Serikali futeni utaratibu wa kudai maiti Hospitali za Serikali

Serikali futeni utaratibu wa kudai maiti Hospitali za Serikali

Prepaid wapi bana,

Pesa ya matibabu iwe mtihani kupatikana, pesa ya kulipia maiti itoke wapi?

Si sawa kudai maiti.
Maiti huwa haidaiwi...

Kinachodaiwa ni huduma alizokuwa amepatiwa kabla hajafariki...

Sasa akifariki wabongo hatutaki kuchangia ili na mwingine akija apate huduma...

Bila kuchangia hizi huduma si hospitali zitacollapse?...
 
Kama maiti haidaiwi, kwanini Huwa inazuiwa kutolewa kwenda kuzikwa Ili Hospitali ibaki inawadai ndugu?

Waislamu akifa mtu, maiti Inatakiwa izikwe siku hiyo hiyo,

Lakini Hospitali haijui Hilo,

Inashikilia mwili Hadi ndugu walipe pesa ya mwisho!!
 
Leo Imeripotiwa Tanga, mjamzito amefariki Kwa kukosa 150,000 gharama ya kujifungua, kama ilivyoripotiwa na ndugu mwana JFBARD AI kupitia Milard ayo.

Cha kushangaza Bado mwili/ maiti itazuiwa hospitali Hadi ndugu walipe pesa zote za kutunza maiti.

Haikubaliki hii.
 
Wabongo wanataka kila kitu kiwe bure,
Elimu bure
Afya bure
Maji bure
Umeme Bure 🤣🤣

Kikubwa kama jamii tuhimizane kukata bima ya Afya
Shida iko wapi ikiwa vyote hivyo vitatolewa bure? Nchi imeejaliwa kila aina ya raslimali, wezesha huduma za kijamii ili jamii ifurahie uwepo wa raslimali kwenye nchi yao.
Kama hamuliwezi hilo ondokeni madarakani wenzenu walifanyie kazi
 
Haiwezekani ndugu wauguze mgonjwa, inatokea bahati mbaya, mgonjwa anaaga Dunia halafu Hospitali ya Serikali igome kutoa mwili kwa maziko hadi ndugu watoe pesa zote.
Hebu fikiria kama mkurugenzi wa hiyo hospitali.

Je? Utakataza watu wasihudumiwe hadi wawe wamelipia? Maana hicho ndio kitazuia maiti kudaiwa (ikitokea amekufa)

Msipende kupokea huduma bila kulipia. Huo nao ni wizi. Ufisadi wa mali za umma kibinafsi
 
Shida iko wapi ikiwa vyote hivyo vitatolewa bure? Nchi imeejaliwa kila aina ya raslimali, wezesha huduma za kijamii ili jamii ifurahie uwepo wa raslimali kwenye nchi yao.
Kama hamuliwezi hilo ondokeni madarakani wenzenu walifanyie kazi
Ushauri mzuri.

CAG anaripoti ubadhirifu mkubwa Kila mwaka,

Kodi zetu zitumikke vizuri kusaidia maskini.
 
Sina HAKIKA kama mabenki yana Utaratibu ya kudai maiti ikitokea mdaiwa amefariki na alikuwa anadaiwa.

Serikali iache TABIA hii ya kudai maiti Ibebe Mzigo huo.
Nadhani ni kwa kuwa mabenki yana bima za mikopo. Hivyo watasolvu juu kwa juu.

Hata hospitali mtu akiwa na bima watamuachia watasolvu juu kwa juu.

Suala tu ni malipo yanafanyika, analipia nani hatujui. Lakini msiangushie mzigo hospitali husika mjue na wao wanakaguliwa mahesabu.
 
Back
Top Bottom