Serikali haimuoni Chief Godlove ?

Duh! Daniel Shila aliwatapeli watu kupitia E-FM ya majizo.

Noma sana.
Hata humu JF tulisha pigwa na yule jamaa aliye dai unalipa robo ya bei kitu chochote cha electronic. Pesa iliyo baki utamalizia utakapo kwenda kuchukua mzigo kwenye warehouse Kigamboni. Jamaa alijiita Mulisa.
 
Huyo ni fake influencer, lengo lake ni kupiga pesa tu. Hana tofauti na kina Andrew Tate.

Wanaanza kwa kuongea vitu vya ajabu kwenye mitandao na kupost maisha ya kifahari, kisha wanakuja kukuuzia kitu fulani.
Sema Andrew tate umekosea, pale pesa ipo.
Ana kama networth ya US 380 million!
Yule sio fake!
 
We jamaa ni mnoko, ni mkuda na una husda. Wanasiasa na (Mitume/wachungaji/freemasons/ illuminati/waganga wa kienyeji) they all fall into one category hivyo kama kushtaki if you're fair basi kashitaki wote hao.
Winning is about setting your strategies intelligently, mjini mipango mambo ya kufanya kazi kwa kutoka mijasho na kuhema ni vijijini huko labda na wabeba mizigo(makuli). Hata ughaibuni usidhani Wabongo wote ni manamba, akili kukichwa.
 
Uzuri hashikii mtu mtutu kumlazimisha kujiunga kwenye huo upuuzi wake, Acha awapige
 
Serikali gani wakati wote wako kitanda kimoja wakifanya kitu kilekile? Kwani huyu shaitwani ni wa kwanza? Umewasahau akina Getrude Rwakatare, Christopher Mwakasege, Gamanywa, Moses Kulola, Kakobe, na wengine wengi? Huwaoni akina Gwajima, Lusekelo, Mwampasa na wengine wengi wanaoendeleza libeneke?
 
Unajua upumbavu/ujinga wako ndio mtaji kwa wengine.
Wewe unakuwa ndio njia ya mafanikio ya wengine
Watu wana tapeliwa kwa njia nyingi:
1.kisiasa
2.kiuchumi (Mr.Kuku, Nguruwe, kalynda,namaingo, deci,Sir Jef, Chief Godlove, nk nk )
3.kiimani (angalia idadi ya mitume na manabii walivyo wageuza watu kuwa mifugo yao )

Leo ghafla mtu anaibuka na kujiita tajiri na kukunga kwenye ma group na kukutoza pesa.
Na wewe unatoa kwa hiari yako,
SERIKALI Hapa ifanye nini sasa?
 
ni fake.

hakuwa na utajiri mkubwa hivyo kabla ya kuanza kutapeli vijana mtandaoni

tapeli ni tapeli tu hata kama hana shida ya hela.
Si tapeli, yule alikuwa kickboxer mwenye mafanikio, alikuwa millionaire toka akiwa kickboxer.
Ana biashara nyingi. Na kiufupi "real world" ambayo wewe unaita utapeli haichangii hata 20% ya utajiri wake!
 
Ushabiwa baba yake ni lugumi bado unaongea ongea shaur yako
 
Wanamhitaji sana ili kuwaweka wapumbavu busy na matumaini hewa
 
Learn to mind your business, utafika mbali
 
1. Mwamposa
2. God Love
3. Geo Davie
4. na wengine kibaooo
Wotee ni matapeli.

Ila unakomaa na serikali amshughulikie God Love tu.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…