwa ya wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja wenyeji kwa wenyeji kwa idadi kubwa bara kuliko Zanzibar. Soko la ushoga Unguja linategemea watalii na raia wa kigeni zaidi lakini kwa bara soko la ushoga litagemea wenyeji - Kwahiyo wapi hapo ushoga umezidi? Tafakari
Tatizo la ushoga haliwezi kutatuliwa na serikali kwasababu ni tatizo la kimaadili sio la kihalifu. Ushoga ni tatizo la kimaadili kama ilivyo umalaya, ulevi wa pome na madawa, uvutaji bangi, uzinzi, uchezaji kamari, uvivu wa kutopenda kufanya kazi na kukaa vijiweni na kucheza pool muda mwingi, nk, haya ni matatizo yanayozalishwa na jamii, hivyo msingi wa ufumbuzi wake lazima uanzie kwenye jamii kama ngazi ya familia, nafasi ya viongozi wa kidini, n,k. Haya ni matatizo ambayo yameshaota mizizi kwenye jamii na chanzo chake ni mmomonyoko wa maadili, hivyo suluhisho lake ni wewe, mimi, familia, viongozi wa dini, wananchi na jamii kwa jumka kujenga maadili na si kunyoosheana vidole.