DOKEZO Serikali, elezeni ukweli kuwa watoto chini ya miaka 5 wanalipia huduma, kama sivyo kituo cha afya Kimara wawajibishwe kwa kutoza pesa na huduma mbovu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hiki ni kituo binafsi, kituo cha Serikali hakiwezi kuwa na E-mail hiyo! Ila si unajua wabongo wanavyopenda kuilalamikia Serikali!
Ni kituo cha Serikali, ni moja ya mambo ya ovyo yaliyoko Serikalini
 
Hii ni kuondoa wafanyakazi wote hapo. Hawafai kuhamishiwa sehemu. Unawapa likizo bila malipo ya miezi 6 wakatafakari uhalali wa kuendelea na utumishi wao.
 
Mkuu, Hela serikali inatoka wapi?? Tamko lao ni ulaghai?
 
Hivi mnaonaga fahari kuwashitaki madaktari? Unataka upigwe x ray..kipimo cha mionzi bure? Poor you
Mkuu umeelewa hoja lakini?,shida sio kulipa bali shida ni sera za wizara ya afya kwa watoto chini.ya miaka 5
 
Bahati mbaya wananchi nao hawana akili
 
Kwani hizo hela ni za serikali ama ni zangu maana nalipa kodi kibao na matozo kibao harafu sheria inasema watoto wa chini ya miaka 5 watibiwe bure ww unaleta story
 
Hawana ufahamu kabisa, hawatambui wana haki na wajibu wa kuihoji Serikali pale ambapo inaahidi vitu ambavyo havitekelezwi.
CCM ndiyo maana wanatoa elimu mbovu sn, mtu ana degree lakini bado anaona maendeleo ni hisani ya Rais na siyo wajibu sembuse ambaye hajasoma hali ikoje?
 
Leo nilifika kituo cha afya Kimara baada ya ndugu yangu kuniita nikalipie gharama ili mtoto wake apatiwe matibabu baada ya kuanguka na kuumia mguu.
Je, ulipoona ''maza'' kavaa saa ya sh milioni 100 ulihoji? Kama hukufanya hivyo, basi tulia dawa ikuingie kwa sababu watanzania wengi tunajifanya eti ''mambo ya siasa'' hayatuhusu.
 
Mama wa hiyo wizara ataibuka kukanusha kama kawaida yake.

BTW:Binafsi natumia zaidi Hospital ya wilaya hapa na malipo ni cash tu kwa wote.

Ina maana tunapigwa?
 
Je, ulipoona ''maza'' kavaa saa ya sh milioni 100 ulihoji? Kama hukufanya hivyo, basi tulia dawa ikuingie kwa sababu watanzania wengi tunajifanya eti ''mambo ya siasa'' hayatuhusu.
Mambo ya siasa yananihusu na naifatilia, kuhusu kuhoji hicho ulichosema nadhani tukutane kwenye hoja husika inayohusika na saa hiyo na si hapa panapojadiliwa kuhusu wajibu wa Serikali kutekeleza sera zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…