Serikali fungeni barabara ya Kibiti, Lindi hadi Mtwara kwaajili ya usalama wa watu

Serikali fungeni barabara ya Kibiti, Lindi hadi Mtwara kwaajili ya usalama wa watu

mbona umewasilisha hoja kibabe hivo..Sote tunajua Barabara nyingi ni mbovu.
Barabara mbovu ni pamoja na niombe makambako ijapokuwa imepata makandarasi.kwa kweli bambu gama angekuwa hai hiyo barabara ingerekebkshwa haraka.nilichogundua kuwa viongozi wa zamani walikuwa wazalendo sana siyo hizi nyang'au zilizoko ck hizi.
 
Barabara mbovu ni pamoja na niombe makambako ijapokuwa imepata makandarasi.kwa kweli bambu gama angekuwa hai hiyo barabara ingerekebkshwa haraka.nilichogundua kuwa viongozi wa zamani walikuwa wazalendo sana siyo hizi nyang'au zilizoko ck hizi.
hiyo barabara nadhani inatengenezwa kuanzia Songea..Afadhali uhai umeonekana Pamoja na ile ya pale Kahama mjini..Sema waongeze kasi.
 
Kwani hiyo barabara si ya lami au imekuwaje.hiyo mikoa ya lindi na mtwara cjawahi kukanyaga.au hii ni barabara nyingine tofauti na hiyo aliyokuwa anapambana nayo Late Mkoa?
Barabara ni hiyohiyo ya sikuzote ilikuwa na Lami na sasa imekuwa ya vumbi kutoka KIBITI Hadi LINDI
 
Sisi watumiaji wa hii barabara ya kutoka DAR , KIBITI,LINDI HADI MTWARA tunaomba serikali hii kiziwi ufunge hii barabara sioni sababu ya kuendelea kutumika huku wananchi wanateseka na barabara mbovu kiasi hiki.

Laiti kama serikali ingekuwa inatujali watu wake ingefunga Tu ili turudi kule kwenye miaka ya 90,s kipindi ambacho tulikuwa tunatumia usafiri wa meli , safari yangu kutoka DAR Hadi MASASI sijakutana na gari ndogo kama hizi sedan zaidi ya land cruiser na crossover pekee.

Sijui serikali imejipangaje na mvua kubwa za El Nino zinazotabiriwa mwezi October! Na kama hizi mvua zitaanza kunyesha baadhi ya barabara zitajifunga zenyewe
Kwa aibu hii ya barabara za Tanzania ni ngumu Sana kupata mwekezaji kwenye sekta ya usafirishaji hasa Kwa nchi zinazotimia bandari zetu
Naunga mkono hoja
Watu wa kusini waruhusiwe usafiri wa asili yao...
 
Sikuamini kama kule kusini ndiko aliko toka marehemu mkapa, kasimu majaliwa, nape nauye, salma kikwete, na wengine walio wahi pata nafasi kubwa za kiuongozi hapa Tanzania!
 
Mkuu nilishakuomba kwasababu upo jikoni huko ongea na maza atandaze lami toka Sanya juu hadi kwenu longido.
Haha ila mkuu kila siku unabadilika tatizo lako ndio hilo.

Ni kweli kulikuwa na mradi wa barabara tokea Siha Mpaka Longido.

Yote hayo yatafanyika chini ya awamu ya sita ya Mama yetu , kaa mkao wa kuteleza tu toka siha mpaka longido.
 
Kiongozi Daaah bora umesema majuzi nilikua kiwanda cha TWYFORD pale MKIU hakufai kabisa. Changamoto hz watawala hawatatui kabisa. Tena ukizingatia kwao ni zenji.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Sisi watumiaji wa hii barabara ya kutoka Dar, Kibiti, Lindi hadi Mtwara tunaomba serikali hii kiziwi ufunge hii barabara sioni sababu ya kuendelea kutumika huku wananchi wanateseka na barabara mbovu kiasi hiki.

Laiti kama serikali ingekuwa inatujali watu wake ingefunga tu ili turudi kule kwenye miaka ya 90,s kipindi ambacho tulikuwa tunatumia usafiri wa meli, safari yangu kutoka DAR Hadi MASASI sijakutana na gari ndogo kama hizi sedan zaidi ya land cruiser na crossover pekee.

Sijui serikali imejipangaje na mvua kubwa za El Nino zinazotabiriwa mwezi October! Na kama hizi mvua zitaanza kunyesha baadhi ya barabara zitajifunga zenyewe.

Kwa aibu hii ya barabara za Tanzania ni ngumu sana kupata mwekezaji kwenye sekta ya usafirishaji hasa Kwa nchi zinazotimia bandari zetu.

..fedha wanazotumia kujenga viwanja vya Afcon zingeweza kufanya makubwa kwa ajili ya barabara ya kusini.
 
Back
Top Bottom