Serikali haiwezi kukwepa lawama ya kuadimika na kupanda kwa bei ya Saruji nchini. Waziri wa Viwanda ana kazi sana, kuna janga linatunyemelea

Hili nalo neno. Mtoa mada amefafanua vizuri kabisa. Serika itabidi ibadilishe policy ili kuendana na wakati or hii hali itakuwa ya kujirudia daily.
 
Hahahaha.. mkuu wa mkoa hawa wapo kutetea ugali wao tu, bei haiwezi kuwa stabilized na matamko. Bei inakuwa stabilised kwa ku adjust supply dynamics. Yaani ili uweze kutuliza bei ya cement ni lazima kuwe na uhakika wa supply ya cement ya kutosha, cement ikipatikana kila mahali, we unadhani ni mafanyabiashara gani huyo atakubali kuuza kwa bei kubwa ili apoteze wateja??...
 
Hapa tuseme kuanzia last year ndio matumizi ya saruji yameongezeka, kwa wingi wa miradi ya serikali ya awamu hii naamini itakuwa inachangi, lakini pia naamini wafanyabiashara wa saruji wanaweza kuwa na siri zao kama nilivyosema kwenye issue ya sukari last time.

Hawa watu mara nyingi huwa wana tabia za kununua mzigo mkubwa na kuuweka kwenye godown kuangalia upepo utavyokuwa.
 
Yaa ni kweli ndo mana umeona 2019 uzalishaji ulipanda kwa 44%. Lakini kwa issue ya wafanyabishara ku 'speculate' kwa kununua stock ya cement, tutarudi pale pale kwamba msukumo wa wewe kama mfanyabiashara ku speculate ni pale unapoona kwamba kuna uhaba, of which hiyo mtu yoyote atafanya kwa sababu binadamu wote tabia yetu ni selfishness.

Lakini nazidi kusisitiza, speculation yoyote haiwezi kufanikiwa kwenye efficiency, nikimaanisha kama unaviwanda vya kutosha na uzalishaji upo stable na unatosheleza mahitaji, hakuna mfanyabiashara hata mmoja atajisumbua kuficha stock, sijui kama umenipata hapo mkuu.
 
Kama watu wote JF wangekuwa kama wewe Naantombe Mushi basi nchi yetu ingekuwa imepiga hatua kubwa sana. Napenda watu wanaotoa hoja kwa data. Big up mkuu, nina imani kama kuna wahusika wa serikali humu basi hii changamoto wataichukua na kuifisha kwa mheshimiwa.
 
Thanks
 
Japo ni tofauti, walifanya hivyo kwenye korosho, imewafanya hata washindwe kwenda kupiga kampeni huko kunako korosho. Mimi nadhani ni kujenga urafiki na sector binafsi na kuwawezesha. serikali awe facilitator na asiwe participant
 
Asante mnama umenifungua macho, hapo kwenye makadirio ya gharama za kiwanda itakuwa nili base kwa gharama za miaka 10 iliyopita.

Nimechukua pia point kwamba viwanda vya ndani nje ya Dangote bado uzalishaji wake ni mdogo na havina uwezo wa ku ongeza output kwa haraka...

Sema pia ukiangalia hivi viwanda vina management issues za ndani, mfano kiwanda kama Tanga Cement, huu ni mwaka wa nne kinajiendesha kwa hasara.. meaning kwamba hawana internal muscles za kufanya more CAPEX na kuongeza output. Same same hata kwa viwanda vidogo kama hivo ulivovitaja vya akina Kilimanjaro cement, bado internally havijastabilize na hiyo ina impair uwezo wao wa kuzalisha
 
A good analysi kwa taaluma ya uchumi. Wanasiasa wanatumiaga maguvu kuliko kuomba ushàuri Wa kitaaluma. Wasichokijua Ni kwamba hata kama bei ya kiwandani itabaki ile ile, bado Luna gharama zinaogezeka kama vile kukaa foleni kusubiria, kutoa rushwa/hongo, umelipia mzigo Na kuchelewa kuletewa nzigo. Kwa hiyo wanasiasa wasikilize ushauri Wa kitaalamu
 

Uchambuzi makini na ushauri sahihi kwa serikali👍

Maendeleo hayana vyama

Naantombe Mushi 💥🙏
 
Kabisa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…