DOKEZO Serikali, elezeni ukweli kuwa watoto chini ya miaka 5 wanalipia huduma, kama sivyo kituo cha afya Kimara wawajibishwe kwa kutoza pesa na huduma mbovu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mambo ya siasa yananihusu na naifatilia, kuhusu kuhoji hicho ulichosema nadhani tukutane kwenye hoja husika inayohusika na saa hiyo na si hapa panapojadiliwa kuhusu wajibu wa Serikali kutekeleza sera zake
Usione kuwa nimekupa challenge kwa sababu hoja yako haina maana.

Nimetaka tu ku-rise awareness ya jinsi kila mwananchi anavyotakiwa kuwa makini na kushiriki kwenye siasa za nchi. Tatizo lako limekuwepo kila siku na kila sehemu ya nchi, labda tu ulikuwa hujakutana nalo.

Ukweli ni kuwa siyo muda wa kuihoji serikali sasa, bali ni muda wa kufanya madadiliko. CCM haiwezi kubadilika tena hata ukihoji namna gani.

Tusipokubali hii fact basi tuendelee kuishi maisha ya kulalamika kila uchao.
 
Hakuna cha mtoto Wala mzee huduma za afya ni malipo hata mtoto akiwa na siku Moja.Ndiyo azabu ya kuminya demokrasia
 
Kipindi cha Magu,
Ummi alionekana kuwa msimamizi mzuri wa sera ya afya.
Ila sasa kusema ukweli wizara imemshinda. Sio kwenye matibabu tuu, hata NHIF nayo imemshinda.
Haiingii akini watoto chini ya miaka 18 wakate bima kwa mkusanyiko.
Je kama mtoto hayuko shule hastahili kuwa na bima? Kuna vitu vingine havihitaji elimu kutoa maamuzi. Ummi kachoka.
 
Dunia ya leo bado kuna mafala wanaamini kuwa wewe zaa kama sungura, halafu wanafikiri kuna wajinga huko duniani watalipa kodi kukutunzia wanao!
 
Tanzania inabidi tuwe na mentality ya kujitegemea. Hizi akili tegemezi za kijamaa zinaturudisha nyuma. Yaani mtoto wangu nimzae mwenyewe, niililie serikali kuhusu shule na matibabu. Kesho utaanza kusema Mwigulu Mchemba anapeleka watoto shule nzuri. Wasiojiweza ndio waisubiri serikali.

 
Usizae na kuacha jukumu lako kama mzazi,
Jukumu lako ni kuhakikisha anatibiwa na sio kusubiria serikali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…