Serikali haimuoni Chief Godlove ?

📌UKITAKA UTAJIRI TAFUTA JAMBO LAKO AMBALO UTAKUSANYA MASKINI WENGI UWAKAMU🤝

ACHA UJINGA UTAJIRI UPO KWA MASKINI.WEWE ENDELEA KULIALIA KILA KITU MNATAKA MFANYIWE.HIZO SHINGO ZENU ZIMEBEBA MAKOPO??!!
 
Kama nitapeli weka hapa ushahidi kama amewahi kukutapeli au kama upo kwenye hilo group lake.
Pengine ni wivu tu unakusumbua hujawahi kujiunga hata kwenye hilo group kama kuna watu wanatapeliwa kwanini wasiende kushitaki
 
Duh! Daniel Shila aliwatapeli watu kupitia E-FM ya majizo.

Noma sana.
 
Mkuu kwani hujui tu chanzo cha utajiri ni wajinga, wajinga ndio daraja la wachache kuwa matajiri.
 
Hao wanaotapeliwa acha waliwe tu si wana hela za kuchezea acha kijana apige hela
 

😃😃😃

Serikali haiwezi kufuatilia mambo kama hayo ambayo ni hiyari ya watu wenyewe.

Serikali haiwezi kuingilia mitazamo, hisia, mapenzi, ya watu kuhusu Jambo Fulani ikiwa inaona halileta madhara makubwa kwenye jamii.

Mfano, kuanzisha Kanisa au huduma za kinabii ni Moja ya utapeli lakini serikali haiwezi ingilia mambo hayo ambayo watu huona kama ni sehemu ya msaada kwao na huyapenda.
 
Yaani mtu awe na code ya kupata hela alafu akufundishe wewe? tena akulazimishe ujiunge?.

Vitu vingekuwa vya kweli asigeweza waambia watu.

hata hao freemason wapo kimya sio rahisi kuingia huko au kupata hela ya hivyo.


Huyo jamaa ni tapeli tu kama yule Nabii shilla .sahizi kaishiwa anapost picha za hela bandia au kama za kweli ni zakukodi kuvutia wajinga.
 
Kama nitapeli weka hapa ushahidi kama amewahi kukutapeli au kama upo kwenye hilo group lake.
Pengine ni wivu tu unakusumbua hujawahi kujiunga hata kwenye hilo group kama kuna watu wanatapeliwa kwanini wasiende kushitaki
Wanachajiwa fedha kila stage .na watu kuaminishwa watakuwa matajiri .

Ni njia ya kuwahadaa watu .
 
Tatizo ni grp la WhatsApp au tatizo ni utapeli? Kama tatizo ni utapeli hata mwamposa ni tapeli
 
Tatizo ni grp la WhatsApp au tatizo ni utapeli? Kama tatizo ni utapeli hata mwamposa ni tapeli
Bulldozer kakufanyizia Nini? Maana Ili uitwe madhabahuni kutoa shuhuda ujue umechangia vya kutosha, Ila Mzee wa rise and shine huwezi kumlinganisha na mtu aliyefungua group whatsapp
 
Nonsense,
iyo serikali iliyojaa uozo ndio ikamfuatilie Kijana wa Mwakibete? Kwa legalities zipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…