Serikali fungeni shule na vyuo kuokoa maisha

Serikali fungeni shule na vyuo kuokoa maisha

Ntate Mogolo

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2016
Posts
410
Reaction score
705
Tunazidi kupoteza nguvu kazi ya taifa! Hii siyo habari njema hata kidogo! Wizara ya afya, funga shule na vyuo. Watoto na vijana wanapata sana covid lakini, haina madhara makubwa kwao!

Covid haina madhara makubwa kwa vijana na watoto, wanaugua na kupona tena bila dawa za maana. Tatizo ni kuwa, wanaambukizana na kuileta majumbani na kuwaambukiza wazazi na watu wenye umri mkubwa nyumbani.

Hii ndo balaa! Kama tutaweza kudhibi maambukizi kwa watoto na vijana, tutakuwa tumefanikiwa sana kuokoa maisha ya watu wazima wanaojikinga katika familia. Shule na vyuo wafunge mwezi mmoja tu, maambukizi yatapungua.
 
Kufikiri kufunga shule na vyuo kwa ugonjwa ambao hujui hatima yake ni ufinyu wa kufikiri. Wewe una kazi nzuri na una uhakika na kesho yako jua kwamba hizo ni ajira za watu!

Kuna watu wanalisha familia zao kwa hizo ajira, toka corona ilivyoanza mwaka 2019 decemba duniani kote, mpaka leo nchi zilizofunga shule na vyuo Hawajui nini hatima yake, kwa hiyo wewe endelea kujikinga kivyako sio kuhamasisha wenzako wapoteze ajira.
 
Kwa jinsi muda ulivyoenda, naona ni vizuri kwa walio umri wa miaka 60 na kuendelea na walio na changamoto za kiafya kuvaa barakoa na kujitenga kadri iwezekanavyo.

Wawaache wenye afya nzuri, vijana na watoto waendelee na shughuli za kila siku kwa kunawa mikono mara kwa mara na kuvaa barakoa.
 
Unazungumzia wizara ya afya ipi hiyo? Tanzania imejaa wapumbavu ndiyo maana Taifa limefika hapa lilipo sasa hivi,ina maana huna habari kuwa Tanzania inaongozwa na mtu mmoja? Yaani unahitaji kuwa na PhD kujua kuwa wizara zote Tanzania zinaongozwa na mtu mmoja?
 
Kama tutaweza kudhibi maambukizi kwa watoto na vijana, tutakuwa tumefanikiwa sana kuokoa maisha ya watu wazima wanaojikinga katika familia. SHULE NA VYUO WAFUNGE MWEZI MMOJA TU, MAAMBUKIZI YATAPUNGUA
1. Waanze kutangaza cases daily na wapi zimepatikana. Wataalamu wa kupambana na magonjwa ya milipuko wapewe confidence na uhuru wa kufanya kazi zao bila kusubiri ruhusa kutoka kwa wanasiasa

2. Weka bylaws kila mtu avae barakoa kwenye public. Mkaidi akamatwe na kulipa faini

3. Wageni kutoka nje wote waje na negative certificate za COVID with immediate effect. Ambae hana arudishwe na ndege aliyokuja nayo

4. Wafanyakazi waanze kuingia ofisini kwa shift na wengine wafanyie home ili kupunguza mikusanyiko. Hakuna haja ya kujazana ofisini

5. Public transport zianze kubeba watu nusu ya uwezo wake

6. Funga clubs kwa mwezi mmoja

Kuna mengi ya kufanya ila kiburi cha Magufuli ni tatizo. Sasa katwaliwa Eng. Kijazi. Who next?
 
Kufunga shule haitasaidia kitu, maana bado mishe mishe za maisha zitabaki vile vile. Napendekeza, barakoa kila mahali, kusiwe na mikusanyiko yoyote, daladala hakuna kusimamisha abiria, watu wapeane distance wanapopata huduma kama za kibenki.
 
Kufikiri kufunga shule na vyuo kwa ugonjwa ambao hujui hatima yake ni ufinyu wa kufikiri!!! Ww una kazi nzuri na una uhakika na kesho yako jua kwamba hizo ni ajira za watu! Kuna watu wanalisha familia zao kwa hizo ajira, toka corona ilivyoanza mwaka 2019 decemba duniani kote, mpaka Leo nchi zilizofunga shule na vyuo Hawajui nini hatima yake, kwa hiyo ww endelea kujikinga kivyako sio kuhamasisha wenzako wapoteze ajira
Kwa hiyo ajira ni muhimu kuliko uhai?
 
Vijana ndio wanaua wazee na wenye changamoto za kiafya kwa kuwaambukiza....It makes sense ,wafunge shule kwanza kwa muda ila Shule kwa sasa ada haiendi bure itafidiwa kwenye term zingine.
Hahahaha mkifungua mnalipa upyaaaaaaa 😂😂😂 !

Wazazi lipeni pesa bana vipi aisee 😂
 
Back
Top Bottom