Monica Mgeni
Member
- Oct 7, 2021
- 82
- 134
TUTAPOTEZA TUKISUBIRI VICHWA VIPYA VYA TRENI 2023.
Tarehe 04/07/2022 Ikulu Jijini Dar Es Salaam wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) sehemu ya Tabora hadi Isaka, Km 165 njia Kuu na Km 35 njia za kupishana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alieleza nia ya Serikali yake ya kuimarisha Usafiri wa Reli Nchini.
Moja ya kauli iliyotolewa na Mhe. Rais ni kwamba Serikali itanunua Vichwa vya Treni vilivyotumika lakini vikiwa katika hali nzuri ili vianze kutumika wakati tunasubiri Vichwa vipya vilivyoagizwa na Serikali ambavyo vinatarajiwa kuwasili Nchini mwaka 2023.
Ifahamike kuwa, Vichwa vya Treni vya awali vinavyotarajiwa kununuliwa na Serikali vitahifadhiwa na kutumika kama mbadala (Backup) pindi Vichwa vipya vitakapopata hitilafu. Suala hili litasaidia kuendelea kutolewa kwa Huduma za Usafirishaji kama kawaida.
Pili, Gharama za ununuzi wa Vichwa vipya vya Treni ya Mwendokasi ni sawa na kununua Mashangingi 10 mapya na gharama zake zinakadiriwa kufikia Tshs. Bilioni 4 kwa kichwa kimoja.
Tatu, Kihistoria kutokana na gharama kubwa ya ununuzi wa vipuri vipya vya Treni, Tanzania haijawahi kununua Vichwa vipya wala Injini mpya ya Treni tangu enzi za Mkoloni. Ambapo mwaka 1990 Shirika ya Reli ilinunua Injini (Used) namba 826 kutoka Sweden.
Uchumi wa Mataifa yanayoendelea umekuwa kikwazo kwa Nchi zetu kufanya manunuzi ya Vichwa vyote vipya kama ilivyofanyika kwa jirani zetu wa Kenya.
Vilevile, Uamuzi huu wa Serikali wa kuanza kutumia Treni iliyotumika yenye hali nzuri ni mzuri kutokana na ushindani wa Kibiashara uliopo katika Nchi za Afrika Mashariki ambapo kusubiri Treni Mpya ni kupoteza mapato katika kipindi ambacho reli tayari imekamilika kwa ajili ya matumizi.
Tumuunge mkono Rais wetu mwenye maono chanya ya kuinua Uchumi wa Taifa letu